Monday, November 6, 2017

Madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani hawavumiliki kuendelea kumiliki leseni-Muslim

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Fortunatus Muslim amesema kuwa madereva watakaokiuka sheria za usalama barabarani, hatawavumilia kuendelea kumiliki leseni walizozipata.

Muslimu aliyasema hayo wakati alipokutana na vyama vya madereva jijini Dar es Salaam, amesema madereva lazima wafuate sheria za usalama bila kufanya hivyo leseni zao zitafutwa.

Amesema udereva ni kazi zilivyo kazi zingine hivyo lazima kazi hiyo iheshimike kwa kufuata sheria za usalama barabarani barabarani kutokana na asilimia 80 ya uchumi inabebwa na madereva hao.

Kamanda Muslim amesema ameomba majina ya madereva kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Nchi Kavu na Majini (Sumatra) ambao wanachezea vidhibiti mwendo ili aweze kufunga leseni za madereva wanaofanya mchezo huo.

Nae Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usafiri wa Barabara wa Sumatra, SACP Johansen Kahatano amesema kuwa kazi ya madereva kupandisha nauli sio kazi yao kwani wanaotakiwa ni wamiliki kupeleka maombi Sumatra juu ya gharama za uendeshaji,Kahatano amesema suala la madereva kulalamikia mikataba ya ajira haliko kwao na badala yake kazi hiyo itafanywa na idara ya ajira ambao ndio wanaweza kujua juu mikataba ya maderva jinsi itavyokuwa.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Fortunatus Muslim akizungumza katika mkutano wa vyama vya madereva juu kufuata sheria za usalama barabarani, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usafiri wa Barabara wa Sumatra, SACP Johansen Kahatano akizungumza na madereva jinsi Sumatra inavyofanya kazi katika kuhakikisha huduma za usafiri zinatolewa bila mwananchi kupata kikwazo, jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kituo cha Ukaguzi wa Mabasi ya Mikoani, Ibrahim Samwix akionyesha jinsi ya ajali katika picha hazipo pichani katika mkutano wa madereva jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya madereva waliofika katika Mkutano na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani.
.Picha ya Basi iliyoacha barabara na kutokana na spidi.
Basi likiwa na spidi 106 ambapo ni makosa ya usalama barabarani

No comments: