Thursday, February 15, 2018

WAPIGA DILI,WALA RUSHWA HAWATAKIWI CCM

 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi kata ya Kiwalani,Mathias Kahinga kulia)akizungumza na waaandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya wapigaji, wala rushwa, pamoja na wapiga dili hawana nafasi kwenye utawala wake,leo jijini Dar es Salaam.


MWENYENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya kiwalani Mathias Kahinga Amesema katika kipindicho chote cha uongozi wake wapigaji, wala rushwa, pamoja na wapiga dili hawana nafasi kwenye utawala wake nakudai mbeleko za kuwabebea zimechanika.

Amesema kwake ni kuchapa kazi aliyotumwa na wanachama wa Chama chake kwa lengo kuu la kutatua na kuisimamia Serikali huku akitoa rai kwa viongozi wezake ndani ya chama hicho kuhakikisha wanakuwa waadilifu na wenye unyenyekevu kwa wananchi na kutatua kero zao.

Mwenyekiti na kada huyo wa Chama ameyasema haya jijini Dar es salaam katika ofisi za Chama hicho Kata zilizopo Kata hiyo ya kiwalani ndani ya manispaa ya Ilalat. Ambapo amesema kwake wapiga dili na wezi hawana nafasi kabisa.

"Nilikuwa na mambo kadhaa ambayo nilihaidi kwa wanaccm wakati nautaka uwenyekiti na moja ya kazi yangu kubwa ni kurejesha mtaa mmoja wa serikali ya mtaa ambao unatawaliwa na CUF kwa miaka 15 sasa na hakuna maendeleo yeyote ndani ya mtaa huo wa kigilagila. "amesema Kahinga

Pia alisema jambo lingine ambalo alihaidi nikuona ofisi za Chama hicho zinakuwa katika mwenekano iliobora kabisa tofauti na ilivyo sasa na tayari kuna hatua mbalimbali ambazo amezichukuwa na anasubiri maombi yake ambayo ameyapeleka ngazi za juu za chama hicho.

Mwenyekiti huo ameongeza kuwa amepanga safu yake vilivyo ambayo lengo lake kubwa nikufanya kazi karibu na wananchi wa Kata hiyo ya kiwalani kwa maana ya kuisimamia serikali vilivyo ili 2019 waweze kurudisha mtaa ambao umekwenda upinzani.

Amesema inawezekana utendaji mdogo wa huko nyuma Kwa kiasi kikubwa ulichangia mtaa kwa miaka yote kuendelea kuwa chini ya Chama cha upinzani pamoja na ngazi ya udiwani."kimsingi sina muda wa kubeba wezi, na kila mmoja afanye kazi kwa moyo kama jinsi akivyoomba nafasi aliyopo na kamwe hatahitaji watu ambao hawatimizi wajibu wao. "amasema Kahinga.

Naye Katibu wa Chama hicho Kata kiwalani  Eva Malenga Amewatoa hofu wanachama wa hicho kuhusu uwepo wa tetesi ya baadhi ya maeneo yao kudaiwa ni maeneo ya wazi ya serikali nakudai kuwa madai hayo hayana hoja nakwamba wao wamefuata taratibu zote za kumiliki maeneo hayo.

Amesema kila eneo ambalo wanajuwa ni mali ya Chama chao basi wamehakikisha kila nakala inyohusu maeneo  wanafanyia kazi na kwamba taarifa zote zipo kwa viongozi husika.

Aidha akizungumzia ukakasi wa utoaji wa mikopo kutoka ngazi ya halmashauri lakini hali hiyo imeshaghulikiwa na hivi sasa mikopo hiyo inapitia ofisi za watendaji wa Mitaa ikilinganishwa na huko nyuma jinsi ilivyokuwa inatolewa huku kiongozi mmoja ngazi ya Kata akijanasibu kwamba mikopo hiyo nijitahada zake.

Akizunguzia mikakati yao kama viongozi amesema kubwa kuliko ni kuhakikisha wanashikamana ili kuweza kufanya vyema ambapo pia watendaji wanatakiwa kutimiza wajibu wao nakuona kwamba wapo kwa ajili watanzania.

Pia katibu huyo Amezungumzia kero ya maji taka ambayo yanatililika kutoka Ndani ya ujenzi wa kiwanja cha Ndege  (Airpot)unaondelea nakudai kwamba eneo hilo wameshapigia kelele sana ikiwa pamoja na kumshirikisha Mbunge lakini hadi sasa kero hiyo bado ipo.

Kwaupande wake Mwenezi wa Chama hicho kata, Haroun Muhajir. Amewataka watendaji wa Serikali kufanya kazi kwa uadilifu na kwamba watambue kuwa CCM ipo kazini nakudai wale watendaji wapiga dili na wala rushwa hawatafumbiwa macho.nakudai baadhi ya walimu walitaka kwenda kinyume na agizo la elimu bure kwa kuwatoza wanafunzi fedha sh. 500 Lakini jambo hilo wameshalimaliza.

"Tumejipanga vizuri kama Kata na kubwa nikuona kila jambo linakwenda kama linavyotakiwa japo kuna kero ya baadhi ya mitaa yetu miwili kukosekana kwa watendaji kwa maana mtaa wa kiwalani na kigilagila japo ambalo linafanya Wananchi kukosa huduma ya kiserikali kutoka kwa watendaji. ."  Amesema
Katibu wa Chama hicho Kata kiwalani,Eva Malenga Amewatoa (kushoto) akisisitiza jambo katika mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii. 


No comments: