WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetumia sh. bilioni 161.9
kuboresha vituo vya afya 170 nchini pamoja na kugharamia huduma ya Afya
ya Mama na Mtoto kwa lengo la kuokoa maisha yao.
Amsema
Serikali itaendelea kukarabati na kupanua miundombinu ya kutolea huduma
pamoja na kununua vifaa vya kisasa katika Hospitali za Mloganzila,
Benjamini Mkapa, Dodoma na Hosptali za Rufaa katika Mikoa na Kanda.
Waziri
Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Februari 14, 2018) wakati akizindua
jengo jipya la mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa-Amana
iliyopo wilayani Ilala jijini Dar es Salaam.
Jengo hilo la ghorofa mbili limejengwa kwa ufadhili wa kundi la kampuni za AMSONS na lina thamani ya sh bilioni 1.2.
Amesema
uzinduzi wa jengo hilo unakwenda sambamba na azma ya Rais Dkt. John
Magufuli za kuimarisha sekta ya afya na kuifanya kuwa miongoni mwa sekta
za kipaumbele.
Amesema
lengo la Serikali ni kuhakikisha inasogeza huduma za afya karibu na
wananchi. “Mfano, Hospitali za Rufaa za Amana, Mwananyamala na Temeke,
zimeendelea kuhudumia wagonjwa kutoka Zahanati, Vituo vya Afya vya
Serikali, binafsi na vya dini kutoka mikoa jirani ya Pwani, Morogoro na
Lindi.
Pia
amesema Serikali itaendelea kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015 – 2020, kuhusu kuwapatia wananchi huduma
bora za afya pamoja na kujenga hospitali nyingine za Rufaa kwa ajili ya
Kanda ya Kusini, Kati na Magharibi.
Akizungumzia
kuhusu changamoto ya idadi ndogo ya watumishi na ukosefu wa huduma za
uangalizi maalumu (ICU) katika hospital ya Amana, Waziri Mkuu amesema
Serikali inaendelea kufanyia kazi changamoto zote zilizopo katika sekta
ya afya zikiwemo n aza hospital hiyo.
Waziri
Mkuu amesema Serikali itaendelea kuthamini na kutambua mchango wa wadau
mbalimbali pamoja na kuendelea kushirikiana nao katika kuhakikisha kuwa
huduma za afya nchini zinaboreshwa.
Hivyo,
alitumia fursa hiyo na kulipongeza kundi la kampuni za AMSON’s
lililoamua kujenga jengo la mama na mtoto katika hospital hiyo kwa
ushawishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda.
Awali,
Mganga Mkuu Hospitali ya Rufaa ya Mkoa – Amana, Dkt. Meshack Shimwella
alisema wazazi wanaolazwa katika hospitali hiyo kwa siku ni 180 hadi 250
na uwezo wa hospitali ni vitanda 353, ambapo vitanda 250 vinatumika
wodi ya wazazi.
Alisema
idadi hiyo hailingani na idadi ya wagonjwa, hivyo kusababisha wakati
mwingine wagonjwa kulala zaidi ya mmoja kwenye kitanda kimoja kutokana
na kasi ya ongezeko wa wagonjwa wanaolazwa hususani wodi ya watoto na
akinamama.
Dkt.
Shimwella alisema wamefanikiwa kuongeza jingo la kutolea huduma ya mama
na mtoto lenye ghorofa mbili ilililojengwa kwa ufadhili wa AMSONS lenye
uwezo wa vitanda 100, ambalo ndilo liliongeza idadi ya vitanda kutoka
253 hadi kufikia 353.
“Kutokana
kukamilika kwa jengo hilo kwa sasa akinamama wanaonyonyesha wanalala
wakiwa mmoja mmoja, watoto wachanga wanahudumiwa katika mazingira mazuri
yanayofanana na viwango Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto.”
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Makonda aliwashukuru
wafadhili waliojenga jengo hilo kwa sababu si kila mtu anayekwenda
hospitali na kukuta changamoto na akaamua kuzifanyia kazi.
Bw.
Makonda alisema awali akinamama walikuwa wanalala hadi watatu katika
kitanda kimoja, hivyo madhumuni ya ujenzi wa jego hilo ni kupunguza
msongamano katika wodi ya wazazi.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, FEBRUARI 14, 2018.
No comments:
Post a Comment