Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Faustine Ndugulileleo ametembelea Bohari ya Dawa (MSD) ambapo pamoja na mambo mengine amepata taarifa yautendaji ya MSD kuhusu usambazaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara na kusemakuwa bajeti ya dawa inayotolewa na serikali iendane na hali halisi ya upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwenye hospitali na vituo vya afya nchini.
Naibu waziri huyo ambaye ni mara yake ya kwanza kuitembelea MSD tangu ateuliwe kwenyenafasi hiyo, amesema hatua ya serikali kuongeza bajeti ya dawa kuanzia mwaka wa fedha uliopita na mwaka huu ina lengo la kupunguza gharama ya dawa na kuhakikisha upatikanaji wadawa muhimu kwenye vituo vyote vya Afya vya umma ili kumpunguzia mwananchi gharama zamatibabu.
Kwa upande mwingine Mhe. Ndugulile amewataka watendaji wa MSD kuwa na utaratibu wakuwatembelea wateja wao ili kuboresha huduma zaidi baada ya kusikiliza maoni, malalamiko n ahata ushauri wao.
Sambambana hilo amewaagiza MSD kitengo cha huduma kwa watejakutembelea wateja wao na kuhakikisha kitengo cha Manununuzi Maalumu (SpecialProcurement) kinaongeza kasi kwenye manunuzi.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu ameeleza kuwakutokana na hatua ya MSD kuagiza dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji, bei ya dawana vifaa tiba imekuwa nafuu kwa watumiaji na kueleza kuwa mpaka sasa tayari MSD imetoamikataba kwa wazalishaji 104, ambapo 11 kati yao ni kutoka ndani ya nchi.
Mikataba hiyo nikwa ajili ya dawa na vifaa tiba takribani 700.Aidha, ameeleza kuwa kiutaratibu MSD hupeleka dawa moja kwa moja vituoni mara nne kwamwaka, yaani kila baada ya miezi mitatu, mpango wa MSD sasa hivi ni kufikisha dawa hizo kilabaada ya miezi miwili kwa mwaka mzima.
Amesema hatua hiyo ya kupeleka dawa moja kwamoja vituoni itapelekea kuongezeka kwa upatikanaji wa dawa nyakati zote vituoni, hasa maeneoya vijijini. Naibu Waziri huyo ameipongeza MSD kwa koboresha utendaji wake, hasa katika hatua yakupunguza muda wa taratibu za ununuzi kutoka miezi tisa hadi miezi sita kwa ajili yakukamilisha mchakato mzima wa manunuzi, kwa kufuata sheria na taratibu za ununuzi wa Umma.
Katika ziara hiyo, Mhe. Ndugulile amepewa taarifa ya kitengo cha ufuatiliaji wamwenendo wa kazi za kila siku za MSD, kijulikancho kama Strategic management office (SMO)ambacho kiko chini ya ofisi ya Mkurugenzi Mkuu.
Amewapogenza watendaji wote wa MSDkwa mabadiliko wanayofanya hasa kwa wateja wao na watanzania kwa ujumla.Naibu Waziri huyo amewahi kuwa Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Bohari ya Dawa (MSD)tangu mwezi Septemba, 2012 hadi mwezi Julai, 2016.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Faustine Ndugulile, akizungumza na wafanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD), alipofanya ziara ya siku moja kutembelea ofisi hizo jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu (kulia), akitoa maelezo kwa Mhe. Ndugulile.
Picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment