Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
Mkurugenzi
wa kampuni ya VIP Engendering na mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL James
Rugemalira na Habinder Seth Sigh, Mwenyekiti mtendaji wa PAP
wamefikishwa mahakamani kujibu mashtaka sita.
Watuhumiwa
hao wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma
uhujumu uchumi na kula njama, kughushi, kujihusisha na mtandao wa
uhalifu, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya
udanganyifu na kuisababisha hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh
309,461,300,158.27.
Washtakiwa
hao wote wamesomewa mashtaka yao na mwendesha mashtaka, wakili wa
serikali, Paul Kadushi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi. Hata
hivyo, wamerudishwa rumande hadi Julai 3 mwaka huu kwa kuwa mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza wala kutoa dhamana kwa
kesi ya uhujumu uchumi.
Wanadaiwa
kuwa kati ya Oktoba 18 ,2011 na Machi 19 , 2014 jiji Dar es Salaam
walikula njama katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India ya kujipatia
fedha kwa njia ya udanganyifu.
Imedaiwa
kuwa, katika shtaka la kujihusisha na mtandao, washtakiwa hao kati ya
Oktoba 18,2011na Machi 19,2014 jijini Dar es Salaam wakiwa siyo
watumishi wa umma na wakisaidiana na watumishi wa umma walitekeleza
mtandao huo wa uhalifu kwa lengo la kujipatia faida.
Katika
shtaka la nne mtuhumiwa Sethi anadaiwa kuwa Oktoba 10,2011 katika mtaa
wa Ohio Ilala DSm akiwa na nia ya ulaghai alighushi fomu namba 14 a ya
usajili wa makampuni na kuonesha yeye ni Mtanzania anayeishi Kitalu
namba 887 Mtaa wa Mrikau Masaki wakati akijua si kweli.
Seth
anadaiwa kutoa nyaraka hiyo ya usajili wa kampuni kwa ofisa msajiri wa
kampuni,Seka Kasera kwa njia ya kuonesha kwamba yeye ni Mtanzania na
Mkazi wa Mtaa wa Mrikau.
Aidha
katika shtaka jingine, Washtakiwa wote, wanadaiwa kuwa kati ya Novemba
28/29, 2011 na Januari23,2014 makao makuu ya benki ya Stanbic kinondoni
na Benki ya Mkombozi tawi St Joseph kwa ulaghai, walijipatia kutoka
Benji Kuu ya Tanzania (BOT), USD 22,198,544.60 na shilingi 309,
461,300,158.27.
Iliendelea
kudaiwa kuwa katika shtaka la kusababisha hasara, washtakiwa hao
wanadaiwa, Novemba 29, 2013 katika Benki ya Stanbic tawi la kati
Kinondoni kwa vitendo vyao waliisababishia Serikali hasara ya USD 22,
198, 544.60 na Tsh 309,461,300,158.27.
Baada
ya kumaliza kusomewa mashtaka yao, wakili wa utetezi Respicius Didas
kwa niaba ya mawakili wenzao aliomba mahakama iwapatie wateja wao
dhamana kwa sababu Mashtaka yanayowakabili yanadhaminika.
Hqta
hivyo, upande wa mashtaka ulipinga vikali hoka hizo na kuiomba mahakama
kuyatupilia mbali maombi ya utetezi ya kuwapatia dhamana washtakiwa
hao.
Akiwasilisha
hoja zake, Kadushi amesema mahakama ya Kisutu haina mamlaka si tu ya
kutoa dhamana bali hata kusikiliza maombi ya dhamana.
Amesema
mahakama pekee yenye mamlaka ya kufanya hivyo ni Mahakama Kuu na ndiyo
maana washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote wakati wakisomewa mashtaka
yao.
Ameongeza
mazingira pekee ambayo yangeifanya mahakama ya kisutu iweze kusikiliza
maombi hayo na keai kwa ujumla ni pale ambapo Mkurugenzi wa Mashtaka
(DPP) angetoa cheti maalum cha kuipa mamlaka mahakama ya Kisutu
kuisikiliza kesi hiyo.
" Maombi ya dhamana yameletwa katika mahakama isiyoweza kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria" amesema Kadushi.
Naye
Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi alisisitza na kuomba mahakama
kutupilia mbali hoja zote za maombi ya dhamana zilizotolewa na upande wa
uetezi na ijielekeze kwa Jinsi inavyoona inafaa washtakiwa waende
mahabusu wakati wakisubiri taratibu za kesi zinazoendelea.
Akijibu
hoja hizo, Hakimu Shaidi amesema sheria inaelekeza kwamba kesi za
uhujumu uchumi zinazozidi milioni 10 Mahakama hii haina mamlaka ya
kuisikiliza wala kutoa dhamana isipkuwa kwa Cheti maalum kutoka kwa DPP
kinachoiwezesha mahakama kufanya hivyo.
Kesi hiyo itatajwa Julai 3,2017, watuhumiwa wameenda gereza la Segerea.
Mmiliki wa VIP Engineering and Marketing, James Rugemarila na Mmiliki wa Kampuni ya IPTL, Habinder Seth Sigh wakiwa Ndani ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam tayari kwa kusomea Mashitaka yao ikiwemo la Uhujumu Uchumi.Picha Humphrey Shao wa Globu ya Jamii.
Mmiliki wa VIP Engineering and Marketing, James Rugemarila na Mmiliki wa Kampuni ya IPTL, Habinder Seth Sigh wakipandishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu jijini Dar es Salaam
Mmiliki wa VIP Engineering and Marketing, James Rugemarila na Mmiliki wa Kampuni ya IPTL, Habinder Seth Sigh wakipandishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu jijini Dar es Salaam wakitoka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mara baada ya kukosa dhamana na kutakiwa kupelekwa mahabusu.
Mmiliki wa VIP Engineering and Marketing, James Rugemarila na Mmiliki wa Kampuni ya IPTL, Habinder Seth Sigh wakipakiwa kwenye gari kwa ajili ya kupelekwa Rumande mara baada ya kukosa Dhamana kutokana na Makosa yanayo wakabili
Mmiliki wa VIP Engineering and Marketing, James Rugemarila na Mmiliki wa Kampuni ya IPTL, Habinder Seth Sigh wakipakiwa kwenye gari kwa ajili ya kupelekwa Rumande mara baada ya kukosa Dhamana kutokana na Makosa yanayo wakabili
Mmiliki wa VIP Engineering and Marketing, James Rugemarila na Mmiliki wa Kampuni ya IPTL, Habinder Seth Sigh wakipakiwa kwenye gari kwa ajili ya kupelekwa Rumande mara baada ya kukosa Dhamana kutokana na Makosa yanayo wakabili
No comments:
Post a Comment