Madaktari na watoa huduma za afya kutoka mikoa ya nyanda za juu Kusini, waliokuwa wakishiriki mafunzo ya wiki moja ya kufanya tathmini kwa mfanyakazi aliyeumia mahala pa kazi, wakionyesha stika watakazobandika maofisini kwao, zikionyesha ofisi ya mtoa huduma, mwishoni mwa mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF na kufanyika jijini Mbeya Desemba 15, 2017.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
KAIMU
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Dkt. Yahya Msuya, (pichani juu), amewataka
madaktari na watoa huduma za afya, waliokuwa wakishiriki mafunzo ya wiki moja
ya kufanya tathmini ya ulemavu kwa wafanyakazi watakaoumia au kuugua kutokana
na kazi zao, kutumia elimu waliyoipata kwa ufanisi na weledi.
Akifunga
mafunzo hayo ya siku tano yaliyoratiubiwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), ili
kuwajengea uwezo wataalamu hao wa afya, Dkt. Msuya alisema, ni ukweli kwamba
Mfuko wa WCF hauna muda mrefu tangu uanzishwe na serikali na kwa mantiki hiyo,
mkakati wa mafunzo ni muhimu ili kuhakikisha kwamba wadau wote wanaonufaika
au kuwajibika na Mfuko kuelewa shughuli zake na kuhakikisha kwamba lengo la
kuanzishwa kwa Mfuko huo linatimia.
“Nahakika
katika kipindi hiki mlichokuwepo hapa mtakuwa mmejifunza mambo mengi mapya na
kuwapa ujuzi ambao huenda hamkuwa nao wakati mnakuja hapa.” Alsiema Dkt. Msuya.
Kwa
upande wake, Mratibu wa mafunzo hayo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tiba na
Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar, alisema, lengo kuu ni kuwaelimisha
madaktari kufanya tathmini ya ulemavu kwa wafanyakazi watakaoumia au kuugua
kutokana na kazi zao kwenye maeneo yao ya kazi ili kutoa mapendekezo kwa Mfuko
kwa ajili ya uamuzi wa mwisho wa kutoa fidia. “Washiriki 85 kutoka mikoa ya
kanda ya nyanda za juu kusini wameshiriki na tuna hakika pamoja na elimu waliyoipata lakini pia watakuwa mabalozi wetu
wazuri watakaporejea kwenye maeneo yao ya kazi.” Alisema Dkt. Omar.
Naye
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano WCF, Bi. Laura Kunenge, amesema, kila mshiriki
amepatiwa cheti cha ushiriki na stika atakayokwenda kuibandika kwenye ofisi
yake kwa nia ya utambuzi wa mtoa huduma ya tathmini.
“Stika
hizi zinamuelekea mteja kuwa ofisi hiyo anapatikana daktari aliyepatiwa mafunzo
ya kufanya tathmini ya mfanyakazi aliyeumia au kupata maradhi mahala pa
kazi.”Alifafanua Bi. Laura.
Naye mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, Dkt. Mertson Mgomale, amesema, binafsi amepata faida kubwa kwani sasa anaelewa kutofautisha kiwango cha madhara aliyoyapata mfanyakazi aliyeumia kutokana na tathmini atakayomfanyia. “tulikuwa tunampima mgonjwa kama wagonjwa wengine, lakini kuchunguza viwango vya kuumia hiyo haikuwepo lakini kwa mafunzo haya sasa nimeelewa ni jinsi gani naweza kumfanyia tathmini mfanyakazi aliyeumia wakati akitekeleza wajibu wake kazini.” Alisema mshiriki huyo.
Mafunzo
hayo ni mkakati wa Mfuko kupanua mtandao wa watoa huduma ya tathmini nchi nzima
ili hatimaye Mfanyakazi aliyeumia aqweze kuhudumiwa kwa kufanyiwa tathmini
iliyo sahihi kwa mafao ya fidia sahihi. Hadi sasa ukiachilia mbali madaktari
hao 85 wakiwemo watoa huduma za afya, jumla ya madaktari 504 kutoka mikoa yote
Tanzania Bara wamepatiwa mafunzo hayo.
Mgeni rasmi Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Dkt. Yahya Msuya, (wapili kulia), akimkabidhi cheti cha ushiriki Dkt. Rehema Mwanga. wanaoshuhudia ni Mratibu wa mafunzo, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tiba na Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar, (kulia), na kiongozi wa timu ya wawezeshaji, Daktarin bingwa na mbobezi wa mifupa na viungo, Dkt. Robert Mhina.
Washiriki wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasilianoi WCF, Bi. Laura Kunenge, (kulia), akimkabidhi cheti mmoja wa washiriki, Dkt. Gloria Mbwile, ambaye ni mganga mfawidhi hospitali ya mkoa wa Mbeya.
Dkt. Ali Mtulia kutoka WCF akitoa mada mwishoni mwa mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki.
Baadhi ya washiriki.
Mgeni rasmi, Kaimu Mganga Mkuu, Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Dkt. Yahya Msuya, (katikati), Mkurugenzi wa Tiba na Tathmini, WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar, (kulia) na Mkuu wa timu ya wawezeshaji wa mafunzo hayo, Daktari bingwa na mbobezi wa mifupa na viungo, Dkt. Robert Mhina.
Mgeni rasmi Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Dkt. Yahya Msuya, (wapili kulia), akimkabidhi cheti cha ushiriki Dkt. Hassan Y. Lumbe. wanaoshuhudia ni Mratibu wa mafunzo, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tiba na Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar, (kulia), na kiongozi wa timu ya wawezeshaji, Daktarin bingwa na mbobezi wa mifupa na viungo, Dkt. Robert Mhina.
Mgeni rasmi Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Dkt. Yahya Msuya(wapili kushoto), akiongozana kutoka kushoto, Dkt. Mhina, Dk. Hussein, na Dkt. Omar.
Picha ya pamoja kundi la kwanza
Picha ya pamoja kundi la pili.
Dkt. Msuya akiagana na Dkt. Omar baada ya shughuli hiyo. Kulia mni Dkt. Mhina.
Dkt. Msuya akiagana na Dkt. Mtulia baada ya shughuli hiyo. Katikati ni Dkt. Omar.
No comments:
Post a Comment