Tuesday, April 4, 2017

SIMUTV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Ulinzi mkali uliimarishwa katika mahakama ya hakimu mkazi wa wilaya ya Biharamulo wakati wafugaji 19 walipo fikishwa katika mahakama hiyo wakikabiliwa na makosa ya kulisha mifugo katika mapori ya hifadhi. https://youtu.be/nVGu2kyoygc

SIMU.TV: Umoja wa Ulaya umekubali kuipatia Tanzania msaada wa zaidi ya shilingi bilioni 490 kwa ajili ya kusaidia mifumo ya kisera na utekelezaji wa miradi ya bajeti kwa kipindi cha miaka minne ijayo. https://youtu.be/NXhHP3e9e7g

SIMU.TV: Wafanyabiashara ndogo ndogo jijini Dar es Salaam leo wamekumbwa na taharuki baada ya kufika eneo la jengo lao la Machinga Complex na kukuta vibanda vyao vya nje ya jengo vimevunjwa. https://youtu.be/7hKPACauF84

SIMU.TV: Chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Mbeya kimeanza kutoa taratibu za uchaguzi na mrejesho wa maeneo ambayo yamefanyiwa marekebisho katika katiba ya chama hicho. https://youtu.be/KWuo7TKhIcQ

SIMU.TV: Baadhi ya wananchi mkoa wa Mara wameiomba serikali kuwapatia mbegu bora za mihogo na mtama ili waweze kutumia mvua zinazoendelea kunyesha kupanda mbegu hizo. https://youtu.be/y1IJlEM8qkA

SIMU.TV: Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Farida Salehe amejitokeza mbele ya vyombo vya habari na kudai amezulumiwa nyumba yake aliyoachiwa na marehemu  mume wake Alfred Choma. https://youtu.be/3k2K1EoTq48

SIMU.TV: Wapangaji sita katika nyumba iliopo mtaa wa Kisukari Mwananyamala jijini Dar es Salaam pamoja na mmiliki wa nyumba hiyo wamekumbwa na taharuki baada ya kuvamiwa asubuhi na kubomolewa nyumba hiyo na mtu anayedai kuinunua. https://youtu.be/PDJ8leFikcI

 SIMU.TV: Licha ya kuongezeka kwa idadi ya mabenki hapa nchini imeelezwa kuwa bado mabenki hayo yameshindwa kutoa huduma zinazowafikia wananchi masikini nchini. https://youtu.be/3oMYgwDc9E4

SIMU.TV: Sekta za viwanda na kilimo nchini zimetajwa kuchukua nafasi ya juu katika uchukuaji wa mikopo tangu kuanzishiwa kwa sera ya uchumi wa viwanda nchini. https://youtu.be/AIsnIeByWBE

SIMU.TV: Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 Serengeti boys imeambulia sare ya mabao mawili kwa mawili katika mchezo wao wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya vijana kutoka Ghana. https://youtu.be/mkU_xDoq5bc

SIMU.TV: Klabu ya Azam Fc leo imezuru makao makuu ya benki ya NMB ambayo ndio wadhamini wakuu wa klabu hiyo ambapo benki hiyo imeahidi kuendelea kuidhamini timu hiyo. https://youtu.be/LlFXN5MdxYg

SIMU.TV: Timu ya soka ya Maji maji kutoka Songe imeonekana kuongeza nguvu za kupambana ili kubaki ligi kuu Tanzania bara baada ya kuifunga Toto Afrika mabao manne kwa moja. https://youtu.be/-_Bak0Ik1Nc  

SIMU.TV: Wizara ya habari utamaduni sanaa na michezo imewataka wadau wa michezo nchini kuachana na tabia ya kuamini ushirikina katika michezo ili kuleta maendeleo katika sekta hiyo. https://youtu.be/V4Tq4hjKYZA

No comments: