Monday, December 11, 2017

WAZIRI UMMY AFANYA Ziara Zahanati ya Mhandu na Segese wilayani Msalala


Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto akimkabidhi kitambulisho cha matibabu bila ya malipo mmoja wa wazee wa kijiji cha Segese Bibi. Shija Petro (60) kulia wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama leo ili kuangalia utekelezaji wa mpango wa malipo wa ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi, Bibi huyo aliwawakilisha wazee 413 waliopata vitambulisho hivyo katika Halmashauri ya Msalala ambapo lengo ni kuwafikia wazee742 kufikia Machi 2018.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto akimsalimia mgonjwa aliyekuwa anasubiri huduma katika Zahanati ya Segese wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama leo ili kuangalia utekelezaji wa mpango wa malipo wa ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akisisitiza jambo kuhusu upatikanaji wa dawa katika Zahanati ya Mhandu wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama leo ili kuangalia utekelezaji wa mpango wa malipo wa ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi.
Baadhi ya Wanakijiji wa Kijiji cha Segese wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu hayupo pichani wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama leo ili kuangalia utekelezaji wa mpango wa malipo wa ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akiangalia friji la kuhifadhia chanjo kwa ajili ya watoto katika Zahanati ya Segese wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama leo ili kuangalia utekelezaji wa mpango wa malipo wa ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kulia akipata maelekezo juu ya upatikanaji wa dawa kutoka kwa mtoa huduma kushoto katika Zahanati ya Segese wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama leo ili kuangalia utekelezaji wa mpango wa malipo wa ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto akifurahia jambo na baadhi ya wazee wa kijiji cha Segese wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama leo ili kuangalia utekelezaji wa mpango wa malipo wa ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi.PICHA NA WIZARA YA AFYA –KAHAMA.
……………
Na.WAMJW-Msalala

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto aweka historia kwa kutembelea Zahanati ya Mhandu kata ya Chela Wilayani Msalala ambapo tangu Uhuru wa Tanzania kijiji hicho hakijawahi kutembekewa na Kiongozi wa Kitaifa.

Waziri Ummy Mwalimu yupo ziara ya kikazi Wilayani Msalala kujionea Utekelezaji wa Mpango wa Malipo kwa Ufanisi(RBF) ambapo ulianza Januari 2016 kwa Mkoa wa Shinyanga

RBFni Mpango wa malipo wa ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya ngazi ya msingi ambapo vituo vinapewa maeneo ya utekelezaji na kupimwa kuona kama wamekidhi na kufikiwa malengo hivyo kituo huhakikiwa na hatimaye kutolewa fedha kulingana na matokeo ya idadi za huduma zilizotolewa na ubora kulingana na miongozo ya utoaji wa huduma za Afya.

Fedha zinazopatikana zinafanya maboresho ya vituo ikiwemo miundombinu ya kituo,madawa na vifaa tiba

Waziri Ummy Mwalimu ameipongeza halmashauri ya wilaya hiyo kwa kufanya vizuri katika kutekeleza Mpango huo hata hivyo aliwataka watendaji kufanya uhakiki na kujiridhisha kwamba huduma za Afya zitolewazo zinakidhi viwango kulingana na miongozo ya Afya ndipo malipo yatolewe

Alisema Mpango huo unahakikisha huduma ya Afya ya msingi zinatolewa bila vikwazo,”nimekuja kufuatilia utekelezaji kwakweli nimefurahi kwani mnatekeleza na mmeboresha huduma zenu”

Aidha,alisema kabla ya utekelezaji wa Mpango huo kuanza mwaka 2015 hali ya miundombinu ilikua mibovu,hakukuwa na dawa,hivyo kupitia Mpango huo Serikali hupeleka fedha ambazo zinasaidia kuimarisha mifumo ya vituo vya Afya,kuongeza huduma za huduma,kuchochea jamii kutumia vituo vya Afya hususan wanawake wajawazito pamoja na kutoa motisha kwa wahudumu na watumishi wa Afya katika vituo vya kutolea huduma.

“Mpango huu tunataka wanawake wajawazito waje vituoni ndani ya miezi mitatu ya mwanzo na serikali tunaleta shilingi 8290,na mjamzito akihudhuria kliniki angalau Mara NNE wakati wa ujauzito tunaleta shilingi 6210 kwenye zahanati” alisema Waziri Ummy

Alitaja kiasi cha shilingi 20,700 serikali inatoa kwa mjamzito akienda kujifungua kwenye Zahanati hivyo alitoa ari kwa wanawake wajawazito wilayani Msalala kuacha kwenda kujifungua kwa wakunga wa jadi kwani Serikali ya awamu ya tano imeboresha huduma za Afya nchini ikiwemo hali ya upatikanaji wa dawa ambapo Msalala kwa mwaka wa fedha 2017/2018 wametengewa shilingi milioni 417 tofauti na ile ya mwaka 2015/2016 ya shilingi milioni 108.

No comments: