Na Mwandishi Wetu
Mwanasiasa mkongwe nchini Augustine Lyatonga Mrema amesema Rais John Pombe
Magufuli ameweka historia ya mapambano ya uchumi nchini kutokana na namna
ambavyo analishughulikia suala la madini.
Bwana Mrema amesema kuwa kitendo cha Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold
Cooperation Profesa John Thornton kusafiri usiku kucha kuja kuonana na Rais Magufuli
na kukubali kuilipa Tanzania fedha zote ilizokoseshwa na Kampuni Acacia ni kielelezo
kuwa sio tu kuwa ujumbe wake umefika lakini zaidi inadhihirisha kuwa madai yake dhidi
ya kampuni hiyo ya uchimbaji madini ni ya msingi.
“Ni kiongozi gani barani Afrika aliyethubutu kuishutumu kampuni ya nje kama
alivyofanya Rais Magufuli halafu viongozi wake wakasafiri kuonana na kiongozi huyo
kutaka suluhu kama alivyofanya Mwenyekiti huyo wa Barrick kwa Tanzania?”alihoji
Bwana Mrema.
Mwanasiasa huyo aliungana na wito wa Rais Magufuli wa kuwataka baadhi ya watu
wanaowahusisha viongozi wastaafu na taarifa za Tume za Rais za kuchunguza
Makinikia.
“Si vizuri na kwamba si sheria kwa mtu yeyote kuwatukana au kuwashambulia marais
wastaafu kama ilivyo kwa Rais aliye maradakani na sheria inatoa dhabu kali kwa
wanaofanya hivyo” alieleza bwana Mrema.
Alibainisha kuwa kuwahusisha na taarifa hizo wakati hazijawataja kunaweza
kusababisha kuigawa nchi na kuhatarisha mshikamano wa Taifa katika kipindi hiki
ambacho watanzania wanapaswa kuwa kitu kimoja kumuunga mkono Rais wao na
Serikali kwa hatua mbalimbali anazozichukua kuimarish uchumi.
“Tumekubali kikatiba Marais wetu waliopo madarakani na wastaafu walindwe kwa kuwa
ndio ni msingi wa utulivu, amani na mshikamano wetu hivyo hatuna budi kuwaheshimu
kwa kutekeleza hilo tulilokubaliana” alieleza Mrema.
Mwansiasa huyo alieleza kushangazwa kwake na baadhi ya watu wakiwemo baadhi ya
wabunge kumdhihaki Rais na kutozipa uzito jitihada zake za kutetea maslahi ya nchi na
kuhoji mbona wananchi wa nchi nyingine kama Uingereza na Japan hawawabezi
watawala wao akimaanisha Malkia na Mfalme.
“Baadhi ya wabunge wanaacha ajenda ya msingi ya kupambana na unyonyaji
unaofanywa na makapuni ya madini badala yake wanaanzisha kampeni dhidi ya
Rais”alieleza Bwana Mrema na kusema kuwa vitendo hivyo ni vya kichochezi, usaliti na
ni vya kizandiki kwa Taifa.
Bwana Mrema alifafanua kuwa kitendo cha baadhi ya wabunge kusema eti “Rais kama
angekuwa makini” asingechukua hatua alizochukua za kuzuia mchanga na kuunda
Tume ni kitendo cha kumdhallisha Rais ambaye alichaguliwa baada ya kuwashinda
wagombea wengine alioshindana nao katika mbio za uchaguzi wa nafasi hiyo.
“Huyo Rais ‘makini’ ni yupi zaidi ya yule aliyewashinda wengine wote. Rais amekuja na
mpango anautekeleza, tumuunge mkono…sisi ndio tuliomchagua” Alisisitiza bwana
Mrema
Anabainisha kuwa haiwezekani mtu mkubwa na mashuhuri kama Profesa John
Thornton atoke Canada kuja kuonana na Rais wetu tena akiwa na Balozi wa nchi yake
iwe ni jambo la kupuuzwa.
Bwana Mrema alisema wako waliotaka Rais ataifishe mali za makampuni
zinazotuhutumiwa kuiibia Tanzania lakini Rais Magufuli ametambua kuwa huu si wakati
tena wa kutaifisha mali bali ni wa kutumia sheria zilizopo kupata haki na ndivyo
anachofanya.
Mrema ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha TLP alilikumbusha Jeshi la Polisi
wajibu wake wa kumlinda Rais dhidi ya kejeli za baadhi ya watu wakiwemo wabunge na
kulitaka jeshi hilo kutofanya ajizi kuwakamata watu wanaofanya vitendo hivyo dhidi ya
Rais na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.
“Sheria ziko wazi kuhusu jambo hilo. Hata mimi mwenyewe niliwahi kushitakiwa
mahakamani kwa kesi kama hiyo lakini nikashinda kwa kuwa waendesha mashitaka
walishindwa kuthibitisha pasipo shaka kuwa nilifanya kosa hilo” alifafanua Mrema na
kujinasibu kuwa akiwa mtu safi aliyelelewa vyema na Taifa lake kamwe hathubutu
kumtusi au kumdhihaki kiongozi wa nchi yake.
Tangu Rais Magufuli aunde Tume za Kuchukunguza Mchanga wa madini
kumwekuwepo na baadhi ya watu wanaopinga hatua hiyo kwa madai kuwa inaweza
kuitia Tanzania katika mgogoro wa kisheria na kampuni ya Acacia.
Hata hivyo, baada ya ripoti ya Kamati ya Pili ya Uchunguzi kuwasilisha taarifa yake kwa
Rais Magufuli hivi karibuni ambayo ilizidi kuonesha namna Kampuni hiyo ilivyoikosesha
Serikali trilioni za shilingi, Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Cooperation Profesa
John Thornton alikuja nchini kwa mashauriano na Rais.
Katika mazungumzo hayo muafaka ulifikiwa kuwa iundwe Tume ya mashauriano kati ya
kampuni hiyo na Serikali huku kiongozi huyo wa Barrick akiahidi kurejeha fedha zote
ambazo itabainika kuwa kampuni ya Acacia ilipaswa kuilipa Tanzania.
No comments:
Post a Comment