Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu Wenye
Ulemavu,Bi. Jenista Mhagama akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa FERUSCO
Sustainable Development,Bw. Felisi Ngonyani mbele mfano wa hundi yenye
thamani ya Tsh. Bilioni 1.2 wakati wa uzinduzi wa utoaji mikopo katika
mikoa ya kanda ya ziwa, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taiifa la
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Bi. Beng’i Issa wapili kulia, Waziri wa
Nishati,Dkt.Medard Kalemani wa pili kushoto, Mkuu wa Mkoa wa Geita,Bw.
Robert Lughumbi wa tatu kushoto, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita na
Mbunge, Bw. Joseph Musukuma kulia na Meneja Tawi TPB Mwanza, Bw. Shaban
Telatela kushoto.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu Wenye
Ulemavu, Bi. Jenista Mhagama wa tatu kulia akimkabidhi mfano wa hundi
Mkurugenzi wa Mtandao wa ViVOBA Endelevu (Visudent) Kamara Mohamed
kulia, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taiifa la Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa wa pili kulia, Waziri wa Nishati,
Dkt.Medard Kalemani wa pili kushoto, Mkuu wa Mkoa wa Geita,Bw. Robert
Lughumbi wa watu kushoto, Meneja Tawi TPB Mwanza, Bw. Shaban Telatela
kushoto.
Wanachama
wa Vikundi vya VICOBA wakiwa katika uzinduz wa utoaji wa mikopo ya
uwezeshaji ambapo vikundi 272 vilipata mikopo toka Benki Posta (TPB) na
Taasisi ya Hudua za Kifedha na Mikopo- UTT Microfinance Chini ya
Udhamini wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),
Vikundi
vya VICOBA 272 vya mikoa ya Kanda ya Ziwa vimenufaika na uwezeshaji wa
mikopo ya Tsh. bilioni 2. 8 toka Benki ya Posta (TPB) na Taasisi ya
Hudua za Kifedha na Mikopo- UTT Microfinance PLC ili wanachama wake
waweze kuitumia katika shughuli za ujasiriamali na kushiriki katika
uchumi wa taifa lao.
Vikundi
vya VICOBA vilivyo nufaika na mikopo hii vinatoka katika Wilaya au
halmashauri za Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Simiyu na Mara kwa lengo
la kuviwezesha viweze kushiriki katika kuondoa umasikini miongoni mwa
wananchi.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa utoaji mikopo hiyo mkoani Geita, Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu,Bi.
Jenista Mhagama alisema mkopo huo ni sehemu ya Uwezeshaji wananchi
kupitia vikundi vya ViCOBA ili waanzishe au waimarishe miradi yao ya
ujasiriamali.
‘’Huu
ni uwezeshaji Mkubwa na tunataka mkatumie fedha hizi kuendeleza miradi
yenu ya ujasiriamali ili ikazalishe na muweze kuondokana na hali duni ya
vipato,” na hiyo pia itawasaidia kushiriki katika uchumi wa
nchi,aliongeza kusema,Bi Mhagama.
Mikopo hiyo imetolewa na TPB na UTT Microfinance PLC chini ya udhamini wa Baraza la Taifa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).
Akifafanua
zaidi alisema TPB ilitoa Tsh.bilioni 2.7 kwa vikundi 228 na UTT
Microfinance imetoa Tsh.milioni 100, 300,00 kwa vikundi viwili vyenye
wanachama 30.
Pia
alizitaka taasisi zote za kifedha hapa nchi kuanza kwenda katika wilaya
au halmashauri kutoa huduma za kifedha kama mikopo ilia wananchi waweze
kuzitumia katika mirdi yaujasiriamali.
Katibu
Mtendaji wa baraza hilo,Bi. Beng’i Issa alisema mikopo hiyo
imedhaminiwa na baraza kupitia mfuko wa taifa wa uwezeshajii wananchi
kiuchumi imetolewa kwa masharti nafuu na ni mwendelezo wa udhamini
inaoufanywa ili mikopo itolewe kwa wajasiriamali kupitia SACCOS na
VICOBA.
“Vikundi
hivi ni matunda ya taasisi mwanvuli zilizokubali kushirikiana na
serikali kuvianzisha na kufundisha elimu ya VICOBA,” serikali itaendelea
kushirikiana na taasisi hizi katika kazi ya kuzidi kuwawezesha wananchi
aliongeza kusema
Alizitaja
taasisi hizo mwamvuliza za VICOBA ni pamoja na Peoples Long Life
Initiative (PLI), Ferusco Organisation VICOBA Sustainable Development
Agency (FOVSDA), Upepo Wetu na VICOBA Sustainable Development Nertwork
VISUDENT.
Kwa
Mujibu wa Bi. Issa ni kwamba taasisi hizo mwanvuli pia zitahusika
katika kusimamia maresjesho ya mikopo ya vikundi ili kuhakikisha
zinarudi kwa wakati na vikundi vingine viweze kupata.
Alisema
serikali kwa sasa imejielekeza katika kufikia uchumi wa viwanda na
viwanda na uwezeshaji huo unalenga wananchi wananzishe au kukuza
viwanda vidogo vidogo ili mazao ya hapa nchini yaweze kuongezewa tham
ani.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Bw. Robert Lughumbi alisema mikopo niyo ni ya
kujivunia na yenye manufaa makubwa katika kukuza vipato vya wananchi
kuondokana na umasikini katika kanda hiyo.
Serikali
inafanya kazi kubwa ya kuweka mazingira wezeshi na kuibua fursa na
serikali za mikoa ya kanda yetu tutahakikisha mikopo hii inaleta tija,”
Wanachama wa vikundi hivyo wanafanya shughuli mbalimbali za
kijasiriamali, aliongeza Kusema,Bw. Lughumbi.
Baraza
hilo la Taifa linafanya kazi chini ya sheria uwezeshaji namba 16 ya
mwaka 2004 na limedhamiria kuhakikisha uwezeshaji huo unawakomboa
wananchi kiuchumi.
No comments:
Post a Comment