Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe.
Alli Karume akipata maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na
SSRA kutoka kwa Afisa Uhusiano wa Mamlaka Bw. Sabato Kosuri
alipotembelea banda hilo wakati wa maadhimisho ya siku ya Bahari
Duniani yaliyofanyika mkoani Kigoma.
Na. Zawadi Msalla.
Waziri
wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar Mh. Alli Karume ameitaka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa
sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) kusimamia kwa ukaribu michango ya
Wanachama kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ili itumike kwa malengo
yaliyokusudiwa kwa mujibu wa Sheria zilizoanzisha mifuko hiyo.
Wito
huo umetolewa jana mjini Kigoma na Waziri Karume alipotembelea banda la
SSRA kwenye maonesho ya wiki ya Bahari duniani yanayoendelea kwenye
viwanja vya shule ya msingi Mlole Mkoani humo.
Waziri
Karume alisema SSRA inawajibu mkubwa wa kumlinda mwanachama wake ili
kuhakikisha hapati matatizo pale anapotakiwa kupata mafao yake.Pia
alisisitiza kuwa Itakuwa ni jambo la kuumiza sana inapotokea mwanachama
mwenye matumaini ya kupata mafao yake atakapoambiwa mfuko umefilisika na
hivyo mafao anayoyatarajia hawezi kuyapata.
Aidha
Mhe. Karume aliipongeza SSRA kwa elimu wanayoendelea kuitoa kwa jamii
juu ya umuhimu wa kujiunga na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na jinsi
wanavyo simamia maboresho mbalimbali yanayoendelea katika sekta hiyo.
Hata
hivyo alisema bado SSRA inawajibu mkubwa wa kutoa elimu kwa jamii ili
kushawishi wananchi kuona umuhimu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwani
wapo wananchi wengi wasio fahamu umuhimu wa mifuko hiyo na wengi wao
hupata shida inapofikia kipindi cha uzeeni.
Awali
akitoa maelezo ya shughuli za SSRA Afisa Uhusiano na Uhamasishaji wa
Mamlaka hiyo Bw. Sabato Kosuri alimhakikishia Mhe. Waziri usalama wa
michango ya wanachama kwenye mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Bw.Kosuri
alisema tayari SSRA imeweka miundombinu imara ya kusimamia eneo hilo
ikiwa ni pamoja na miongozo ya uwekezaji pamoja na kaguzi za mara kwa
mara ili kuhakikisha mifuko inaendeshwa kwa mujibu wa Sheria kanuni na
taratibu na hivyo kuwahakikishia usalama wachangiaji wote kwenye mifuko
ya hifadhi ya jamii.
Mamlaka
ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii iliundwa kwa
Sheria ya Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii, Sura ya 135
(Toleo la 2015) kwa lengo la kusimamia na kudhibiti Sekta ya Hifadhi ya
Jamii kwa manufaa ya Wanachama na Taifa kwa ujumla. Mamlaka ilianza
kazi rasmi mwishoni mwa Mwaka 2010.
Mamlaka
ina jukumu la msingi la kuhakikisha kwamba Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
inakuwa endelevu, inaendeshwa kwa kufuata kanuni, taratibu na kisheria,
wanachama wanapata taarifa za Mifuko/michango yao, na mafao yaliyobora.
No comments:
Post a Comment