Mhe. Kairuki akimsikiliza mmoja wa watumishi wa Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kanda ya nyanda za juu kusini jijini Mbeya alipowapa fursa watumishi hao kutoa maelezo ya vikwazo wanavyopambana navyo .
Katibu wa Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma , Erick Mbembati (aliyevaa suti nyeusi) akimwonyesha Mhe. Angellah Kairuki kiwanja kinachotarajiwa kujengwa Ofisi za sekretarieti hiyo jijini Mbeya.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, mhe. Angellah Kairuki akifungua bomba la maji lililojengwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF – katika kijiji cha Majengo katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, wa kwanza kushoto ni mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga.
Waziri Kairuki akimwangalia Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Ladislaus Mwamanga anayekunywa maji kutoka kisima kilichochimbwa na TASAF katika eneo la Majengo ,Wilayani Mbarali ,mkoani Mbeya.
Waziri Angellah Kairuki akikagua kwa dhati moja ya kitambusho cha mlengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini unaotekelezwa na TASAF katika kijiji cha Majengo ,wilaya Mbarali mkoani Mbeya wakati alipofanya ziara ya kikazi mkoani hu. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF , Ladislaus Mwamanga.
Hapa ni furaha kubwa,Waziri wa nchi ofisi ya Rais menejimenti ya Utumishi wa umma na utawala bora, Angellah Kairuki akiwa ameketi katika nyumba iliyojengwa na mmoja wa walengwa wa TASAF katika kijiji cha Majengo, Gervas Ngei (mwenye shati ya drafti) kushoto kwa Waziri ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga aliyevaa miwani.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na mmoja wa walengwa wa TASAF Bw. Gervas nje ya nyumba aliyoijenga kwa kutumia fedha za ruzuku zinazotolewa na Mfuko huo kwa takribani kaya milioni MOJA NA LAKI MOJA nchini kote. Mwenye suti nyeusi ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga.
Waziri Angellah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa TASAF na halmashauri ya wilaya ya Mbarali nje ya nyumba iliyojengwa na mmoja wa walengwa wa Mfuko huo katika kijiji cha Majengo , Gervas Ngei kwa kutumia fedha alizozipata baada ya kulima mpunga kwa ruzuku hiyo.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, Mhe. Angellah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma Kanda ya Nyanda za juu kusini jijini Mbeya.
No comments:
Post a Comment