Thursday, February 8, 2018

MKUU WA WILAYA YA KIBAHA ASSUMPTER MSHAMA ATOA SIKU TISINI KWA MWEKEZAJI KURUDISHA HEKARI 5000 KWA WANANCHI WA KIJIJI CHA LUKENGE

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama akizungumza na umati wa wananchi wa kijiji cha Lukenge kata Magindu hawapo pichani katika mkutano wa adhara ambao aliuandaa kwa ajili ya kuweza kutatua mgogoro wa aradhi kati ya wananachi hao na mwekezaji ambao umedumu kwa kipindi kirefu
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama akiwa anatoka kwenye mkutano na wananchi wa kijiji cha lukenge alipokwenda kwa ajili ya kumaliza sakata la mgogoro baina ya wananachi hao pamoja na mwekezaji.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha lukenge wakiwa wanamsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama wakati wa mkutano wa adhara ambao uliandaliwa kwa ajili ya kusikiliza mgogoro uliopo katia ya wananchi na mwekezaji.
Wananchi wa kijiji cha lukenge wakiwa wameshika mabango yaliyokuwa yameandikwa ujumbe wa kumkataa mwekezaji huyo, ambapo walipita mbele kwa ajili ya kuweza kumuonyesha Mkuu wa Wilaaya ya Kibaha.
PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGUNA VICTOR MASANGU, KIBAHA PWANI

SERIKALI wilayani Kibaha,Mkoa wa Pwani imemtaka mwekezaji ambaye alichukua eneo lenye ukubwa wa hekari zipatazo 5000 za ardhi bila ya kuzingatia sheria na taratibu kuzirudisha kwa kipindi cha siku tisini kutokana na kushindwa kuliendeleza kwa kipindi cha zaidi ya miaka nane kama walivyokubaliana katiba mkataba na wananchi wa kijiji cha lukenge kata ya Magindu.


Sakata la mgogoro wa ardhi baina ya wananchi hao na mwekeaji limechukua sura mpya kufuatai Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi hivyo kumtaka mwekezaji huyo kuzirudisha hekari hizo 5000 kwa wananchi ambazo alikuwa amepewa na serikali ya kijiji kwa ajili ya uwekezaji wa ufugaji wa kisasa wa ng’ombe pamoja na samaki lakini ameshindwa kutekeleza makubaliano aliyopatiwa hapo awali.


Akizungumza katika mkutano maalumu wa adhara ambao uliandaliwa kwa ajili ya kujadili sakata hilo Mkuu huyo wa Wilaya amesema eneo hilo mwekezaji huyo alipewa kwa ajili ya kuliendeleza lakini amekuwa akijinufaisha mwenywe na kuwanyonya wakazi wa eneo hilo bila ya kuwaletea maendeleo ya aina yoyote tofauti na makubaliano yao.


Kwa upande wake aliyekuwa Mwenyekiti wa zamani wa kijiji hicho cha Lukenge Seif Maleta ambaye kwa sasa amemaliza muda wake amesema kwamba eneo hilo la hekari 5000 hawakumuuzia mwekezaji huyo ila walimpatia kulitumia kwa muda tu kwa ajili ya kuweza kufanyia shughuli zake mbali mbali za ufugaji wa ng’ombe na samaki kwa makubaliano maalumu.

Naye mwekezaji huyo ambaye analalamikiwa na wananchi anayejulikana kw ajina la Tangono Kashima alisema kwamba eneo hilo la uwekezaji wa ng’ombe alilipata kwa kuzingatia taratibu za serikali ya kijiji kwa kuandika barua maalumu kwa ajili ya kuomba eneo hilo kwa ajili ya kufuga ufugaji wa kisasa wa ng’ombe pamoja na kuchimba bwawa kwa ajili ya ufugaji wa samaki

ENEO hilo la ardhi lililopo katika kijiji cha lukenge kata ya magindu katika halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani lina ukumbwa wa hekari zipatazo 5000 na kwa sasa limeingia katika mgogoro mkubwa baina ya wananchi pamoja na mwekezaji huyo kutokana na kukiuka kanuni na sheria za umiliki wa ardhi.

No comments: