Na David John Misungwi
WANANCHI wa Kijiji cha Mwasonge kilichopo Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza wameiomba Serikali kuharakisha ujenzi wa Daraja linalotenganisha wilaya hiyo na Wilaya ya Nyamagana.
Wamesema kuwa wananchi wa wilaya hizo hususani wanaoishi mpakani wamekuwa wamekuwa wakipata adha kubwa kutokana na serikali kushindwa kujenga Daraja.
Akizungumza Wilayani hapa leo Mwenyekiti wa Kijiji hicho cha Mwasonge Masumbuko Reuben alisema Tangu dunia iumbwe Serikali licha ya kutambua umuhimu wa eneo hilo lakini haijawahi kutengeneza Barabara hiyo wala Daraja.
"Naiomba sana Serikali yangu ifike mahala waone huruma dhidi ya wananchi hawa ambao wengi wao wanakatisha hapa kwenda Buhongwa katika wilaya ya Nyamaga kilometa mbili kuliko kuzunguka Usagala ambako ni zaidi ya kilometa 10."amesema Masumbuko.
Ameongeza kuwa eneo hilo linakuwa hatari zaidi linapojaaa maji kutokana na Mvua ambazo wakati mwingine zinanyesha mfululizo na kusababisha kutumia mitumbwi kuvusha wananchi hali inayohatarisha usalama.
Amefafanua kuwa miaka ya hivi karibuni kutokana na eneo hilo kujaa maji pameshawahi kutokea maafa ya raia hivyo kuna kilasababu na haja ya serikali kujenga Daraja katika eneo hilo.
"kimsingi tumesikia tu kwamba kuna fedha ambazo zimetengwa kwa ajili ya eneo hili lakini hadi leo hatuoni kitu chochote kinachoendela na tuna Muomba Mbunge kufuatilia na kutusemea ili sisi wananchi wake tujengewe Daraja hili. Amesema Masumbuko.
Akitolea ufafanuzi juu ya eneo hilo linalolalamikiwa na wananchi Mbunge wa Jimbo la Misungwi Charles Kitwanga amesema ni kweli fedha za ujenzi wa Daraja hilo zipo kiasi cha shilingi bilioni 1 na milioni mia tisa.
"fedha zipo kwani zilishatolewa na Tanroads na kilichobaki nadhani ni ujenzi tu japo nimesikia tu kuna namna namna zinataka kufanyika mara upembuzi lakini mimi ninachojuwa upembuzi yakinifu ulishafanyika na fedha za ujenzi tayari. "amesema Kitwanga
Aidha amesema yeye kama mbunge amelipigia kelele sana eneo hilo na nikweli kwamba ni linaumuhimu kwa wananchi hao pande zote mbili kwa maana wilaya ya Misungwi na wilaya ya Nyamagana.
Ameongeza kuwa kutoka Mwasonge kwenda Buhongwa ni karibu zaidi kwa kukatiza eneo hilo kuliko kuzungukia Usagala ambako kuna zaidi ya kilometa kumi.
"Naomba Halmashauri ya Wilaya kama fedha hizi zimeshaingia na mimi najuwa hivyo kuna haja ya kuaza ujenzi na nadhani hili ni kwa wilaya zote mbili kwa maana ya Misungwi na Nyamagana. Amesisitiza Kitwangwa.
No comments:
Post a Comment