Wednesday, April 19, 2017

NEEC FANYENI TATHMINI YA KISAYANSI KUHUSU MANUFAA YA MIFUKO YOTE YA UWEZESHAJI-MAJALIWA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkurugenzi wa manispaa ya Dodoma, Bw. Godwin Kunambi (wapili kushoto) hundi ya Shilingi 1, 469, 358,0 00/= kwa ajili ya vijana kabla ya kufungua maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kwenye uwanja wa mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017. Wanne kushoto ni Wziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na kulia ni Naibu Wziri wake, Anthony Mavunde. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini , Christina Mndeme na watatu kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la  Taifa wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng Issa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Mawasiliano wa Benki ya TPB, Noves Moses (kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Sabasaba Moshingi ( wapili kulia) cheti maalum cha kushiriki Maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kabla ya kufungu maonyesho hayo kwenye uwanja wa Mashujaa mjni Dodoma Aprili 18, 2017. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama. (picha na Ofiai ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mzee Maarufu wa Dodoma, Job Lusinde baada ya kufungua maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya serikali kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017. Wengine pichani kutoka kulia ni Waziri wan chi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, AjiraKazi, Jijana, ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Christina Mndeme na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng Issa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TBP, Bw. Sabasaba Moshingi akizungumza kwa niaba ya viongozi wa Mifuko ya Uwezeshaji ya Serikali katika maonyesho ya mifuko hiyo yaliyozinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akiwasalimia wananchi wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipofungua Maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kwenye uwanja wa Uhuru mjini Dodoma Aprili 18, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi walioshiriki katika maonyesho ya Mifuko ya Uwezesha Wananchi ya serikali baada ya kufungua maonyesho hayo kwenye Uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi walioshiriki katika maonyesho ya Mifuko ya Uwezesha Wananchi ya serikali baada ya kufungua maonyesho hayo kwenye Uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Mawasiliano wa Benki ya TPB, Noves Moses (kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Sabasaba Moshingi ( wapili kulia) cheti maalum cha kushiriki Maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kabla ya kufungu maonyesho hayo kwenye uwanja wa Mashujaa mjni Dodoma Aprili 18, 2017. (Picha na Ofiai ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Meneja wa PPF wa Kanda ya Mashariki na Kati, Bw. Michael Christian cheti maalum cha kushiriki Maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kabla ya kufungu maonyesho hayo kwenye uwanja wa Mashujaa mjni Dodoma Aprili 18, 2017. (Picha na Ofiai ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikilza Bi. Evelyne Mandenje amabaye ni mmoja wa wajasiriamali walionufaika na mikopo inayotolewa na Benki ya TIB wakati alipotembelea banda la wasindikaji vyakula kabla ya kufungua Maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na watumishi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) wakati alipotembelea banda la benki hiyo kwenye maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali aliyoyafungua kwenye uwanja wa Mashujaa mjni Dodoma Aprili 18, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama wakijadili jambo katika maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma Aprili 28, 2017. Kulia ni Afisa Mwandamizi wa Fedha wa Benki ya TIB, Kenneth Lusesa(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amelitaka Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), lianze kufanya tathmini ya kisayansi kuhusu manufaa ya Mifuko yote ya uwekezaji nchini ili kujiridhisha endapo inawanufaisha wananchi kama ilivyokusudiwa.

Pia amelitaka baraza hilo lifanye tathmini kuhusu namna ya kuunganisha mifuko hiyo bila ya kuathiri majukumu ya msingi na mantiki ya kuanzishwa kwake, ili inayofanya kazi zinazofanana iunganishwe .
Ametoa agizo hilo leo (Jumanne, Aprili 18, 2017) wakati akifungua maonesho ya mifuko ya uwezeshaji katika uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma. Amesema uzinduzi wa maonesho hayo ni fursa nzuri kwa wananchi kuweza kudadisi kuhusu huduma zitolewazo na Mifuko hiyo na kutoa ushauri, ili kuboresha huduma.

“Lengo ni kuwa na Mifuko michache, lakini inayobadilisha maisha ya wanufaika, ambao ni wananchi. Nitafurahi kupata taarifa hiyo kabla au ifikapo Mwezi Mei, 2018,” amesema.

Aidha, Waziri Mkuu amesema mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi yanayofanywa na Serikali yanalenga kuwawezesha Watanzania wengi wafanye shughuli za kujiongezea kipato bila kusumbuliwa na baadhi ya Watumishi wasio waadilifu.

Ameongeza kuwa “uwezeshaji wananchi kiuchumi ni jambo ambalo lipo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025; Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2016/2017 – 2020/2021,”.

Amesema kuwawezesha wananchi kiuchumi, sio ubaguzi wala upendeleo, bali ni jitihada za makusudi za kuwashirikisha wananchi walio wengi ambao kwa sababu za kihistoria, wamejikuta wakiwa nje ya mfumo rasmi wa kiuchumi, hivyo kubaki kwenye hali duni jambo ambalo ni hatari kwa ustawi na usalama wa nchi.

Waziri Mkuu amesema jitihada za uwezeshaji wananchi kiuchumi zilizoanza tangu Serikali ya Awamu ya Kwanza na kuendelezwa na awamu zote zilizofuata, ambapo kwa sasa kuna mifuko 19 ya kuwezesha wananchi kiuchumi.

Amesema mifuko hiyo imesaidia upatikanaji wa mitaji kwa wajasiriamali na kupunguza kiwango cha umaskini nchini. “Hadi kufikia mwaka 2016 Mifuko hiyo kwa pamoja ilikuwa imetoa mikopo yenye thamani ya sh. trilioni 1.759 kwa wajasiriamali 400,000.

Awali Katibu Mtendaji wa NEEC, Bi. Beng` Issa alisema maonesho hayo ya siku nne yatawezesha kuwaongezea wananchi uelewa juu ya shughuli zinazofanywa na mifuko ya uwezeshaji.

Amesema kati ya mifuko 19 ya uwezeshaji mifuko 13 imeweza kushiriki katika maonesho hayo ya kwanza kufanyika nchini, ambapo kauli mbiu ya maonesho hayo ni “Wezesha wananchi kiuchumi ili kujenga uchumi wa kati na Tanzania ya viwanda”

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB Bank PLC, Bw. Sabasaba Moshingi aliyezungumza kwa niaba ya washiriki alisema madhumuni ya maonesho hayo ni kukuza uelewa juu ya uwepo wa mifuko ya kuwezesha wananchi kiuchumi na fursa zitolewazo na mifuko hiyo.

Pia kuhamasisha wananchi juu ya kujijengea utamaduni wa kujiwekea akiba na kuwekeza katika miradi yenye kuleta faida pamoja na uanzishwaji na uimarishwaji wa vikundi na miradi ya kiuchumi ili kuunganisha wananchi na fursa za huduma ya mikopo, mafunzo na huduma nyingine zinazotolewa na mifuko hiyo.

No comments: