HOSPITALI
ya Teule wilayani Muheza Mkoani Tanga imepata msaada wa mashuka 50 kwa
ajili ya kukabiliana na uhaba uliopo kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa
ya wagonjwa wanao kwenda kupata matibabu kutoka maeneo mbalimbali hasa
vijijini.
Hatua ya uhaba huo unatokana na uchakavu wa wa mashuka unaotokana na kufubaa unaosababishwa na maji wanayotumia kufulia kutokana na uhaba wa maji hali iliyopelekea kuwepo uhitaji kila wakati ili kuweza kukithi mahitaji ya wagonjwa wanaokwenda kupata matibabu.
Hayo yalibainishwa jana na Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza, Boniphace Mhabe wakati akipokea msaada wa mashuka 50 kutoka kampuni ya Suba Agro Trading na Engineering ambao ni mzalishaji wa mbegu bora zamahindi kwa kushirikiana na Cimmity taasisi ya kimataifa ya utafiti wa mahindi na Ngano.
Shuka hilo zilitolewa kwa ajili ya wodi ya wakina mama wajawazito kwenye hosptali ya Teule Muheza,Hospitali ya wilaya ya korogwe na ile ya wilaya ya Handeni lengo kubwa likiwa kuwaondolea changamoto zinazowakabili.
"Vitanda vipo vingi lakini tatizo kubwa ni mashuka na hili linatokana na asilimia kub wa kuchakaa kutokana na maji lakini pia wakati mwengine yanabadilika rangi jambo ambalo limekuwa changamoto kwao.
Aidha alisema wanaishukuru kampuni hiyo kwa kuona umuhimu wa kusaidia msaada huo ambao umefika wakati muafaka kwa kusadia baadhi ya vikwazo wanazokutana navyo wakati wa utoaji wa huduma za afya.
Awali akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo,Afisa Masoko na Mauzo wa Kampuni hiyo,Neema Ng'unda alisema alisema wamekuwawakishiriki katika kuhamasisha kilimo Tanzania hususani kwa wakina mama ambao ndio nguzo kubwa hapa nchini kufikia mafanikio.
Alisema wamelenga wanawake kwa sababu ndio muhimili muhimu kwenye jamii wa kuwawezesha wakina baba kwenye kulima kilimo bora ambapo kinaweza kuwainua kiuchumi.
"Lakini pia tunawashukuru wakulima wote Tanzania kwa kutumia mbegu zao kwa kulima kilimo cha kisasa ambacho kinaweza kuwa mkombozi kijiinuakimaendeleo na kukuza mitaji yao "Alisema.
Naye kwa upande wake,Afisa Mauzo wa Suba Agro Trading yenye makao makuu yake mjini Arusha,Shillaga Samweli alisema zoezi hili limelenga kurudisha fadhila kwa wakina mama wa Tanzania maana ndio wamekuwa wakishiriki kikamilifu katika kilimo.

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha
No comments:
Post a Comment