Friday, March 24, 2017

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Rais Dr John Pombe Magufuli amewaapisha mawaziri wawili kufuatia marekebisho kidogo aliyoyafanya kwenye baraza la mawaziri hapo jana. https://youtu.be/wT6aeZ1SUfY

SIMU.TV: Rais Dr John Pombe Magufuli amepokea hati za utambulisho kwa mabalozi sita walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa Tanzania. https://youtu.be/6CJT2hTZN7U

SIMU.TV: Jengo la Raha Tower lililopo barabara ya Bibi titi jijini Dar es Salaam limenusurika kuungua baada ya kuzuka moto uliosababishwa na hitilafu ya umeme. https://youtu.be/zwjJPy6YATI

SIMU.TV: Serikali imepiga marufuku shughuli za utafutaji na uchimbaji wa madini katika eneo la hifadhi ya mazingira la Amani katika wilaya ya Korogwe na Muheza mkoani Tanga. https://youtu.be/uFqEZECyXuQ

SIMU.TV: Zaidi ya shilingi 9.9 zilizotolewa na benki ya dunia zinatarajiwa kutumika katika utengenezaji wa barabara kwa kiwango cha lami katika manispaa ya Musoma. https://youtu.be/NGPrd8oJb5U

SIMU.TV: Kamati ya Bunge ya miundo mbinu leo imetembelea mradi wa reli unatoa huduma ya usafiri kutoka eneo la Pugu hadi Stesheni jijini Dar es Salaam ili kujionea namna huduma hiyo inavyotolewa kwa wananchi. https://youtu.be/LsW8LNkUQZ4

SIMU.TV: Serikali imeombwa kuijenga kwa kiwango cha lami barabara ya Kamanga hadi Sengerema mkoani Mwanza ili kuwaondolea wananchi adha ya usafiri kipindi cha mvua. https://youtu.be/-nMyzdGGQR0

SIMU.TV: Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema serikali ina utashi wa dhati wa kuboresha mazingira ya uwekezaji kwa kuondoa urasimu na rushwa katika uwekezaji. https://youtu.be/GhlG_B-A6p4

SIMU.TV: Vijana wajasiriamali zaidi ya sabini wanaojihusisha na ufyatuaji wa matofali katika eneo la Mbagala jijini Dar es Salaam wameiomba serikali kuwasaidia eneo mbadala la kufanyia shughuli zao kutokana na kuondolewa eneo wanalofanyia kwa sasa. https://youtu.be/Ni20XNz7dUM

SIMU.TV: Wafanyabiashara katika kata ya Hasanga wilayani Mbozi wameiomba serikali ya halmashauri hiyo kuwapa eneo la soko kutokana na kukosa eneo la kufanyia biashara zao. https://youtu.be/ARWwvsCvD2A

SIMU.TV: Rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar amewataka viongozi wa Soka visiwani humo kutopeleka masuala ya soka mahakamani ili kuiepusha migogoro katika sekta ya mchezo wa soka. https://youtu.be/Gh8OmAE9VVE

SIMU.TV: Nahodha wa timu ya taifa Taifa Stars Mbwana Samatta amesema wakati umefika kwa watanzania kukubaliana na mabadiliko anayoyafanya kocha Mayanga. https://youtu.be/H-hwEBIIiQk

SIMU.TV: Ofisi ya mwanansheria mkuu wa nchini Uswisi imemhoja Franz Anton Beckenbauer kuhusu njia walizotumia kupata wenyeji wa kombe la dunia la mwaka 2006. https://youtu.be/O5by5E8_avI

Rais Dkt John Magufuli amewataka watanzania kuwa wazalendo na kuachana na vitendo vya Uchochezi vitakavyopelekea kuvunjika kwa amani; https://youtu.be/n8-t814yZ2M  

Kamati ya kudumu ya Bunge ya hesabu za serikali imemtaka wakala wa majengo ya Serikali TBA kuangalia upya bei za nyumba wanazojenga; https://youtu.be/QqCJiEn10bI

Kamati za ulinzi na Usalama wilayani Kongwa na Kiteto zimewataka wananchi waliovamia chanzo cha maji kilichopo mpakani mwa wilayani hizo kuondoka maramoja; https://youtu.be/RkhzjFEQCMI

Wajumbe wa kamati za ulinzi na usalama kwa mikoa ya Magharibi wamekutana mkoani Kigoma na kupanga mikakati ya kupambana na wahalifu; https://youtu.be/NgFt7yuhh28

Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme amewataka wananchi mkoani Dodoma kutambua kuwa kuhamia kwa serikali mkoani humo ni Fursa kubwa; https://youtu.be/5X0pYV-Kwdg

Fahamu hapa biashara mpya ya Ufugaji wa Vipepeo unavyoweza kukuletea kipato kikubwa katika maisha yako; https://youtu.be/0t-DJhSOZmw

Jumla ya wakulima na wafugaji zaidi ya laki moja wamenufaika na mradi wa kuboresha kilimo unaoendeshwa na shirika moja lisilo la kiserikali; https://youtu.be/VEoT7W5ckEY

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amewataka wafanyabiashara nchini Mauritius kuja kuwekeza nchini Tanzania katika nyanja mbalimbali; https://youtu.be/hbsWHFJ8wRM

Timu ya Taifa ya Tanzania kesho itashuka dimbani kucheza mchezo wa kirafiki unaotambulika na FIFA dhidi ya timu ya Taifa ya Botswana; https://youtu.be/FuQs5Yu3DuI

Wanamasumwbi hapa nchini wamesema waziri mpya wa Michezo Dkt Mwakyembe ni mtu sahihi kwani hata sheria anaifahamu vizuri; https://youtu.be/6WJ6XHpgpCc

Furahia habari mbalimbali za michezo kutoka anga za kimataifa tulizobahatika kukusogezea  kwa siku ya leo; https://youtu.be/3BshZ6Fa_VINo comments: