Rais wa Palestina “Mahmoud Abbas” amesisitiza kuwa uhuru wa nchi yake upo karibu hauepukiki na kwamba uvamizi wa Israeli unafikia mwisho, akisema: "Aidha upatikane uhuru au haki kamili ya wote katika nchi ya Palestina ya kihistoria."
Rais Abbas Jumatano jioni akihutubia Mkutano wa 72 wa Umoja wa Mataifa, ameongeza kusema kwamba, imepita miaka ishirini na minne tangu kusainiwa kwa Mikataba ya mpito ya Oslo, ambayo ilionesha ukomo wa uvamizi wa Israeli na kuwapa matumaini Wapalestina, ya kuanzishwa kwa Dola yao huru, huku akihoji " Tuko wapi sasa na matumaini haya?."
Amesema:"Tumekubali uwepo wa Dola ya Israeli kupitia mipaka ya mwaka 1967, lakini Israeli kutokubali uwepo wa Dola ya Palestina kunatupa maswali mengi. Badala ya kuzingatia sababu, inafanya juhudi kuteka misimamo ya kimataifa kwa masuala yasiyo na uzito wowote, yatokanayo na sera zake za kikoloni. Tunapoitaka na kutakiwa na jumuiya ya kimataifa kukomesha uvamizi wake, inadai ni uchochezi na kukosekana ushiriki wa Palestina na kuwekwa kwa masharti yasiyowezekana."
Rais Abbas ameongeza kusema kuwa,anaelea machafuko ni Utawala wa kivamizi wa Israeli katika ardhi yetu,uvamizi ambao umefikia zaidi ya nusu karne,huku zaidi ya miaka kumi sasa tumekubaliana kuunda kamati ya pande tatu ambazo ni Marekani,Israeli na Palestina, ili kumaliza suala la uchochezi.Kamati imefanya kazi kwa muda, lakini tumekuwa tunatoa wito wa kufufuliwa wa kamati hiyo hatupati mrejesho. Hivi ni nani anaekaribisha hilo na kufanya juhudi ya kulifanya liwepo?.
Amesema pia,kuendelea kwa uvamizi ni aibu kwa Israeli na Jumuiya ya Kimataifa,ni wajibu wa Umoja wa Mataifa kumaliza uvamizi huo ili kuwezesha jamii ya Palestina kuishi kwa uhuru na ustawi katika ardhi yake,huku mji mkuu wake ukiwa ni Jerusalemu ya Mashariki.
"Kukomesha uvamizi na vitendo vyake vya kidhalimu, vitakuwa na athari kubwa mno katika kupambana na udaidi pia mashirika yake kukosa karatasi muhimu ambazo huzitumia kwa kuuza fikra zao."Tunatilia mkazo la kukaliza uvamizi ili kukamilisha juhudi zetu katika kukabiliana na mashirika hayo ya kigaidi,kwani Wapalestina wapo dhidi ya ugaidi wa ndani,kikanda na wa kimataifa.
"Kukomesha uvamizi na vitendo vyake vya kidhalimu, vitakuwa na athari kubwa mno katika kupambana na udaidi pia mashirika yake kukosa karatasi muhimu ambazo huzitumia kwa kuuza fikra zao."Tunatilia mkazo la kukaliza uvamizi ili kukamilisha juhudi zetu katika kukabiliana na mashirika hayo ya kigaidi,kwani Wapalestina wapo dhidi ya ugaidi wa ndani,kikanda na wa kimataifa.
"Tuliwasilisha mpango wa amani wa Kiarabu unaoitaka Israeli kuondoka katika maeneo ya Palestina yanayokaliwa kimabavu tangu mwaka 1967 lakini Israeli haikujibu,kama ilivyoufanyia ule mpango ujulikanao kama “Road Map” uliowasilishwa na pande nne na kupitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,hali inayoonekana kana kwamba Israeli ipo juu ya sheria. Vilevile ukaja mpango wa amani wa Ufaransa ukifuatiwa na mkutano husika mjini Paris,lakini juhudi zote hizi zilikataliwa na kupigwa na Israeli."
Ameongeza kusema:”Tulimuomba Waziri Mkuu wa Israeli akubali ufumbuzi wa dola mbili, kisha tukae kuzungumzia suala la mipaka akakataa,licha ya jitihada zetu kufikia amani ya kweli, lakini Israeli inaendelea kuvuruga na kuendeleza ujenzi wa makazi ya walowezi Ukingo wa Magharibi na kila mahali, hatimae hakuna tena nafasi kwa ajili ya taifa la Palestina.
"Vitendo viovu vya Israeli katika mji mtakatifu, vitachochea hisia za uadui wa kidini, ambao unaweza kugeuka mgogoro mkubwa wa kidini, tumeiomba serikali ya Israeli kuheshimu sheria na historia ya sehemu hizo takatifu lakini Israel tangu ilipoikalia kimabavu Jerusalemu mwaka 1976, imekuwa ikiihodhi kwa azimio la upande mmoja.
"Vitendo viovu vya Israeli katika mji mtakatifu, vitachochea hisia za uadui wa kidini, ambao unaweza kugeuka mgogoro mkubwa wa kidini, tumeiomba serikali ya Israeli kuheshimu sheria na historia ya sehemu hizo takatifu lakini Israel tangu ilipoikalia kimabavu Jerusalemu mwaka 1976, imekuwa ikiihodhi kwa azimio la upande mmoja.
Rais Abbas amesema kuwa, “Jerusalemu imekaliwa kimabavu na hatua zote za Israeli ni batili kama ilivyo katika ujenzi wake wa makazi ya walowezi Jerusalemu ya Mashariki na maeneo mengine ya Palestina. Ieleweke wazi kuwa,ubadilishaji wa historia ya Jerusalemu na kuuchafua Msikiti wa Aqswa ni kuchezea hatari,pia ni kushambulia majukumu ya Palestina na yale ya Jordan.Tunaitahadharisha hilo, isijaribu kusababisha vita vya kidini wakati mgogoro wetu ni wa kisiasa”.
"Chaguo letu kama Waarabu na chaguo la dunia ni sheria za kimataifa, uhalali wa kimataifa na uwepo wa dola huru ya Palestina kwa mujibu wa mipaka ya 1967.Tutatoa ushirikiano wote katika kufanikisha hilo la kihistoria,ili tupate kuishi kwa amani pamoja na Israeli. Lakini kama ufumbuzi wa dola mbili utaharibiwa na kuimarisha dola moja yenye serikali mbili,hapatakuwa na linguine kwetu wala kwenu ila mapambano na kutaka kupata haki zetu kamili ndani ya Palestina ya kihistoria. Hivi si vitisho ila ni kutaka haki zetu kama wapalestina”.
Tatizo letu kwa utawala wa kivamizi wa Israeli sio Uyahudi kama dini, kwani hiyo ni dini ya Mungu kama Uislamu na Ukristo.Tumebeba majukumu yetu katika Ukanda wa Gaza,ambayo haiwezekani kuwepo Palestina bila hiyo,ninafarijika leo kuona kufikiwa kwa makubaliano mjini Cairo kufuatia juhudi nzuri za Misri.Yamekomesha vitendo vya Hamas vilivyoleta mgawanyiko na hatimae kufanyika kwa uchaguzi mkuu,hatimae serikali yetu mwisho wa wiki ijayo itakwenda Ukanda wa Gaza ili kufanya kazi huko.
"Ukimya wa jumuiya ya kimataifa juu ya vitendo dhalimu vya Israeli,ndio uliohamasisha vitendo hivyo tangu awali hadi inakiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake, uko wapi Umoja huo na maazimio yake?Vipi unatendea mataifa kwa viwango tofauti? Basi huu ni wajibu wa Umoja wa Mataifa." Aidha ameuomba kumaliza uvamizi wa Israeli ndani ya muda maalumu,kwani haiwezi tena kutoa data huru kuhusu mpango wa amani wa kiarabu,hasa kuhusiana na faili wakimbizi kwa mujibu wa azimio la Umoja wa Mataifa 194,huku akiashiria kuwa maazimio ya Umoja wa Mataifa yanaendelea kupuuzwa na Israeli”.
Rais Abbas amesisitiza haja ya kusitisha shughuli za ujenzi wa makazi ya walowezi katika maeneo ya Palestina,kwani hatuna uwezo wa kulinda raia zetu chini ya utawala wa mabavu,Umoja wa Mataifa uitake Israeli kutambua mipaka Palestina ya mwaka 1967 na kupunguza mpaka na kuomba wajumbe wote wa Umoja wa Mataifa kutangaza kwamba kutambuliwa kwao kwa msingi wa mipaka ya 1967,pia wanachama wote wa Umoja huo kutambua mipaka hiyo ili kutilia mkazo maazimio ya sheria za kimataifa.
Amesema:"Iko wapi mipaka ya Israeli mlioitambua wakati Israeli yenyewe haijaikubali,sheria za kimataifa zinaitaka dunia kuweka hiyo mipaka". Aidha Rais ametoa wito kwa nchi zote duniani kutoshiriki katika ujenzi wa makazi ya kikoloni ulio kinyume na sheria,huku zikichukua hatua stahiki dhidi yake kama ilivyofanya jumuiya ya kimataifa dhidi ya utawala wa kibaguzi wa Afrika ya kusini na tunataka kutangaza habari mbaya za mashirika ambayo yanafanya kinyume cha sheria na makazi."
Hivyo, amezihimiza nchi wanachama kuitambua dola ya Palestina kwa mujibu wa mipaka ya mwaka 1967,huku akitilia mkazo kuwa hatua hiyo haitoathiri mpango wa amani,hasa hasa ikiwa Wapalestina wanaitambua dola ya Israeli. Tunauhimiza Umoja wa Mataifa kuikubali Palestina kama mwanachama wake kamili,huku tukiiomba jumuiya ya kimataifa kuendelea kuisaidia kiuchumi na kifedha ili iweze kujitegemea na kujiamini.
Aidha Rais Abbas, ametahadharisha juhudi za kutaka kubadilisha majukumu ya shirika la misaada UNRWA na kanuni zake,pia kufuta kipengele cha saba katika Baraza la haki za binaadamu au kuzuia kutoa orodha chafu ya mashirika yanayofanya kazi katika makazi ya walowezi wa Israeli nchini Palestina inayokaliwa kimabavu.
Rais Abbas amehitimisha hotuba yake kwa kutilia mkazo msimamo wa nchi yake,katika kuheshimu haki za binaadamu na kutekeleza mikataba ya Umoja wa Mataifa na ile yote iliyosaini,kwani Palestina ni sehemu ya jumuiya ya kimataifa na si vingine. Huku nchi yake pia itaandaa matakwa hayo kwa maazimio yatayokwenda sambamba na misingi husika,kisha kuyawasilisha kwa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
No comments:
Post a Comment