Monday, December 11, 2017

UZINDUZI WA WIKI YA NENDA KWA USALAMA MKOA WA GEITA

Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita aliyevaa koti la rangi ya dhambarau na miwani akipata maelezo juu ya matumizi ya kamera za barabarani kutoka kwa Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Geita, Mkaguzi wa Polisi Mark Thomas Masawe wakati wa ukaguzi wa mabanda ya maonyesho katika maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama mkoani humu.
ofisa wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) Hagai Ruben akitoa maelezo kuhusu ukataji wa leseni za usafirishaji kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Robert Gabriel wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani iliyofanyika kimkoa katika Mji Mdogo wa Katoro Geita.
Wataalam wa Jeshi la Zima Moto na Wokozi Mkoa wa Geita wakiwaeleza wajumbe wa Baraza la Usalama barabarani la Mkoa wa Geita juu ya matumizi mbalimbali ya mitungi yenye Gesi ya kuzima moto wakati wajumbe hao walipotembelea banda la kikosi hicho.
Emmanuel Chacha mtaalam kutoka Kampuni ya uchimbaji wa Dhahabu ya Geita (GGML) akitoa maelezo kuhusu matumizi ya vifaa vya wokozi katika maeneo ya migodi kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita na wajumbe wa baraza la Usalama barabarani .
Wanafunzi wa Shule za Msingi za Mji wa mdogo wa Katoro wakiwa katika maandamano ya maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani Mkoani Geita.
Maandamano ya maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa usalama barabarani yakipita mbele ya Mgeni rasmi (hayupo kwenye picha).
Waendesha Piki Piki maarufu kama boda boda wakiwa katika maandamano ya maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani iliyofanyika Katoro Geita.
Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa Geita akimpongeza Alfred Hussein Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Geita wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani Mkoani Geita.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Robert Gabriel akihutubia wananchi(awapo katika Picha) wakati wa wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama barabarani Mkoani Geita.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Mponjoli Mwabulambo akizungumza na wanahabari baada ya uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama barabarani Mkoani Geita. (PICHA ZOTE NA BALTAZAR MASHAKA)

No comments: