Friday, November 3, 2017

JAFO: Wafanyakazi Mzigo Hawahitajiki

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akiongea kwenye kikao cha kamati ya kudumu ya bunge ya utawala na Serikali za mitaa na kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mjini Mhandisi Victor Seif akieleza majukumu ya TARURA kwenye kikao cha kamati ya kudumu ya bunge ya utawala na Serikali za mitaa na kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mjini Bw.Abdul Digaga akiongea kwenye kikao cha kamati ya kudumu ya bunge ya utawala na Serikali za mitaa na kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma.

……………

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo amesema hatavumulia kuwa na watumishi mizigo ambao hawatimizi majukumu yao kikamilifu na kuleta mabadiliko katika sekta ya barabara ambayo ni nguzo ya uchumi nchini.

Waziri Jaffo ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa semina ya siku moja kwa wabunge wa Kamati ya kudumu Serikali za mitaa(TAMISEMI) sambamba na Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC) kuhusu majukumu ya Wakala wa barabaraza vijijini na mijini(TARURA) iliyofanyika katika ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma

Mhe. Jaffo amesema Serikali ilishatoa muongozo wa malengo ya utendaji kazi katika utumishi wa umma na kuwapima kulingana na malengo yao hivyo watumishi ambao watashindwa kutekeleza na kufikia malengo waliyopangiwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua za kiutumishi.

Amesema kuwa Serikali haitavumilia suala zima la ubadhilifu kwa watumishi wa umma, kwa kuwa Serikali haiwezi kumbeba mtu ambaye ni mbadhilifu kwa kuwa Serikali inahitaji kuleta mabadiliko katika utendaji kazi na kuleta maendeleo kwa jamii.

Amesema kuwa Taruara ni chombo kipya hivyo haitaji kuajiri watumishi ambao ni mzigo ambao waleta sura mbaya kwa jamii kabla chombo hiki hakijafanya kazi ya kuwahudumia wananchi katika kutatua kero ya miundombinu ya barabara vijijini na mijini.

Amewataka Wabunge wa kamati zote mbili (LAAC&TAMISEMI) kusimamia utekelezaji wa miradi iliyoko chini ya TARURA na kuhakiki ubora wa miradi hiyo na kukosoa pale wanapoona miradi haitekelezwi kwa viwango vinavyotakiwa ili wahusika waweze kurekebisha makosa kabla ya kukabidhi miradi hiyo kwa wahusika.

Aidha aliwahisi Wabunge kuendelea kuishauri TARURA kwa kuwa chombo hiki kimeundwa kwa ajili ya kutoa majibu ya changamoto za Wananchi hivyo ni wajibu wetu kuwasilisha yale yote ambayo tunaona yanawakwaza wananchi katika majimbo yetu.

Mhe Jafo amemuuagiza Mkurugenzi wa TARURA Mhandishi Victor Seif kuhakikisha Mameneja katika ngazi ya Wilaya wanasaini Mkataba wa Makubaliano ya kazi “Performance contract”na kuwafuatilia utendaji wao kwa mujibu wa Mkataba na atakeyeshindwa kufikia malengo yaliyowekwa atolewe bila kigugumizi ili kupisha watendaji wengine watakaofanya kazi kulingana na matakwa ya Serikali.

Wakati huohuo Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa barabara vijijini na mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seif amesema kulingana na muundo na majukumu ya Wakala wa Barabara mahitaji halisi ya watumishi ni 3,222 lakani mpaka sasa ni watumishi 1,147 wameshapatikana ambapo 47 wako Makao Makuu, 103 Mikoa na 997 katika halmashauri, na pia kuna upungufu wa watumishi 2,075 katika kada mbalimbali.

TARURA ina majukumu ya Msingi ya ujenzi, ukarabati na matengenezo ya mtandao wa barabara zenye urefu wa Km 108,946.2 za vijini, mijini pamoja na madaraja, na kati ya hizo barabara 56,000 zinafanyiwa uhakiki ili ziweze kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali ili zitambulike kisheria na Km 52,946.2 tayari zimeshatambulika na kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali.

No comments: