Friday, June 16, 2017

WAANDISHI WA HABARI ZANZIBAR WAELIMISHWA KUHUSU KIPINDUPINDU

 Mkuu wa Wilaya ya Mjini Marina Joel Thomas akifungua mafunzo ya waandishi wa habari  juu ya maradhi ya kipindupindu yaliyoandaliwa na Idara ya Kinga katika Ukumbi wa  RCH Kidongochekundu Mjini Zanzibar.
 Afisa  Afya Juma Mohd Juma akitoa maelezo ya historia ya kipindupindu duniani na hatimae kuingia Zanzibar katika miaka ya 1976 na kurejea kila baada ya kipindi.
 Mwandishi wa habari wa Redio Coconut Tabia Makame akitoa mchango katika mafunzo ya waandishi wa habari ulioandaliwa na Idara ya Kinga na Elimu ya Afya kuhusu maradhi ya kipindupindu.
 Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Afya Halima Ali Khamis akieleza malengo ya Wizara ya Afya katika kukabiliana na maradhi ya kipindupindu ili kuhakikisha yanaondoka Zanzibar. 
 Daktari dhamana Wilaya ya Mjini Ramadhani Mikidadi Suleiman akieleza dalili za maradhi  ya kipindupindu Zanzibar na dalili zake katika hatua za awali katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika ukumbi wa RCH.
 Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Hassan Vuai akifunga mafunzo  ya waandishi wa habari kuhusu maradhi ya kipindupindu katika ukumbi wa RCH Kidongochekundu.

No comments: