Tuesday, February 6, 2018

MKUU WA MAJESHI YA ULINZI AITAKA GOLF LUGALO KUREJESHA HESHMA YA JESHI MICHEZONI

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akisalimiana na Wachezaji wa Timu ya Wanawake ya Klabu ya Gofu ya jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo inayotarajia kushiriki mashindano ya Wazi ya Wanawake ya IBB nchini Nigeria Hivi karibuni
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akimkabidhi Bendera ya taifa Nahodha wa Timu ya Wanawake ya Klabu ya Gofu ya jeshi la ulinzi la Wananchi wa tanzania ya Lugalo inayotarajia kushiriki mashindano ya Wazi ya Wanawake ya IBB nchini Nigeria Hivi karibuni
Mwenyekiti wa wa Chama cha Gofu nchini Joseph tango (Aliyesimama) akizungumza wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari makao makuu ya jeshi Upanga ambapo Timu ya Wanawake ya Klabu ya jeshi ya Lugalo walikabidhidhwa bendera kwa Ajili ya kushiriki Michuano ya Wazi nchini Nigeria aliyeka Kushoto ni Mwenyekii wa Lugalo Brigedia Jenerali Michael Luwongo Mstaafu.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akiwa katika Picha ya Pamoja na Wachezaji na Viongozi wa Klabu ya Gofu ya jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo Wakuu wa Matawi na Wachezaji wanaotarajia kushiriki mashindano ya Wazi ya Wanawake ya IBB nchini Nigeria Hivi karibuni (Picha na Luteni Selemani Semunyu



Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo amewataka wachezaji wa Timu ya Wanawake ya Gofu ya Klabu ya Jeshi ya Lugalo kuhakikisha wanarejesha heshma ya jeshi kuwa kinara katika michezo na kuzalisha wachezaji bora wanaowakilisha nchi kwa mafaniko.

Aliyasema hayo Makao Makuu ya jeshi Upanga Jijini Dar es Salaam wakati akiagana na wachezaji Sita wa Gofu wanaotarajia kuwakilisha nchi katika michuano ya wazi ya wanawake nchini Nigeria IBB Ladies Open Championship 2018 yanayaotarajia kufanyika hivi karibuni.

Jenerali Mabeyo alisema kama ilivyokuwa katika Michezo ya Riadha na Ngumi sasa tunataka na kwenye gofu na kwa kuanza ni timu hii ya Gofu ya Wanawake kuhakikisha inarudi na ushindi mnono.

“ Nikiwa mlezi wa Klabu naamini mtatuwakilisha vyema na Jeshi kwa ujumla tutaendelea kuwaunga mkono wachezaji wa Gofu na hata Michezo mingine kuhakikisha jeshi linaendelea kuwa kinara w michezo nchini na kuwa chachu kwa wengine” Alisema Jenerali Mabeyo.

Aliongeza kuwa licha ya matumaini yake katika Gofu lakini pia katika Soka licha ya Mchezo huo kutawaliwa na simba na yanga lakini sasa walau mwanga unaonekana baada ya ya Timu ya Jeshi ya Green Worriorrs kuifurusha Timu ya Simba katika Michuano ya Kombe la Shirirkisho.

“Ushindi ule ulikuwa Mwanzo mzuri wa kupunguza Ubabe wa Simba na Yanga na Ushabiki wa Simba na Yanga hata miongoni mwa Wachezaji hivyo nanyi kama mlivyofanya vyema katika mashindano Uganda sasa tunatarajia Ushindi toka Nigeria” Alisema Jenerali Mabeyo.

Kwa Upande wa mwenyekiti wa Klabu hiyo Brigedia Jenerali Michael Luwongo Mstaafu aliwataja wachezaji hao kuwa ni Nahodha Ayne Magombe, Sara Denis , Sophia Mathius ,Hawa Wanyenche ,Christina Charles na Angel Eaton huku mkuu wa Msafara akiwa ni Kapten Japhet Masai.

“ Nina matumaini makubwa na Kikosi hiki tunachokituma Nigeria naamini kitarejesha furaha kwa Klabu ,jeshi na Watanzania kwa ujumla ukizingatia uwezo Binafsi wa Wachezaji Mazoezi na Historia kutokana na michuano iliyotangulia” Alisema Brigedia Jenerali Mstaafu Luwongo.

Kwa Upande wake mwenyekiti wa Chama cha Gofu nchini TGU Joseph tango amelipongeza jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania kwa jitihada katika kuendeleza michezo hasa mchezo wa gofu ambao klabu ya Lugalo imekuwa kielelezo.
Aliomba mkuu wa majeshi ya ulinzi na Mlezi wa Klabu ya Lugalo kuendelea kuisaidia Klabu hiyo ambayo ndio klabu yenye mashindano mengi kwa mwaka ukilinganisha na Klabu nyingine nchini ikiwemo kusaidia utekelezaji wa Ujenzi wa Uwanja makao makuu ya nchi Dodoma.

Mashindano hayo ya Siku Tatu yanatarajiwa kuanza Tarehe Nane Februari huku wachezaji kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Kenya,Uganda, Zambia na Malawi wakitarajiwa kushiriki.

No comments: