Na Jacquiline Mrisho na Bushiri
Matenda - MAELEZO.
Matenda - MAELEZO.
Serikali
imewapiga marufuku mawakala wa forodha wanaogushi nyaraka kwa ajili ya
kuingiza kemikali kwani ni kinyume cha Sheria na pia wanaipotezea
Serikali mapato.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA),
Prof. Samwel Manyele alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
uingizaji wa kemikali nchini kutoka nje ya nchi.
Prof.
Manyele amesema kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Udhibiti na Usimamizi wa
Kemikali nchini kila anayeingiza kemikali anatakiwa awe amesajiliwa na
kupewa hati ya usajili huo vile vile anatakiwa kupata idhini ya wakala
wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kabla ya kuagiza mzigo wa kemikali
nchini.
“Natoa
onyo kwa mawakala wote wa forodha wasiofuata taratibu zilizowekwa na
Serikali hasa wanaogushi nyaraka zenye lengo la kukwepesha Sheria na
kukwepa kulipa kodi na tozo mbalimbali za Serikali hivyo watakaokaidi
hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao,” alisema Prof. Manyele.
Prof.
Manyele amesisitiza kuwa kuanzia Leo Agosti 17, 2017 hakuna mtu
atakayeruhusiwa kujishughulisha na shughuli za kemikali bila kuwa na
hati ya usajili wa shughuli anayoifanya pia hakuna atakayeruhusiwa
kuagiza mizigo ya kemikali bila kuwa na kibali.
Aidha,
Prof. Manyele alifafanua lugha elekezi zinazotakiwa kutumika katika
kuweka lebo za kemikali husika kuwa ni Kiswahili na Kingereza tu hivyo
hakuna kemikali itakayoruhusiwa kuingia nchini ikiwa imendikwa kwa lugha
tofauti na hizo.Vile
vile hakuna mdau atakayeruhusiwa kushiriki tenda za ununuzi kwa ajili
ya kuuza kemikali bila kuwa na usajili kutoka kwa Mkemia Mkuu wa
Serikali.
Ofisi
ya Mkemia Mkuu inaendelea kukabiliana na changamoto za wadau wa
kemikali kwa kuendelea kuwaelimisha wadau kuhusiana na matakwa ya Sheria
na Kanuni za uingizaji wa kemikali nchini, kuchukua hatua za kisheria
kwa wale wanaokiuka matakwa ya Sheria na kanuni zake, kuboresha mifumo,
vifaa na sehemu za kufanyia kazi pia wakala inaendelea kufanya kazi kwa
masaa 24 katika siku saba za wiki.
No comments:
Post a Comment