Na Geofrey Chambua
Hapa duniani kuna mambo mengi sana. Yapo ya kawaida na pia yapo ya kustaajabisha. Yanastaajabisha pale mtu binafsi unavyoona kwamba iko juu ya uwezo wako na wengine na kukufanya mhusika uone kama ni maajabu vile.
Nataka kusema ni kwa uwezo wa Mwenyenzi Mungu, kwa sababu binadamu anaweza kufanya kitu zaidi ya ufikiri wa binadamu mwenzake.
Mmoja wa watu wa aina hiyo anaitwa Ramadhan Yasin Isuja (pichani) ambaye ni mwanafunzi wa Kidato cha Tatu Shule ya Sekondari Moshi (Zamani Old Moshi) mkoani Kilimanjaro.
Huyu kijana hakika ana kipaji cha pekee, kwani yeye ni MTUNZA MUDA wa shule mwenye ulemavu wa macho, lakini ana uwezo wa kukutajia SAA na DAKIKA bila kuangalia SAA.
Na si hivyo tu, hata saa yenyewe wala SIMU hana maungoni mwake
Sidhani kama utaamini kirahisi kama ambayo nami sijaamini maajabu hayo hata sasa lakini ndio ukweli halisi ambao nimeushuhuda bila kusimuliwa na mtu kwa kumuuliza majira zaidi ya mara tatu naye akinijibu bila kukosea hata chembe.
Licha ya kuwa mtunza muda wa Shule, Kijana Ramadhani pia ana uwezo wa kutaja ratiba ya shule nzima, yaani kila darasa na kipindi chake na hili tulilithibitisha wenyewe.
Ramadhani ni mzaliwa wa pili kwenye famlia ya watoto watano, na anasema wazazi wake walikua wakifanya kwa Wahindi na sasa mmojawapo anauza nguo, biashara ambayo ndiyo inayomsomesha kwa sasa.
Katika ziara yangu niliambatana na Mkurugenzi wa Ubunifu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia Dr Mafunda ambaye naye alichukua kumbukumbu kadhaa kwa tafakuri zaidi
Ramadhan Yasin Isuja mlemavu wa macho ambaye ni mtunza muda (timekeeper) wa shule ya Sekondari Moshi (zamani Old Moshi) mkoani Kilimanjaro.
Dr Dugushilu Mafunda (kulia) akiwa na kijana Ramadhan Isuja na wanafunzi wenzie shuleni hapo
Dr Dugushilu Mafunda akiwa anatajiwa noti na thamani yake na Ramadhan Isuja
Dr Dugushilu Mafunda (Aluminae 1978) akipata ushahidi zaidi kwa wenzie na Ramadhan. Kulia ni Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule Hiyo Bwana Koshuma ...Wenye Imani haba huenda itakuwa vtema waende kumuona Shuleni Hapo..
No comments:
Post a Comment