Tangu
kuzinduliwa Dirisha la Ukusanyaji Kodi kidigitali June mosi 2017
(Electronic Revenue Collection System - eRCS) ambalo lilizinduliwa na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akiongozana na Makamu wa Rais Mhe. Mama Samia Suluhu Hassani pamoja na
Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Mohamad Shein, mawaziri kadhaa wa serikali
za Muungano na serikali ya Mapinduzi; Kwa mara ya kwanza serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar imejipatia bila bugudha Ushuru mkubwa wa bidhaa na
kodi ya Ongezeko la Thamani zitokanazo na makampuni ya simu.
Mfumo
huu uliosukwa na vijana wa Kitanzania wazalendo, umefanikisha kuongeza
mapato litokanalo na mtandao (Ciber Space) kwa Zanzibar kwa 51% kwa robo
ya tatu ya mwaka 2017 ukilinganisha na miezi kama hiyo 2016.
Uchunguzi uliofanyika katika robo hiyo (tatu) ya mwaka 2017
(Julai,August na Septemba 2017), umebaini Zanzibar imelipwa kupitia
mfumo wa eRCS Tsh Bil 7.2 ambayo imeongezeka kwa 51% ukilinganisha na
miezi kama hiyo mwaka 2016 ambapo makusanyo ya jumla ya kodi yalikuwa
Tsh Bil 3.5 pekee.
Kwa
mujibu wa vielelezo vya makusanyo wa TRA, miezi mitatu kabla ya mfumo
huu kuzinduliwa rasmi (April,May na June); Makampuni ya simu yalilipa
jumla ya kodi ya Tsh Bil 101.7 lakini baada ya kuzinduliwa rasimi kwa
mfumo huu wa eRCS na makampuni ya simu (TTCL, HALOTEL, AIRTEL, VODACOM,
ZANTEL, SMART na TIGO) kuugwa ndani ya mfumo; Kwa kipindi cha miezi
mitatu pekee ( Julai,Agost na Septemba 2017), yameweza kulipa kwa njia
ya kielektroniki Tsh Bil 128.9 kukiwa na ongezeko la Sh Bil 27.2 sawa na
21% huku ongezeko la kodi ya thamani ikipanda kwa 9% yaani Tsh. Bil 4.7
sambamba na ongezeko la Ushuru wa Bidhaa 29% yaani Tsh. Bil 22.
Taarifa
za kiuchunguzi zimebaini serikali inafuatilia kwa kina udanganyifu
wowote utakao ama uliojitokeza kabla na baada ya mfumo hasa taarifa za
makampuni ya simu katika matumizi yaoya kila mwezi.Mpaka sasa, benk
kadhaa nchini zimekamilisha taratibu za kuungwa katika mfumo huu na
kuanza kulipa kodi kielectroniki. Huu ni ushindi mkubwa kwa mkakati wa
Rais Magufuli katika kupata njia bora za kukusanya mapato nchini.
Ikumbukwe wajenzi wa mfumo huu ni vijana wazalendo walioaminiwa na
serikali ili kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambazo zingetumika katika
ujenzi wa mfumo huo kutumia wataalamu na makampuni ya kigeni.Hivi ndivyo
mapato yanavyoonekana katika Dashibodi ambazo viongozi wakuu wa nchi
wanaona mapato yanavyokusanywa kielectroniki kwa kutumia mfumo wa eRCS
kila sekunde.
Jedwali hili linaonyesha Mabenk yaanza kulipa baada ya yale yaliyokamisha kujiunga na ERCS ambyo ni BANK M na AMANA BANK Tanzania ina Mabenk zaidi ya 20 |
No comments:
Post a Comment