Wednesday, December 20, 2017

ACACIA YAFANYA TAMASHA LA AJIRA KUWAPA FURSA WAFANYAKAZI WALIOACHISHWA KAZI MIGODI YA BUZWAGI NA BULYANHULU




Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Acacia kupitia migodi ya dhahabu ya Buzwagi na Bulyanhulu imefanya tamasha la ajira kwa kuwakutanisha waliokuwa wafanyakazi wa migodi hiyo na makampuni zaidi ya 20 kwa ajili kubalishana mawazo na kupeana mawasiliano na taarifa ili wafanyakazi hao wapate kazi.

Tamasha hilo limefanyika leo Jumatano Desemba 20,2017 katika ukumbi wa Umoja uliopo katika mgodi wa Buzwagi uliopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkufunzi katika Idara ya Saikolojia ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dk Chris Mauki.

Akizungumza wakati wa tamasha hilo,Meneja wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu Benedict Busunzu alisema lengo la tamasha la ajira lilioandaliwa na Acacia ni kuwaonesha fursa za ajira waliokuwa wafanyakazi wa kampuni ya Acacia kwa kuwakutanisha na makampuni mbalimbali katika kipindi cha kuelekea kufunga migodi hiyo.

“Tumekutana hapa ili kuonesha fursa za ajira kwa wafanyakazi wetu waliobobea katika kazi za migodini, kuna maisha mengine baada ya mgodi,tumealika kampuni ambayo yanachukua mawasiliano na CV na kama kuna nafasi za ajira basi watapatia ili maisha yaendelee nje ya mgodi”,aliongeza Busunzu.

“Tulialika makampuni zaidi ya 40, 15 yalikubali kushiriki,na 11 leo yamehudhuria,lakini pia wafanyakazi zaidi ya 260 wamehudhuria kwa ajili ya kuonana na makampuni haya,Acacia inaamini tamasha hili litakuwa na mafanikio makubwa tuliyotarajia”,alieleza.

Aidha Busunzu alisema kupitia program yao ‘No Harm 2020’ yenye miradi 10,wamekuwa wakitoa elimu na mafunzo mbalimbali kwa wafanyakazi wao kuhusu namna ya kuishi baada ya kumaliza muda ajira mgodini ambapo wafanyakazi 800 katika mgodi wa Bulyanhulu na 600 katika mgodi wa Buzwagi wamepatiwa mafunzo ya ujasiriamali na ajira.

Kwa upande mgeni rasmi Dk Chris Mauki ambaye ni Mkufunzi katika Idara ya Saikolojia ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam aliipongeza Acacia kwa kuwaandaa wafanyakazi wake kwa kuwapatia mafunzo ya namna ya kuishi baada ya migodi kufungwa huku akiwataka kukubali mabadiliko na kuthubutu kufanya kazi nyingine badala ya kukata tamaa.

“Mnayo nafasi ya kufanya biashara,kuajiriwa,kujiajiri na kuajiri wengine, ,mnachotakiwa kufanya ni kujitambua,kukubali mabadiliko,kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha,muishi maisha ya kuokoa muda,kuweni na mahusiano mema na watu wanaowazunguka na hapo ndipo mtakubaliana nami kuwa kuna maisha baada ya mgodi”,aliongeza Dk. Mauki.

Nao washiriki wa tamasha hilo waliishukuru Acacia kuwakutanisha na makampuni hayo kwani wamewapa urahisi wa kutafuta kazi kwa kukutana na waajiri moja kwa moja na kuwapatia taarifa zao (CV).

Nayo makampuni hayo yalisema Acacia ina wafanyakazi wazoefu na waliobobea katika kazi za migodini hivyo yanaamini yatapata wafanyakazi wazuri watakaowatumia kwenye makampuni yao.

“Acacia ni kampuni kubwa ya kimataifa, hii ni sehemu nzuri ya kupata wataalamu wanaojua kazi vizuri”,alisema Kaimu Meneja rasilimali watu kutoka shirika la Madini la taifa- STAMICO Lameck Kabeho na Jolene Ngaluko Mtalo kutoka Wakala wa ajira. –CV People Africa.

Naye Meneja wa Huduma na Mahusiano wa Acacia, Elias Kasitila alisema mpaka sasa wafanyakazi 3000 wameachishwa kazi katika migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu na zoezi la kupunguza wafanyakazi bado linaendelea katika mgodi wa Buzwagi hivyo idadi itaongezeka.

Kasitila aliyataja makampuni yaliyoshiriki katika tamasha hilo kuwa ni Twiga Cement,Mantrac Tanzania Ltd,Northern Engineering,SAO Hill,Shanta Gold mine,IMED,LINDAM,CV People,Junior Construction,Sandvick na STAMICO.

Mgeni rasmi Mkufunzi katika Idara ya Saikolojia ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dk Chris Mauki akizungumza katika Tamasha la Ajira lililoandaliwa na Kampuni ya Uchimbaji madini ya dhahabu ya Acacia lililofanyika leo Jumatano Desemba 20,2017 katika mgodi wa Buzwagi na kukutanisha pamoja makampuni zaidi ya 10 na wafanyakazi zaidi ya 260 walioachishwa kazi katika mgodi wa Buzwagi na Bulyanhulu wakati Acacia ikielekea kufunga migodi hiyo.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog



Dk Chris Mauki akizungumza katika Tamasha hilo la Ajira.Kulia ni Meneja wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu Benedict Busunzu.
Meneja wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu Benedict Busunzu akielezea lengo la kufanya tamasha la ajira lililokutanisha pamoja makampuni na wafanyakazi wa Acacia ili kupeana fursa za ajira. Kulia Meneja Uendelevu mgodi wa Buzwagi George Mganza,kushoto ni Dk. Chris Mauki.

Meneja wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu Benedict Busunzu akiwasisitiza waliokuwa wafanyakazi wa Acacia kutumia fursa ya tamasha hilo kutafuta maisha nje ya migodi.

Washiriki wa tamasha la ajira wakimsikiliza Meneja wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu Benedict Busunzu

Meneja wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu Benedict Busunzu akielezea namna Acacia inavyoendelea kutoa elimu ya ajira na ujasiriamali kwa wafanyakazi wake ili kujiandaa kuanza maisha mengine nje ya migodi.Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Huduma na Mahusiano wa Acacia, Elias Kasitila. Wa kwanza kulia ni Meneja Msaidizi wa Ulinzi katika mgodi wa Buzwagi Allan Bunyan akifuatiwa na Meneja Ulinzi katika mgodi wa Buzwagi Gordon Surgeon

Washiriki wa tamasha la ajira wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea

Meneja wa Huduma na Mahusiano wa Acacia, Elias Kasitila akielezea kuhusu tamasha la ajira ambapo alisema zaidi ya makampuni 40 yalialikwa kushiriki tamasha hilo, makampuni 15 yakakubali kushiriki na leo makampuni 11 yamekutana na wafanyakazi wa Acacia zaidi ya 260 walioachishwa kazi katika migodi hiyo.

Kasitila alisema mpaka sasa wafanyakazi 3000 wameachishwa kazi katika migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu hivyo wanafanya jitihada za kuhakikisha wafanyakazi hao wanapata fursa za ajira sehemu zingine ili maisha yaendelee

Mtaalamu wa Mawasiliano Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi Mary Lupamba akitoa maelekezo kwa washiriki wa tamasha hilo la ajira

Tamasha linaendelea

Washiriki wa tamasha hilo wakiwa eneo la tukio

Tamasha linaendelea

Washiriki wa tamasha wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea



Tamasha linaendelea





Tamasha linaendelea





Washiriki wa tamasha hilo wakiwa eneo la tukio





Waliokuwa wafanyakazi katika migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu wakiwa katika ukumbi wa Umoja katika mgodi wa Buzwagi kwa ajili ya kutembelea vibanda vya makampuni yaliyoshiriki katika tamasha la ajira kwa ajili ya kupata mawasiliano na kutoa taarifa zao (CV) kutafuta fursa za ajira





Waliokuwa wafanyakazi katika migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu wakiwa katika banda la shirika la Madini la taifa- STAMICO,wakisikiliza maelezo kutoka Kaimu Meneja rasilimali watu wa shirika hilo,Lameck Kabeho





Waliokuwa wafanyakazi wa Acacia wakiwa katika banda la Shanta Gold Mine kutafuta fursa za ajira





Hapa ni katika banda la kampuni ya Sandvik,kulia ni aliyekuwa mfanyakazi wa Acacia akiuliza jambo





Mfanyakazi wa Mantrac Tanzania Ltd akimsikiliza kwa makini mmoja wa waliokuwa wafanyakazi wa Acacia





Hapa ni katika banda la LINDAM huduma kwa waliokuwa wafanyakazi wa Acacia inaendelea


Ndani ya ukumbi wa Umoja washiriki wa Tamasha la ajira wakibadilishana mawazo



Kulia Mfanyakazi wa CV People,Jolene Ngaluko akimsikiliza kwa makini mmoja wa waliokuwa wafanyakazi wa Acacia aliyeamua kupeleka CV yake kwa ajili ya kutafuta fursa za ajira
Wafanyakazi wa CV Peole Africa wakiendelea kukusanya CV kwa kuziweka kwenye Laptop



Waliokuwa wafanyakazi wa Acacia wakiangalia CV walizokuja nazo kwenye tamasha la ajira kwa ajili ya kuzikabidhi kwenye makampuni



Waliokuwa wafanyakazi wa Acacia wakibadilishana mawazo



Meneja Msaidizi wa Ulinzi katika mgodi wa Buzwagi Allan Bunyan (kulia) na  Meneja Ulinzi katika mgodi wa Buzwagi Gordon Surgeon wakifurahia jambo katika ukumbi wa Umoja wakati wa Tamasha la ajira



Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog 

2 comments:

Tiba asili said...

SAFARI YAKO YA MAFANIKIO UTAJIRI NA RIZIKI ZAKO ZIMESIMAMA NA KUZINASUA UWEZE KUSONGA MBELE SOMA KWA UMAKINI UWEZE KUIJUA SIRI HII.

KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO TUNAPITIA MENGI ILI TUWEZE KUFANIKIWA LAKINI WENGI WETU KUNA MAMBO MACHACHE SANA WENGI WETU TUNAYADHARAU NA KUMBE NDIO CHANZO CHA MAFNIKIO YETU.

N.B KWA WALE WAHITAJI WA PESA ZA NDAGU au MAJINI kwa mudamfupi nipigie DOKTA MDIRO +255 742162843
MALIPO NI BAADA YA KUFANIKIWA PIA UMBALI POPOTE ULIPO KENYA,UGANDA, OMAN, CONGO RWANDA N.K
WOTE NAWAKARIBISHA.

(kuhusu utajiri au pesa) KABLA YA KUPIGA SIMU ZINGATIA YAFUATAYO
1. uwe una umri wa miaka 18+
2. uwe tayari kupokea masharti yote
3.uwe na uwezo wa kutunza siri
4. uwe jasiri wa kupokea taarifa yoyote
KARIBU SANA KWA SHIDA NYINGINE PIA ULIYONAYO AMBAYO SIJATAJA INSHAALAH ITATATULIWA IKIWA NDANI YA UWEZO WANGU.(HUSITUME SMS PIGA SIMU KUHEPUKA MATAPELI)

HAYA NI MAMBO 7 YAKUZINGATIA KATIKA SAFARI YAKO YA MAFNIKIO

i) Wazazi wako wakiwa wamekulea mpaka ukawa mkubwa wafumbua macho unawaona akikisha usiwafanye wakajuta kukuzaa asilimia kubwa wazazi wanakuwa na tabu sana ila zile tabu zao ndio zinazokufanya wewe una aminiwa na watu na unaeshimika na kujieshimu

Kwaiyo jitahidi sana kuwa nao vizuri kuna wengi maisha yao wanaishi kwa shida chanzo ni utofauti baina ya wazazi wao

Ukiona wazazi wako wanatabu sana usiwajibu vibaya wewe kaa nao mbali ila wape majukumu yao unacho fanya kuwaona nakurudi ulipo apo utaona mambo yako yatakuwa vizuri sana

ii) JAMBO LA PILI
Akikisha unatunza uzao wako yani ukijua ni mtoto ni wako basi jitahidi sana kutoa uduma ata kidogo ulicho nacho lakini udumia usiache uzao wako unateseka na njaa wewe una kula maisha aisee fahau

Kila mtoto wako anavyo kuwa ndio mambo yako yanaaribika usipo udumia kwaiyo ukiwa waitaji kufanikiwa zaidi jali uzao wako

iii) JAMBO LA TATU
ukiwa umeoa au umeolewa usitoe talaka au kuomba talaka kabla mwenzio ayupo tayari kwa muda huo fahamu ukiomba talaka au akikupa talaka bila bila sababu ya msingi yeye tu ana matamanio ya kidunia basi anamuda atapoteza muelekeo wa maisha yake

iv) UKIWA WAPATA PESA
ukiwa wapata pesa alafu utoi sadaka basi kufikia kwenye ukuu utachelewa sana mana mana pesa badala ya kutoa kwa iyari yako utatoa kwa matatizo kwaiyo jitahidi icho icho kidogo toa sadaka kwa wenye uitaji

v) USIMZULUMU MTU
kama wataka kufika mbali kwenye mafanikio yako usimzulumu mtu ata kwa uchache wa kitu usifanye ivyo itakugarimu kiasi kikubwa

vi) USIZARAH MILA
ukiwa kwenu kuna mambo ya mila mzimu tambiko jitahidi kufatilia sana aya mambo yanarudisha nyuma sana usipo yawahi mapema

vii)USIWE WA NAMNA
1)ikiwa ujafanikiwa jitahidi sana usiwe mvivu kufanya kazi usiwe muhuni usiwe mwenye chuki na asira zisizo za msingi usiwe na tamaa nyoa vizuri vaa nguo za eshima na usiige maisha ya watu.

KWA MAWSILIANO ZAIDI KUHUSU MATATIZO MBALIMBALI YA TIBA ASILI NA TIBA MBADALA, PETE MALI ZA NDAGU NA MAJINI N.K

DOKTA MDIRO Call/whatsup +255 742162843.

Tiba asili said...

PESA AU UTAJIRI MKUBWA WA MAJINI,, NDAGU NA PETE YA BAHATI,,

======= KUTANA NA MGANGA BINGWA WA TIBA ZA ASILI ,,BINGWA WA TIBA ZA MAPENZI ,,BIASHARA NA KUKUPA UTAJIRI MKUBWA WA MAJINI NA NDAGU,, SI MWENGINE NI DR.Mdiro

MAWASILIANO
WHATSAPP +255742162843
KWA WALIO NJE YA NCHI TUMIENI WHAT'S UP KWA MAWASILIANO

Malipo ni baada ya mafanikio

====Natibu magonjwa sugu kisukali presha kifafa nguvu za kiume uzazi chango ngiri busha ganzi miguu,,tumbo gesi,,maumivu ya mwili,,ndoto mbaya,,na kutafasri maana ya ndoto unazo ota ,, nk

===== Nasafisha nyota,,kutoa mikosi,,nuksi,,kutoa majini mabaya,,kutoa chuma ulete kwenye biashara,, kupandishwa nyota,, kupandishwa cheo,, kupata kazi,, kushinda kesi,,kulipa kisasi kwa ulicho fanyiwa nao wajisikie vibaya Kama wewe ilivyo jisikia,,nk

===== Kumrudisha mpenzi mchumba mume mke uliye tengana nae ,,au kakutelekeza,, kumshika mme wako au mpenzi wa mtu awe anakusaidia na kukutimizia mahitaji Kama NI mpenzi wako,, au Kama anakutaka awe anakupa pesa bila kumuomba ,,

===== Kumrudisha mke mme kwenye himaya yako tena kama mmeachana na unahitaji muwe pamoja au muishi wote Kama zamani,,au Kama humuitaji yeye unataka pesa zake tu pia atakusaidia hata bila kumpa pezi lako,,

=====Kumilikishwa Mali au utajiri mkubwa wa majini,, kupata utajiri mkubwa wa ndagu,,kupata utajiri mkubwa wa freemason,, kukupa utajiri mkubwa kuliko wengine utajiri wa Pete ya bahati ambayo itakuvutia mali pesa na itakupa mvuto mkubwa wa kupendwa na watu,,

===== Kukupa chuma ulete,,kukupandisha nyota ya uganga,, kukupa karama ya kumiliki uchawi,, kukupa nyota ya kushinda bahati nasibu au kamali,, kukupa kinga ya kiwaona wabaya ,, kuona matatizo yako,, kukupa mvuto mkubwa wa kuolewa au kuoa Kama unamchumba au huna kabisa yaani ajitokezee mwenyewe aseme anataka kukuoa au umuowe,,

===== NJOO NIKUHUDUMIE,, PIA NATIBU HATA UKIWA MBALI NAMI UWE MKOANI AU NCHI NYINGINE HUDUMA UTAIPATA KWA HARAKA NA UTAFANIKIWA KWA MDA MFUPI TU,,

====KWA UTAJIRI MKUBWA WA MAJINI
====KWA UTAJIRI MKUBWA