Na Mwandishi Wetu.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi
Hassan Simba Yahya, amewaomba washiriki wa Mkutano wa Kamati
Ndogo ya Usalama wa Raia ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika (SADC), kuhakikisha wanapambana kupunguza vitendo vya
ujangili, biashara ya magendo, biashara ya binadamu, uhamiaji haramu
kwani vitendo hivyo vinarudisha nyuma maendeleo ya nchi zilizopo
katika jumuiya hiyo, hivyo kupelekea kurudi nyuma kwa shughuli za
maendeleo na uchumi.
Balozi Simba aliyasema hayo alipozungumza katika Mkutano huo
uliojadili masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama katika maeneo ya
nchi wanachama wa jumuiya hiyo, uliohusu masuala ya uhamiaji,
ukimbizi, mbuga na wanyamapori katika maeneo ya nchi wanachama
wa jumuiya ya SADC, leo jijini Dar es Salaam.
“Hatuwezi kuendelea kiuchumi katika nchi zetu za wanachama wa
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, kama matendo ya
ujangili,biashara ya binadamu, masuala ya wakimbizi, uhamiaji haramu
hayajatafutiwa ufumbuzi, kwani haya yatazorotesha shughuli za
kiuchumi ikiwepo utalii, hivyo ni bora tukayafanyia kazi maeneo hayo,”
alisema Balozi Simba.
Akizungumza wakati wa uchangiaji mada katika mkutano huo,
Mkurugenzi wa Masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya
Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Jorge Cardoso, alisema uhalifu
katika mipaka ya nchi wanachama ikiwemo uwindaji haramu wa pembe
za ndovu, uhamiaji haramu,biashara ya binadamu na madawa ya kulevya
lazima vidhibitiwe kwani vikiachwa mbeleni vitahatarisha Amani na
utulivu uliopo katika nchi wanachama.
“Amani na utulivu katika nchi wanachama ni kichocheo cha mabadiliko
ili kupiga hatua za kimaendeleo kwenda mbele na kushirikiana kukuza
uchumi katika nchi wanachama wa SADC, hivyo yatupasa wote kwa
pamoja kuunga mkono harakati za kukomesha vitendo vya uhalifu
katika nchi na mipaka yetu,” alisema Cardoso.
Aidha washiriki wa mkutano huo kutoka katika nchi za Tanzania,
Afrika Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Swaziland, Malawi,
Zimbabwe kwa pamoja walikubaliana kupitia Kamati za Ulinzi na
Usalama katika nchi zao kudhibiti matendo yote yanayohatarisha amani
na utulivu.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi
Hassan Simba Yahya, akizungumza wakati wakati wa ufunguzi wa
Mkutano wa Kamati Ndogo ya Usalama wa Raia ya Jumuiya ya
Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), uliofanyika katika Ukumbi wa
Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, leo jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi wa Masuala ya Siasa,Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya
Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Jorge Cardoso, akizungumza
wakati wa Mkutano wa Kamati Ndogo ya Usalama wa Raia ya Jumuiya
hiyo,uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa
Mwalimu Julius Nyerere,leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi
Hassan Simba Yahya, akiongoza Mkutano wa Kamati Ndogo ya
Usalama wa Raia ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika,Kulia ni
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini, Dk. Anna Makakala.Mkutano
huo umefanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa
Mwalimu Julius Nyerere,leo jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias
Andengenye ,akichangia hoja wakati wa Mkutano wa Kamati Ndogo ya
Usalama wa Raia ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika(SADC),uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano
wa Mwalimu Julius Nyerere,leo jijini Dar es Salaam.
Balozi Mdogo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo nchini, Profesa
Jean Kitembo Mbilika ,akichangia hoja wakati wa Mkutano wa Kamati
Ndogo ya Usalama wa Raia ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika(SADC),uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano
wa Mwalimu Julius Nyerere,leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu kutoka Malawi,Michael Gama ,akichangia hoja
wakati wa Mkutano wa Kamati Ndogo ya Usalama wa Raia ya Jumuiya
ya Maendeleo Kusini mwa Afrika(SADC),uliofanyika katika Ukumbi
wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere,leo jijini Dar
es Salaam.
Naibu Mkuu wa Uhamiaji kutoka nchini Swaziland,Makhosi Simelane
,akichangia hoja wakati wa Mkutano wa Kamati Ndogo ya Usalama wa
Raia ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika(SADC),uliofanyika
katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius
Nyerere,leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Balozi wa Zimbabwe nchini, Walter Sande akichangia hoja
wakati wa Mkutano wa Kamati Ndogo ya Usalama wa Raia ya Jumuiya
ya Maendeleo Kusini mwa Afrika(SADC),uliofanyika katika Ukumbi
wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere,leo jijini Dar
es Salaam.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi
Hassan Simba Yahya (wapili kulia), akiwa katika picha ya pamoja na
washiriki wa Mkutano wa Kamati Ndogo ya Usalama wa Raia ya
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Watatu kulia ni
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini, Dk. Anna Makakala.Mkutano
huo umefanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa
Mwalimu Julius Nyerere,leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi).
No comments:
Post a Comment