Wednesday, October 18, 2017

MBAO FC WAKABIDHIWA BASI LEO MBELE YA MLEZI WA TIMU HIYO MBUNGE WA ILEMELA ANGELINA MABULA


Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi Angelina Mabula akiwashukuru kampuni ya FT Trucks & Equipments kwa kuipatia udhamini kwa timu ya mkoani kwake Mwanza pamoja na basi sambamba na yeye kuwa mlezi wa timu hiyo leo Jijini Dar es salaam.


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi Angelina Mabula na   Mbunge wa Ilemela, ameishukuru Kampuni ya GF Trucks & Equipments kwa kutimiza ahadi yao kwa Mbao kwa kukabidhi gari yenye thamani ya milioni 70 na tayari wakiwa wamelipia gharama zote za ushuru na kufikia jumla ya milioni 100.

Mabula amesema kuwa baada ya kuingia mkataba na kampuni hiyo wameanzisha kampeni ya ubingwa ili kulitoa taji kwa timu za Mkoa wa Dar es Salaam na wanaweza kufanikiwa kwa hilo kama wadhamini watajitokeza kwa wingi kwa timu za mikoani.

Mbao FC ya Mwanza imekabidhiwa basi lenye thamani ya Sh70 milioni kwa ajili ya wachezaji.Basi hilo wamekabidhiwa leo Jumatano na wadhamini wao Kampuni ya GF Trucks & Equipments katika makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Vingunguti, Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa  Kampuni ya GF Trucks & Equipments Alijawad Karmali alisema basi hilo ni sehemu ya mkataba ambao waliingia na Mbao miezi miwili iliyopita na wameweza kutimiza ahadi hiyo na wanaimani kuwa watalitunza katika kipinci chote..


Mwenyekiti wa Mbao FC, Solly Njashi amewashukuru  Kampuni ya GF Trucks & Equipments kwa udhamini huo mkubwa waliouweka kwani mpaka basi hilo wanalipokea katika mikono yao limezidi thamani ya Sh70 milioni na litakuwa msaada mkubwa sana kwa timu yao kuhusiana na masuala ya usafiri na pia mpaka sasa udhamini wao umeshazidi milioni 140 


Mbao inashika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi sita, huku Simba ikiwa kileleni na pointi 12 ikifuatiwa na Yanga ambayo ndiyo mabingwa watetezi wakiwa na tofauti na mabao ya kufunga na kufungwa.

Ofisa Masoko wa Kampuni ya GF Trucks Equipment, Kulwa Bundala akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kuwakabidhi gari lenye thamani ya milioni 70 kwa timu ya Mbao ikiwa ni moja ya makubaliano yaliyopo katika udhamini wao wa mwaka mmoja kwa timu hiyo.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi Angelina Mabula pamoja na 
Mkurugenzi wa GF Trucks & Equipments Alijawad Karmal (kulia) na mwenyekiti wa timu ya Mbao Solly Zephania Njashi wakikata keki.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi Angelina Mabula akikata utepe katika gari ya waliokabidhiwa Mbao na kampuni ya GF Trucks & Equipments lenye thamani ya milioni 70 ikiwa ni katika makubaliano ya mkataba walioingia miezi mitatu iliyopita, juu ni Mkurugenzi wa GF Trucks & Equipmens Alijawad Karmal akimkabidhi mfano wa funguo ya gari mwenyekiti wa timu ya Mbao Solly Zephania Njashi akishuhudiwa na viongozi wengine wa Mbao Fc pamoja na wengine kutoka GF Trucks & Equipments.
Muonekano wa basi walilokabidhiwa timu ya mpira wa miguu Mbao Fc ya Jijini Mwanza na kampuni ya GFTrucks & Equipments leo mbele ya Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi Angelina Mabula ambaye pia ni Mbunge wa Ilemela na mlezi wa timu hiyo.
Picha ya pamoja ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi Angelina Mabula na viongozi wa timu ya Mbao Fc na wafanyakazi kutoka kampuni ya GF Trucks & leo jijini Dar es salaam wakati wa makabidhiano ya basi lenye thamani ya milioni 70.

No comments: