Friday, July 7, 2017

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI LEO

SIMU.TV: Viongozi wastaafu wakiwemo mawaziri nchini Tanzania wametakiwa kuwaunganisha watanzania kuwa kitu kimoja badala ya kuwagawa; https://youtu.be/s8h1VsZuCa0

SIMU.TV: Waziri wa elimu Prof Ndalichako amewaagiza wakaguzi wa elimu kuhakikisha shule zote za sekondari zitakazopokea wanafunzi wa kidato cha tano zinakidhi vigezo; https://youtu.be/M3GwoGHe9R4

SIMU.TV: Mke wa rais mama Janeth Magufuli ameagiza taasisi za serikali na zisizo za kiserikali kushirikiana katika kuwatunza wasiojiweza na wazee nchini; https://youtu.be/3T2bZfgg7T0

SIMU.TV: Serikali ya Tanzania imesema kuwa itaendelea kuthamini mchango wa ushauri wa wazee na machifu mbalimbali katika maendeleo ya nchi; https://youtu.be/WwdGZ37UDLY

SIMU.TV: Serikali ya Tanzania imetangaza kushusha bei za dawa na vifaa tiba baada ya kuingia mikataba na wazalishaji 73 wakiwemo wazalishaji wa ndani; https://youtu.be/1Y-cf6h3bbg

SIMU.TV: Mtandao wa vikundi vya wakulima mkoani Morogoro umeendelea kutoa elimu ya namna ya kuzalisha mbegu bora za vitunguu ; https://youtu.be/KPCjJCMmRzk

SIMU.TV: Waziri wa maji na umwagilaji mhandisi Gerson Lwenge amemuagiza mkandarasi anayejenga mradi wa maji wilayani Bunda mkoani Mara kukamilisha haraka; https://youtu.be/0PTRBhATnas

SIMU.TV: Uongozi wa mkoa wa Mbeya umeelezea kuridhishwa na zoezi la ukarabati wa shule kongwe ya Iyunga unaofadhiliwa na serikali ya Tanzania; https://youtu.be/v_ixPvUJiWQ

SIMU.TV: Mwili wa marehemu Shaban Dede ambae alikuwa muimbaji wa bendi ya muziki ya Msondo Ngoma “Baba ya Muziki” umezikwa leo katika makaburi ya Kisutu; https://youtu.be/b4IdHz9YYvA

SIMU.TV: Mabondi kutoka nchi za Congo, Malawi na Zimbabwe wanatarajia kuwasili nchini wiki hii kwa ajili ya kucheza mapambano kadhaa na mabondia wa watanzania; https://youtu.be/mduFFhS9x6A

SIMU.TV: Uchaguzi wa chama cha soka cha wanawake unatarajia kufanyika hapo kesho jijini Dar Es salaam ili kuweza kuwapata viongozi wapya; https://youtu.be/5f_Se0RYVr8

SIMU.TV: Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars itashuka dimbani usiku huu kumenyana na timu ya Lesotho kuwania nafasi ya mshindi wa tatu; https://youtu.be/ek4Ff7Gf4uA

SIMU.TV: UDP kwa kupitia mwenyekiti wake John Cheyo yawapongeza wabunge kwa kusimama pamoja kuhakikisha miswada ya rasilimali za taifa inapita.. https://youtu.be/09ljHYqehuw

SIMU.TV: Wananchi wamelalamikia kiwango cha juu cha kiingilio kwenye maonesho ya biashara ya sabasaba kwa mwaka huu ukilinganisha na miaka ya nyuma. https://youtu.be/y_ct_6zKYvY

SIMU.TV: Wawekezaji wa sekta ya utalii Zanzibar wameiomba serikali kungalia upya mapendekezo ya kima cha chini cha mishahara ambacho ni shilingi laki tatu ili kunusuru kupunguzwa kwa wafanyakazi kwenye sekta hiyo. https://youtu.be/WCWAgObqAss

SIMU.TV: Kampuni ya Azam inayozalisha maji safi ya Uhai imewataka wafanyabiashara na wajasiriamali kununua maji hayo kutokana na kuwa na ubora wa kuridhisha. https://youtu.be/2__5wGB-MRsv

SIMU.TV: Mkuu wa wilaya ya Hanang Sara Msafiri amepiga marufuku usafirishaji wa mchanga unaosadikiwa kuwa na madini kwenda nje ya wilaya hiyo kwa ajili ya utafiti. https://youtu.be/f-jYDCsN6Ak

SIMU.TV: Uhaba wa wataalamu katika uhifadhi na utunzaji wa mazingira nchini umeelezwa kuchangia kwa kiwango kikubwa vitendo vya uharibufu wa mazingira nchini. https://youtu.be/G_-Wh7Diajw

SIMU.TV: Wakuliama wa zao la vitunguu wameiomba serikali kuwasaidia changamoto zinazowakabili hasa ya wafanyabiashara kununua kwa vipimo vya Lumbesa. https://youtu.be/E-fNIhvkUys

SIMU.TV: Kampuni inayojihusisha na masuala ya kilimo viwanda na wasoko JATU PLC imehimiza elimu ya kilimo kuelekezwa kwa vijana zaidi ili waweze kujiajiri. https://youtu.be/3b2lScTd6dQ

SIMU.TV: Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kilwa kwa kushirikiana na wakala wa misutu TFS imeendesha operesheni ya kuondoa mifugo na wafugaji waliovamia maeneo ya hifadhi. https://youtu.be/XSAzRRhGmLY

SIMU.TV: Wilaya ya Iramba mkoani Singida imeanzisha utaratibu wa kumenzi Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kushiriki michezo mbalimbali kila wanapofanya mikutano ya baraza la madiwani wa halmashauri hiyo. https://youtu.be/hFsqKClaqQM

SIMU.TV: Timu ya vijana ya Yanga chini ya miaka 21 inatarajiwa kucheza na timu ya vijana ya Korea Kusini hapo kesho katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. https://youtu.be/QwyqPk1c0Rg

SIMU.TV: Baadhi ya mabondia kutoka nchi za Congo na Zimbabwe wanatarajiwa kuwavaa mabondia wa Tanzania katika mapambano ya ubingwa mbalimbali. https://youtu.be/vz2EuF_WqYU

No comments: