Tuesday, May 9, 2017

MUFINDI YA ENDELEA KUTEKELEZA SERA YA KUWA NA ZAHANATI KWENYE KILA KIJIJI.


Na Afisa Habari Mufindi
Halmashauri ya Wilaya ya Maufindi imeendelea kutekeleza sera ya serikali ya kuhakikisha kila Kijiji kinakuwa na Zahanati kwa kuzindua na kuweka mawe ya msingi kwenye  zahanati za Vijiji vinne kati ya vitano zilizopo kata ya Ihalimba Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi.
 Uzinduzi na uwekaji wa mawe ya msingi umetekelezwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mh. Festo Mgina, Diwani wa kata Ihalimba Mh. Award Mahanga sanjari na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmahauri Prof. Riziki Shemdoe.
Taarifa hiyo imevitaja vijiji vilivyo nufaika na huduma hiyo muhimu kwa usatawi wa afya ya jamii kuwa, ni pamoja na Kijiji cha Wamimbalwe uwekaji wa Jiwe la msingi, uzinduzi wa Zahanti ya Kijiji cha Vikula, uzinduzi wa zahanati ya Kijiji cha Nundwe pamoja na uwekaji wa jiwe la Msingi kwenye azahanati tarajiwa ya Kijiji cha Ihalimba.  
Awali akiwahutubia wakazi wa Vijiji hivyo, Mwenyekiti wa Halmashauri Mh Festo Mgina, alitoa rai kwa wananchi kujiepusha na tabia hatarishi zinazochochea maambukizi ya Virusi vya ukimwi huku akiutaja Mkoa wa Iringa kuwa na asilimia kubwa ya maabukizi ya  09.1 wakati asilimia ya kitaifa ni 05.6 Pekee. 
Aidha, Kiongozi huyo mwenye dhamana ya juu ya uongozi katika halmashauri hiyo, amekemea vitendo vya ubakaji kwa Watoto ambavyo vinashamili kwa kasi Wilayani Mufindi.
Mnamo mwaka 2015 wakati wa ufunguzi wa Bunge la Tanzania, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanazania Mh. Dk. John Pombe Magufuli, aliahidi kuwa serikali ya awamu ya Tano itahakikisha sera ya kuwa na zahanati kwenye kila kijiji na kituo cha afya kwa kila kata inatekelezwa kwa vitendo.

No comments: