Tuesday, October 17, 2017

serikali ya viwanda Viwanda ni pamoja na ufugaji Kuku na Samaki - Ulega

Na Chalila Kibuda, Globu  ya Jamii
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, amesema serikali ya Viwanda inakwenda na ufugaji Kuku pamoja na samaki kwa kutengeneza  Viwanda vya Kuku pamoja na mabwawa ya ufugaji samaki.

Ulega aliyasema hayo wakati wa ziara yake  aliyoifanya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani kwenye vijiji vinne, ambapo  alisema hakuna sababu ya wananchi wa Mkuranga kuchukua Kuku mikoa mingine  wakati wanaweza kufuga wenyewe na kujipatia kipato na maendeleo yakapatikana na kuwawezesha kuuza hata sehemu nyingine.

Amesema yuko tayari kuwasaidia wananchi wa Mkuranga mbegu za Kuku pamoja na watalaam wa kuwafundisha jinsi ya kufanya ufugaji wa Kuku na samaki wa kisasa. Amesema ajira katika Wilaya hiyo zipo ikiwa ni pamoja na ufugaji Kuku pamoja na samaki ambayo ni ajira ya kudumu na soko ni kubwa kutokana mahitaji ya vitoweo hivyo kuhitajika kwa wingi.

"Sioni sababu wananchi wa Mkuranga kuchukua kuku kutoka mikoa mingine wakati mnaweza kufanya nyinyi wenyewe kutokana na maeneo mlionayo, haitawezekana kama nyinyi hamtaweza  kuonyesha mfano nikiwa ni Mbunge na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi"alisema Ulega.

Katika ziara yake  alitembelea Ujenzi wa Zahanati za Kibamba, Kimazichana na Mwandege na kuahidi kuwaunga mkono wananchi katika juhudi mbalimbali wanazoonyesha katika maendeleo ya huduma za jamii. Ulega amesema kuwa wakati uliopo ni kufanya kazi za Maendeleo kwa kuunga mkono jitihada za Rais Dk. John Pombe Magufuli juu ya dhamira ya serikali ya Viwanda.

 Naibu waziri  aliaahidi kuchagiaji  sh. Milioni moja na mifuko ya saruji kwa ajili ya kikundi cha VICCOBA cha wanawake waliojenga ukumbi wa mikutano na sherehe kilichopo Mwandege.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kibamba juu ya maendeleo mbalimbali ikiwemo ujenzi wa Zahanati.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa Kimazichana.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akiangalia ufugaji wa Kuku katika eneo la Rabica ,Kibamba.
Mmoja wa wazee wa vijiji alivyovitembelea Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ullega akiuliza swali ili aweze kupatiwa ufafanuzi.
Naibu Waziri wa Mifugo na Kilimo, Abdallah Ulega akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mwandege wakati wa kuhitimisha ziara yake iliyokuwa ya siku mbili.
Naibu waziri akipewa zawadi ya Kondoo na wanakijiji cha Kibamba kama sehemu ya zawadi kutokana na utendaji kazi wake.
Picha mbalimbali za Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi , Abdallah Ulega katika Vijiji vya Mkuranga alivyovitembelea.


No comments: