Benki
ya KCB Tanzania imeendelea kuwekeza kwa wajasiriamali wadogo na wakati
kupitia kitengo chake cha “Biashara Club”, kitengo kinachohudumia
wajasiriamali wadogo na wakati yaani (SME) kwa kuwapa huduma za kibenki
na huduma endelevu za kimaendeleo kwa wateja wake.
Zaidi
ya wanachama 100 wa Biashara Club wamekutana kujifunza jinsi ya kutunza
fedha, jinsi ya kufanya kwa vitendo uwekaji wa kumbu kumbu za hesabu ,
jinsi gani taarifa ya fedha za biashara yako na taarifa za kifedha za
mtu binafsi zinavyokusanywa na kukaguliwa, na kwa njia gani taarifa hizi
zinapatikana kwenye taasisi za mikopo kupitia taasisi za kifedha.
Kwa
kuongezea, maelezo mafupi yalitolewa na Taasisi ya biashara, Viwanda na
kilimo Tanzania kuhusu utolewaji na uthibitishwaji wa vyeti halali kwa
bidhaa zinazo zalishwa hapa Tanzania, wao wamebobea katika kufanya
tafiti mbalimbali nchi nzima kwa kutumia mtandao wao na kuanzisha mfumo
maalumu kwa wajasiriamali wadogo na wakati,
kuzisaidia
taasisi za wajasiriamali wadogo na wakati, na kuwakutanisha wadau wa
misitu kwa pamoja na kufanya ushirika wa biashara kwa wadau na
kuwaunganisha wanachama na fursa zilizopo kwa washirika wa kibiashara wa
kimataifa. Akiongea kwenye warsha ya KCB Biashara Club iliyofanyika
kwenye hoteli ya Hyatt Jijini Dar es salaam,
Mkurugenzi
Mkuu wa KCB Bwana Godfrey Ndalahwa alisema kwamba, Benki ya KCB
inatambua umuhimu wa wajasiriamali wadogo na wakati katika kukuza uchumi
wa nchi. “ Dhumuni letu sio kutoa suluhisho yakinifu kwa masuala ya
kibenki tu bali pia ni kuwapa ujuzi na nyenzo zinazohitajika katika
kufanikisha biashara zao” Wanachama wa KCB Biashara club watapatiwa
ujuzi wa kutosha kupitia warsha mbalimbali ambapo ushauri wa kibiashara
utatolewa kutoka kwa wataalam waliothibitishwa.
Warsha
hizi zinatoa fursa kwa wajasiriamali wadogo na wakati kuwa kwenye
mtandao na kuwasiliana wao kwa wao na kushirikishina ujuzi bora wa
kibiashara. Katika kuongezea hili, pia wanachama watapata fursa ya
kusaidiwa na mameneja uhusiano wanaowasikiliza kwenye mahitaji yao ya
kifedha. Wanachama wa KCB Biashara club pia watanufaika na fursa
zilizopo nje ya nchi ambapo matawi ya benki za KCB yapo.
“
Ikiwa ni moja ya maidhinisho yanayotolewa na club hii, tumeweza kupata
maelezo kutoka kwa mtendaji wa KCB Biashara club Bwana Moses Odipo
ambaye ametushirikisha safari za kibiashara za mwaka 2017. Hii
itawawezesha wanachama wetu kushiriki kwenye safari za mkoa mpaka safari
za kimataifa katika kuwezesha biashara zao.Wanachama watahudhuria
maonesho ya kibiashara ya Kimataifa ili kujifunza jinsi wajasiriamali
wengine wa kiwango chao wanavyo jiendesha kwa dhumuni la kuboresha
biashara zao .
Wakati
akitoa mchanganuo wa KCB Biashara Club, Bwana Masika Mukule, mkuu wa
kitengo cha wateja masuala ya kibenki, alisema kwamba, Biashara club
imedhamiria kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wakati kwa kuwapa nyenzo
na kuhakikisha wana ujuzi sahihi wa kuendesha biashara zao na kutoa
dondoo juu ya taarifa za kifedha zinazohitajika na taasisi za kifedha
pindi wanapo omba mkopo.
“Mwaka
huu warsha yetu ina maudhui mazuri sana yaliyoandaliwa kwa kufuata
maoni yaliyotolewa kwenye warsha yetu ya mwaka jana na tunaamini mwakani
tutakuwa tumewawezesha baadhi ya wajasiriamali wadogo na wakati kufikia
kiwango cha wateja wa kiwango cha juu.Bwana Mukule aliendelea kusema
kwamba KCB wanazo bidhaa mbalimbali kwa ajili ya soko la wajasiriamali
wadogo na wakati ikiwa ni pamoja na Masharti ya mkopo, overdaft
facilities, Overdraft facilities, Bank Guarantees, Invoice Discounting,
Documentary letters of Credit, Asset Based Finance na Bills
Discounting.
Mbali
na hizi kitengo hiki kinatoa mikopo ya nyumba kwa wanao nunua,
matengenezo au kumalizia ujenzi, Advantage Banking na bidhaa za kibenki
kwa wateja wetu waliopo nje na ndani ya nchi .Wanachama wetu wana mengi
ya kupokea kutoka kwetu,” Alimalizia Bwana Mukule
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya KCB, Godfrey Ndalahwa akizungumza machache wakati wa warsha ya KCB Biashara Club iliyofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Jijini Dar es salaam leo.
Mkuu wa Kitengo cha Kiislamu wa Benki ya KCB, Rashid Rashid akitoa machache kwa wanachama wa Jukwaa la Kibiashara 'Biashara Club' iliyofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Jijini Dar es salaam. Mkuu wa kitengo kinachohudumia wajasiriamali wadogo na wakati (SME) ,Juma Abdul akiwakaribisha wageni waalikwa mbalimbali waliofika kuhudhuria Warsha hiyo iliyoandaliwa na benki hiyo ya KCB mapema leo jijini Dar.
Wanachama wa Jukwa la Kibiashara 'Biashara Club' wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri ukumbi humo mapema leo.
Wafanyabiashara wakifuatilia. Wanachama wa Jukwa la Kibiashara 'Biashara Club' wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo mapema leo asubuhi.
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya KCB, Godfrey Ndalahwa akizungumza machache wakati wa warsha ya KCB Biashara Club iliyofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Jijini Dar es salaam leo.
Mkuu wa Kitengo cha Kiislamu wa Benki ya KCB, Rashid Rashid akitoa machache kwa wanachama wa Jukwaa la Kibiashara 'Biashara Club' iliyofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Jijini Dar es salaam. Mkuu wa kitengo kinachohudumia wajasiriamali wadogo na wakati (SME) ,Juma Abdul akiwakaribisha wageni waalikwa mbalimbali waliofika kuhudhuria Warsha hiyo iliyoandaliwa na benki hiyo ya KCB mapema leo jijini Dar.
Wanachama wa Jukwa la Kibiashara 'Biashara Club' wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri ukumbi humo mapema leo.
Wafanyabiashara wakifuatilia. Wanachama wa Jukwa la Kibiashara 'Biashara Club' wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo mapema leo asubuhi.
No comments:
Post a Comment