Thursday, January 18, 2018

KAMISHNA GASTON SANGA AMWAKILISHA KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA KUFUNGUA MAFUNZO YA MAAFISA VIUNGANISHI WA UTUNZAJI WA TAKWIMU

Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza, Afande Gaston Sanga (aliyevaa suti) akiingia Makao Makuu ya Envirocare na kupokewa na Mgurugenzi wa kituo hicho Bi Loyce Lema (wa pili toka kushoto). Wa kwanza kulia ni Meneja mradi bi Catherine Jerome na wa kwanza kushoto ni mwanasheria wa Jeshi la Magereza Makao Makuu, Mkaguzi Msaidizi Hobokela Mwansumbule.
Kamishna Gaston Sanga akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkurugenzi wa Envirocare huku Mkurugenzi Bi Loyce Lema akishuhudia.
Mkurugenzi wa Envirocare Bi Loyce Lema akitoa maelezo mafupi ya historia ya Envirocare kabla ya kumkaribisha Afande Kamishna Gaston Sanga kutoa hotuba ya Kamishna Jenerali wa Magereza na kufungua rasmi mafunzo ya siku tatu kwa wataalamu wapya wa Utunzaji wa Takwimu katika Mradi wa Msaada wa Kisheria Magerezani


Kamishna Sanga akitoa Nasaha za Kamishna Jenerali wa Magereza kabla ya kufungua rasmi mafunzo ya wataalam wapya Utunzaji wa Takwimu ambayo yanafanyika Makongo juu jijini Dar es Salaam kwenye ofisi Envirocare
Meneja Ufuatiliaji na Tathmini wa Envirocare Bi Salome Kisenge akiwa darasani akiwafundisha wataalamu wapya wa Utunzaji wa Takwimu katika Mradi wa Msaada wa Kisheria Magerezani
Meneja Mradi wa Envirocare, Bi Catherine Jerome (aliyesimama) akitoa maelezo mafupi kuhusu mradi wa Envirocare na changamoto zake kwa Kamishna Gaston Sanga.
Afisa Mradi wa Envirocare , ndugu Antony Mlelwa (Mwenye shati jeupe) akifungua na kumkabidhi kompyuta Afande Kamishna Gaston Sanga huku Mkurugenzi na Meneja Mradi wakishuhudia. Kompyuta hizo zitatumika kuhifadhia Taarifa na Takwimu kwa wataalam wapya wa katika Mradi wa Msaada wa Kisheria Magerezani.
Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Magereza Afande Gaston Sanga( wa pili kulia), Mkurugenzi wa Envirocare Bi Loyce Lema (wa pili kushoto) ,Meneja Mradi Bi Catherine Jerome( wa kwanza kulia) na Mwanasheria wa Jeshi la Magereza Makao Makuu, Mkaguzi Msaidizi Hobokela Mwansumbule(wa kwanza kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya Utunzaji wa Taarifa na Takwimu.


Picha zote na Makao Makuu ya Magereza kitengo cha Habari

No comments: