Na Beatrice Lyimo, MAELEZO- DODOMA.
Serikali
imepokea zana za kukusanya na kutoa taarifa za watoto walio katika
mazingira hatarishi kwa ajili ya wasimamizi wa mashauri ya watoto ngazi
ya jamii inayojumuisha kata, vijiji na mitaa.
Zana
hizo zimekabidhiwa leo mjini Dodoma kwa Kamisha wa Maendeleo ya Jamii
Dkt. Naftal Ng’ondi na Shirika la John Snow Inc(JSI) kushirikiana na
MEASURE Evaluation na PACT Tanzania kupitia Mradi wa Uimarishaji wa
Mifumo ya Afya na Ustawi wa Jamii(CHSSP) unaofadhiliwa na Shirika la
Misaada la Maendeleo la Watu wa Marekani(USAID).
Wakati
wa makabidhiano hayo Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali Ng’ondi
amesema kuwa ni muhimu kupeana taarifa katika utekelezaji wa mipango
mbalimbali iliyopo ili kuwe na matumizi sahihi ya rasilimali zilizopo
hivyo zana hizo zitasaidia katika utoaji wa taarifa zilizo sahihi.
Dkt.
Naftali Ng’ondi ameongeza kuwa Serikali kupitia Idara ya Ustawi wa
Jamii itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kuhakikisha
mtoto anayeishi katika mazingira hatarishi anapata huduma stahiki.
“
Zana hizi zitasadia wasimamizi wa mashauri ya watoto ngazi ya jamii
katika kuwasaidia watoto waliopo katika mazingira hatarishi” alisema
Dkt. Ng’ondi.
Nae
Mkurugenzi wa Miradi kutoka Shirika la John Snow Inc (JSI) Dkt. Tulli
Tuhuma amesema kuwa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Afya na Ustawi wa
Jamii unaosimamia na JSI unalengo la kuimarisha mifumo ya Afya na Ustawi
wa Jamii.
“Zana
hizi tisa ni matokeo ya ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na
Shirika la Misaada la Maendeleo la Watu wa Marekani USAID na mfuko wa
dharura wa Rais wa Marekani wa UKIMWI na zitawasaidia wasimamizi wa
mashauri ya watoto kuweka kumbukumbu na kufuatilia mashauri ya kiulinzi,
ustawi wa jamii na afya katika halmashauri na kutoa huduma pamoja na
rufaa kwa watoto walio katika mazingira hatarishi”alisema Dkt. Tulli.
Aidha,
Dkt. Tulli ameongeza kuwa awali kulikuwa na muingiliano wa katika
utoaji wa huduma na kusababisha ugumu katika kufanya ufuatiliaji wa
huduma na upatikanaji wa takwimu.
Kamishna
wa Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali Ng’ondi akifungua kikao cha
makabidhiano ya zana za kukusanya na kutoa taarifa za watoto walio
katika mazingira hatarishi kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina leo
Februari 14,2017 mjini Dodoma.
Kamishna
Msaidizi wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi(kulia) akimpongeza
Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali Ng’ondi (kushoto)baada ya
kufungua kikao cha makabidhiano ya zana za kukusanya na kutoa taarifa
za watoto walio katika mazingira hatarishi kilichofanyika katika Ukumbi
wa Hazina leo Februari 14,2017 mjini Dodoma.
Meneja
Miradii wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) Bw. Grey Saga
akizungumzia miradi inayofadhiliwa na Shirika hilo wakati wa Kikao cha
Makabidhiano ya zana za kukusanya na kutoa taarifa za watoto walio
katika mazingira hatarishi kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina leo
Februari 14,2017 mjini Dodoma.
Mkurugenzi
wa Miradi JSI Dkt. Tulli Tuhuma akitoa maelezo kuhusu umuhimu wa zana
za kukusanya na kutoa taarifa za watoto walio katika mazingira hatarishi
katika makabidhiano ya zana hizo katika halfa iliyofanyika katika
Ukumbi wa Hazina leo Februari 14,2017 mjini Dodoma.
Sehemu
ya washiriki wakifuatilia mada mbalimbali katika Kikao cha
makabidhiano ya zana za kukusanya na kutoa taarifa za watoto walio
katika mazingira hatarishi kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina leo
Februari 14,2017 mjini Dodoma.
Kamishna
wa Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali Ng’ondi akikata utepe kuzindua zana za
kukusanya na kutoa taarifa za watoto walio katika mazingira hatarishi
katika hafla ya makabidhiano ya zana hizo katika Ukumbi wa Hazina leo
Februari 14, 2017 mjini Dodoma.
Kamishna
wa Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali Ng’ondi pamoja na wadau wakionesha
zana za kukusanya na kutoa taarifa za watoto walio katika mazingira
hatarishi katika picha ya pamoja na wadau hao mara baada ya Kikao cha
makabidhiano ya zana hizo kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina leo
Februari 14,2017 mjini Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
No comments:
Post a Comment