Katibu
wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama akiwa
kwenye mmoja ya mikutano ya kampeni wa kumtafuta diwani wa kata ya
Igombavanu wilayani mufindi akikitumikia chama.
Katibu
wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama akiwa
kwenye mmoja ya mikutano ya kampeni akimwombea kura Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Maguli mwaka 2015 katika uwanjwa wa
wambi mafinga.
Katibu
wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama akipeana
mkono na waziri mkuu mstaafu wa awamu ya nne mh Mizengo Pinda kwenye
moja ya majukumu ya kukitumikia chama.
Katibu
wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama akipeana
mkono na Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na
kubadilishana maneno ya hapa na pale.
Na Fredy Mgunda, Mufindi
KATIBU
wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama
ametangaza nia ya kugombea nafsi ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa Bunge la
afrika mashariki kwa kuiwakirisha Tanzania.
Akizungumza
kwa njia ya simu Mhagama alisema kuwa atahakisha lugha ya kiswahili
inatumika barani afrika kama lugha mama kwa kuwa ndio lugha ilisamba
zaidi barani afrika.
“Nimetembea
nchi nyingi hapa afrika nimekutana na watu wengi wanazungumza Kiswahili
hivyo hoja yangu itakuwa kuahakikisha natimiza kitu alichotuachia
hayati baba wa taifa mwalimu Julias Kabarage Nyerere”.alisema Mhagama
Mhagama
alisema kuwa atalazimaka kuwatetea wakulima kwa kuwa asilimia kubwa ya
watanzania wengi ni wakulima na uchumi wetu bado unategemea kilimo hivyo
ni lazima kuwekeza nguvu kwenye kilimo chenye tija na kufanikiwa kuinua
mazao yanayozalishwa hapa nchi na kukuza uchumi.
“Tanzania
tumebatika kuwa na ardhi nzuri na kubwa ambayo kwa asilimia kubwa bado
haijatumika kwa mjibu wa wataalam wa kilimo hivyo ni lazima kutafuta nja
mbadala ya kuwainua wakulima hawa ili kuviwezesha viwanda vyetu kupata
mali ghafi nyingi na za kutosha ili kuinua kipato cha kila sekta hapa
nchi”.alisema Mhagama.
Aidha
Mhagama amewataka watanzania kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa kazi anazozifanya kwa kutafuta
njia bora ya kuinua uchumi wa wananchi wake kutoka hapaulipo hadi
kufikia uchumi wa viwanda kama sera yake alivyoielekeza kwenye Tanzania
ya viwanda.
“Angalia
sasa tunapata wawekezaji wengi kwenye sekta ya viwanda hii ni dalili
nzuri ya kuukalibia uchumi wa viwanda hivyo nikiwa mbunge wa bunge la
Afrika Mashariki nitandelea kuunga mkono Rais kwa kutafuta njia za
kuwanua wawekezaji wazawa ili waboreshe na kuanzisha viwanda
vyao”.alisema Mhagama
Mhagama aliwaomba watanzania kwa ujumla kumuombea ashinde kiti hicho ili aweze kuiwakirisha vyema nchi kwa uadilifu uliotukuka
No comments:
Post a Comment