Friday, November 3, 2017

MPINA: “WAFUGAJI TEMBEENI KIFUA MBELE WAZIRI MNAYE”

Waziri Mpina na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Bukoba wakielekea katika zoezi la upigaji chapa ng’ombe katika kata ya katerero kijijini Kyerwa leo.
Katika picha ikionekana sehemu ya ng’ombe aliyepigwa chapa katika kata ya Katerero kijijini Kyerwa leo.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Luhaga Mpina, Mkuu wa Wialaya ya Biharamulo Bi. Saada Malunde baada ya zoezi la kukagua uvamizi wa mifugo katika sehemu ya pori la Bugiri Biharamuro, wengine katika picha ni askari wanyamapori wa pori hilo.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Luhaga Mpina, Mkuu wa Wialaya ya Biharamulo Bi Saada Malunde wakizungumza baada ya zoezi la kukagua uvamizi wa mifugo katika sehemu ya pori la Bugiri Biharamuro.NA MWANDISHI MAALUM – KATERERO

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhanga Mpina amewataka wafugaji nchini kutembea kifua mbele kwa kumpata yeye kama Waziri mwenye dhamana ya Mifugo, Mpina ameyasema hayo leo aliposhiriki katika zoezi la kupiga chapa Mifugo katika Kijiji cha Kyelwa kilichopo katika kata ya Katerero halimashauri ya wilaya Bukoba mkoani Kagera, na kuwataka viongozi kuzingatia maadili wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo ili kuepuka hujuma na ubaguzi kwa wafugaji.

Waziri Mpina alipofika katika kata ya Katerero aliwakuta wafugaji wamejitokeza kwa wingi kuunga mkono zoezi la uwekaji alama katika mifugo yao na kushiriki zoezi hilo kwa kuonyesha msisitizo.

Mara Baada ya kushiriki zoezi hilo, Waziri Mpina aliwataka wafugaji hao kuendelea kujitokeza kwa wingi na kuleta mifugo yao kupigwa chapa na kusema kuwa zoezi hilo ni la manufaa na faida kwa wafugaji kwani litaweza kuwasiadia kuhepuka maambukizi ya magonjwa ya wanyama kwa mifugo yao kuto kuchanganyikana na mifugo mingine sambamba na kusaidia upotevu wa mifugo.

Akiongea katika zoezi hilo diwani wa kata ya Katerero Bw. Nuru Abdul Kabendera alisema kuwa, amefurahishwa na ziara ya Waziri Mpina katika kata ya katerero kwani ni mara ya kwanza kwa kata hiyo kupata ugeni kutoka katika ngazi ya juu ya serikali na kumuomba Mpina kupitia Wizara yake kutatua changamoto inayoikabili kata hiyo la josho la kuoshea ng’ombe ambapo Waziri Mpina amehaidi kuitatua.

Katika hatua nyingine Waziri Mpina ametembelea mapori ya Burigi yaliyopo wilayani Biharamulo ambapo ameupongeza uongozi wa mkoa kwa uporasheni iliyofanyika ya kuondoa mifugo katika mapori tengefu na hifadhi za misitu ambapo amewashuhudia wanyama pori ambao tayari wamerejea katika mapori hayo huku mkuu wa wilaya hiyo Bi SAADA MALUNDE Akiwataka wananchi wa wilaya hiyo kutoa ushirikiano katika zoezi la kuondoa mifugo.

Aidha, Mpina amewataka wakuu wa Mikoa ya mipakani kuwasilisha kwake taarifa ya uondoshwaji wa mifugo katika mikoa yao mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo la oparesheni ondoa mifugo.

Waziri MPINA amemaliza ziara yake ya siku mbili mkoani kagera kubwa akiwa ameagiza mifugo yote iliyokamatwa kutoka nje ya nchi itaifishwe na kupigwa mnada haraka sana kwa mujibu wa sheria.

No comments: