Naibu
Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. George Joseph Kakunda
anayeshughulikia Elimu, Maji, Kilimo, Mifugo na Maliasili, amefungua
Mkutano wa kwanza wa kazi kwa Kaimu Makatibu Wasaidizi wa Tume ya
Utumishi wa Walimu (TSC) katika ukumbi wa chuo cha Mipango mjini Dodoma
leo.
Mkutano
huo ni wa kwanza tangu kuanzishwa kwa Tume ya TSC mwaka 2015, ambao
hutakiwa kufanyika kila baada ya miaka mitatu kwa malengo mbalimbali
likiwemo kupitia kanuni, sheria na taratibu za Tume hiyo.
Akifungua
kikao kazi hicho mjini Dodoma, ameagiza kuwepo kwa ushirikiano baina ya
TSC, Idara ya Elimu na Wadhibiti Ubora wa Elimu (Wakaguzi) ngazi ya
wilaya bila kuwepo kwa muingiliano wa majukumu ili kuinua kiwango cha
elimu nchini badala la kuendelea kubishana na kuingiliana katika
majukumu yao.
“Kuanzia
sasa naagiza Maafisa Elimu wa Wilaya wote nchini, Wadhibiti wa Ubora
kote nchini na Makatibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu katika Halmashauri
zote nchini; kwamba ushirikiano wa kikazi ni jambo la lazima kwenu
vinginevyo tutaendelea kudidimiza Ubora wa Elimu nchini”
Mhe.
Kakunda amewaasa Wajumbe wa Mkutano huo kuendeleza mafanikio ambayo
Tume mpya ya TSC imeyapata kwa kipindi kifupi cha mwaka mmoja kama
kusimamia vema mikataba ya ajira za waalimu wanapoanza kazi, kwani ndio
maisha yao.
“Mnapowasainisha
mikataba ya kudumu ya kazi walimu wapya yenye masharti ya pensheni,
tambueni kwamba, walimu wanaithamini sana mikataba hiyo kwa sababu licha
ya kuhakikishia walimu uhakika wa ajira, mikataba hiyo huwaongoza
walimu jinsi wanavyotakiwa kujiheshimu kazini ikiwa ni pamoja na
kuainisha baadhi ya maadili yao kazi”
Aidha,
amewataka wajumbe kutumia kanuni ya kuwathibitisha walimu kazini ndani
ya mwaka mmoja bila kusubiri malalamiko ya walimu. “walimu wote
wanaotimiza masharti yanayoonesha kuwa wameweza kutekeleza majukumu yao
kwa ustadi na weledi unaotakiwa, wathibitisheni kazini ndani ya muda
usiozidi miezi 12”,
Katika
hatua nyingine, Mhe. Kakunda ameiagiza TSC kuwachukulia hatua wale wote
watakaochelewesha kuwathibitisha walimu bila sababu za msingi, “nataka
kuona hatua hatua zikichukuliwa dhidi ya wote ambao kwa namna moja au
nyingine watachelewesha kuwathibitisha kazini walimu kwa muda mrefu bila
sababu za msingi” Pia
amewaasa wajumbe kusimamia vema suala la kuwapandisha madaraja walimu
kwa mujibu wa kanuni ili kuondoa malalamiko na manung’uniko na kuongeza
ufanisi wa kazi.
Lakini
pia, Mhe. Kakunda ameshauri Kitengo cha Sheria katika Tume ya TSC Makao
Makuu iwe Kurugenzi ya Sheria (Idara kamili) kutokana na umuhimu wa
kazi za Tume kama Mamlaka ya Nidhamu.
Naye
Katibu Tume ya Utumishi wa Walimu Tanzania (TSC), Winfrida Rutaindurwa,
amesema Tume hiyo imepata mafanikio makubwa katika kipindi kifupi tangu
kuanzishwa kwake, kwa sheria namba 25 ya mwaka 2015, ikiwa ni pamoja na
kuandaa Mpango Mkakati wa Tume kwa miaka mitano 2017/18 hadi 2021/22,
kufunga mtambo wa malipo ya mishahara na upatikanaji wa taarifa muhimu
za watumishi kwa wakati.
Amesema
Tume pia imeweza, “kuandaa bajeti ya matumizi ya kawaida na mishahara
wa Tume kwa mwaka 2017/2018, kutengeneza barua pepe za Serikali kwa
ajili ya Watumishi wa Tume Makao makuu, kutengeneza tovuti ya Tume,
kujiunga na Mkongo wa Taifa kutoka TTCL na kuratibu madai ya Watumishi
ya likizo, kusafirisha Wastaafu, gharama za matibabu na posho za
kujikimuambayo yaliwasilishwa kwa Mwajiri wa zamani ambayo ilikuwa
ikiitwa Tume ya Utumishi wa Umma”
Rutaindurwa
amesema pamoja na mafanikio zipo baadhi ya changamoto zinazoikabili
Tume ya TSC ambazo ni ufinyu wa bajeti unaopelekea kutofanya uteuzi wa
Viongozi wa ngazi ya Wilaya ambao ni Makatibu Wasaidizi, uhaba wa Ofisi
za Tume ngazi ya Makao Makuu na Wilaya, upungufu wa vitendea kazi na
samani Makao makuu na Wilayani.
Changamoto
nyingine ni upungufu wa watumishi unaozorotesha utendaji wa Tume hiyo,
“upungufu wa watumishi wa kada mbalimbali wilayani na makao makuu.
Wanaopaswa kuwepo ni watumishi 775”na waliopo ni 417 na upungufu uliopo
ni watumishi 358.
Aidha,
amesema baadhi ya ofisi za TSC katika mikoa na Halmashauri zisizo na
Wakuu wa Wilaya zimeondolewa na kusababisha kupungua kwa ufanisi kwa
ofisi za Tume ngazi ya Makao makuu na wilaya 139, ikiwa ni kutokana na
ukosefu wa usimamizi wa karibu katika ngazi za mikoa.
Rutaindurwa
amesema TSC inarajia kukamilisha zoezi la uteuzi wa Viongozi wa wilaya
kabla ya kuisha kwa mwaka wa fedha 2017/18, kufuatilia mabadiliko ya
muundo wa TSC ili kukidhi mahitaji yake, kutafuta uwezeshaji wa
kuboresha mawasiliano ya kielektroniki makao makuu na wilayani, na pia
kuandaa mazingira ambayo TSC itaongezewa bajeti kwani inahudumia
watumishi zaidi ya asilimia 55 wa Serikali.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Tume ya TSC, Oliva Mhaiki amesema, tangu
kuanzishwa kwa TSC mwaka 2015 na kuanza kazi mwaka 2016, “Tume ilianza
kushughulikia mashauri ya kawaida, lakini kutokana na wingi wa mashauri,
tuliona tuyarudishe wilayani na kama Tume tumeona tujikite na mashauri
ya rufaa”.
Kikao
kazi cha Tume ya Utumishi wa Walimu ni cha siku mbili ambacho ni kikao
cha kwanza tangu kuanzishwa kwa TSC mwaka 2015, kabla ya hapo ilikuwa ni
Tume ya Utumishi wa Umma ambayo ilivunjwa na kuanzishwa kwa Tume ya
Utumishi wa Walimu (TSC).
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Joseph Kakunda
anayeshughulikia Elimu, Maji, Kilimo, Mifugo na Maliasili akielekea
kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma kwa ajili ya kufungua kikao
kazi cha Makaimu Makatibu TSC Wasaidizi mjini Dodoma kushoto kwake ni
Katibu Tume ya Utumishi wa Walimu Tanzania (TSC), Winfrida Rutaindurwa
na kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya TSC, Oliva Mhaiki.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Joseph Kakunda
anayeshughulikia Elimu, Maji, Kilimo, Mifugo na Maliasili akitoa hotuba
wakati wa kufungua kikao kazi cha Makaimu Makatibu TSC Wasaidizi katika
chuo cha Mipango mjini Dodoma, kushoto kwake ni Katibu Tume ya Utumishi
wa Walimu Tanzania (TSC), Winfrida Rutaindurwa, Katibu wa Tume ya TSC
Dodoma Manispaa na kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya TSC, Oliva Mhaiki.
Baadhi
ya Washiriki wa kikao kazi cha Makaimu Makatibu TSC Wasaidizi wa Wilaya
139 nchini, wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Mhe. Kakunda hayupo
pichani katika chuo cha Mipango mjini Dodoma.
Katika
picha ya pamoja waliokaa, katikati ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais
TAMISEMI Mhe. George Joseph Kakunda anayeshughulikia Elimu, Maji,
Kilimo, Mifugo na Maliasili kushoto kwake ni Katibu Tume ya Utumishi wa
Walimu Tanzania (TSC), Winfrida Rutaindurwa na kulia ni Mwenyekiti wa
Tume ya TSC, Oliva Mhaiki.
No comments:
Post a Comment