Wednesday, August 16, 2017

Chid Benz awekwa chini ya uangalizi na mahakama kwa kutumia dawa za kulevya.

Na  Mwene Said wa Globu ya Jamii, Dar es Salaam.
Mahakama ya Wilaya ya Ilala imewaweka chini ya uangalizi kwa kipindi cha miaka miwili Msanii wa Bongofleva Rashid Abdalah maarufu Chid Benzi (pichani) na wenzake watano baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha hati ya kiapo dhidi ya maombi hayo.
Aidha, upande wa mashtaka uliwasilisha kiapo hicho kwamba mahakama iwaweke chini ya uangalizi baada ya kubainikia kujihusha na matumizi ya dawa za kulevya.
Maombi hayo yalisikilizwa na kutolewa uamuzi jana mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Ritha Tarimo. Mbali na Chidi Benzi, wengine watakaokuwa chini ya ungalizi ni, Hadia Abeid, Said Ally, Athuman Elias na Hassan Mohamed.
Wakili wa Serikali Glory Mwenda, alidai kuwa upande wa Jamhuri unawasilisha hati ya kiapo kutoka kituo cha polisi Msimbazi kwamba watuhumiwa hao wamekuwa wakijihusisha na matumizi ya dawa za kulevya hivyo mahakama itoe dhamana kwani wamekuwa na tabia mbaya katika jamii.
Glory alidai kuwa wanaiomba mahakama itoe amri ya kuwaweka wajibu maombi chini ya uangalizi wa polisi na mahakama kwa kipindi kisichozidi miaka mitatu na kusaidi dhamana ambayo itahakikisha wanakuwa na tabia njema na kutojihusisha vitendo vya dawa za kulevya.
Baaada ya kuwasilishwa kwa maombi hayo, Chidbenz na wenzake hakuwa na pingamizi.
Akitoa uamuzi hakimu alisema wajibu maombi watakuwa chini ya uangalizi wa polisi miaka miwili na kudhaminiwa na wadhamini wawili watakaotia saini ya dhamana ya Sh.milioni mbili kila mmoja na kuripoti kituo cha polisi Msimbazi kwa mwezi mara moja.
hata hivyo, mjibu maombi Ally alishindwa kutimiza masharti ya dhamana hivyo alirudishwa mahabusu.
Awali, Februari 18, 2015, Chidbenz alikiri katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaa, mashitaka matatu ya kukutwa na Dawa za kulevya aina ya Heroin yenye thamani ya Sh. 38,638, bangi ya Sh. 1,720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo kijiko na kigae.
Msanii huyo alikiri mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Warialwande Lema.Februari 26, 2015 Hakimu Lema alimhukumu kulipa faini ya Sh. 900,000 au kwenda jela miaka miwili na msanii huyo alinusurika kwenda jela baada ya kulipa faini.


Katika kesi ya Kisutu, ilidaiwa kuwa Oktoba 24, mwaka huu katika uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, uliopo Ilala jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alikutwa dawa za kulevya aina ya heroin isivyo halali zenye uzito wa gramu 0.85, gramu 1.72 za bangi isivyo halali, vifaa vinavyotumika kuvuta dawa za kulevya aina ya heroin, kigae na kijiko huku akijua ni kosa.



No comments: