Wednesday, October 18, 2017

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI, MHE. JAPHET HASUNGA, AWASILI MAKAO MAKUU YA WIZARA MJINI DODOMA LEO

NA HAMZA TEMBA - WMU-DODOMA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Ngailonga Hasunga leo tarehe 18 Oktoba, 2017 ameripoti rasmi Makao Makuu ya Wizara hiyo yaliyopo Mtaa wa Kilimani, Makao Makuu ya Nchi, Mjini Dodoma.

Mhe. Hasunga amepokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi na kuingia ofisini kwake kwa mara ya kwanza ambapo amesaini kitabu cha wageni na baadaye akapata fursa ya kuzungumza na watumishi wa Wizara hiyo waliopo Dodoma.

Akizungumza na watumishi hao baada ya kutambulishwa, Mhe. Hasunga aliwaomba ushirikiano katika kufanikisha majukumu ya Wizara ambayo ni kuhifadhi na kusimamia matumizi endelevu ya maliasili na malikale, na kuendeleza ufugaji nyuki na utalii.

“Nawaombeni ushirikiano tufanye kazi kama timu na tutekeleze majukumu yale ambayo tumepewa, nadhani kwa ushirikiano kwa pamoja tutaweza”. Alisema Mhe. Hasunga.

Naibu Waziri Hasunga ni mingoni mwa mawaziri wapya walioteuliwa na Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli na kuapishwa Oktoba 9, 2017 baada ya kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri. Awali nafasi hiyo ilikuwa imeshikiliwa na Mhe. Mhandisi Ramo Makani.

Aidha, katika uteuzi huo, Dkt. Magufuli alimteua pia Mhe. Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla kuwa Waziri wa Wizara hiyo akichukua nafasi ya Mhe. Prof. Jumanne Maghembe. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kushoto) akikaribishwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi (katikati) alipowasili kwa mara ya kwanza katika ofisi ya makao makuu ya wizara hiyo zilizopo mtaa wa Kilimani mjini Dodoma leo. Kulia anaeshuhudia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Tutubi Mangazeni.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi (kushoto) akimtambulisha Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) kwa watumishi wa Wizara hiyo kabla ya kuzungumza nao leo mjini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kushoto) akizungumza na baadhi ya watumishi wa wizara hiyo baada ya kuwasili kwa mara ya kwanza katika ofisi ya makao makuu ya wizara hiyo zilizopo mtaa wa Kilimani mjini Dodoma leo. 
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kushoto) akizungumza na baadhi ya watumishi wa wizara hiyo baada ya kuwasili kwa mara ya kwanza katika ofisi ya makao makuu ya wizara hiyo zilizopo mtaa wa Kilimani mjini Dodoma leo.   
Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Maliasili wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Japhet Hasunga (hayuko pichani).
 Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Maliasili wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Japhet Hasunga (hayuko pichani).

No comments: