Balozi. Modest J. Mero akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. António Guterres. |
Balozi. Modest J. Mero na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. António Guterres wakipeana mikono baada ya zoezi la kuwasilisha Hati za Utambulisho kukamilika |
Akizungumza baada ya makabidhiano ya Hati za Utambulisho, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Guterres alisema Umoja wa Mataifa unaishukuru Tanzania kwa jinsi inavyojitolea kwa hali na mali katika jitihada za kumaliza migogoro ya kisiasa katika Ukanda wa Maziwa Makuu.
Alitaja hatua zinazochukuliwa na Tanzania kurejesha amani DRC, Burundi na Sudan Kusini kuwa ni mfano wa kuigwa na kwamba anayo imani kwamba jitihada hizo hazitakoma mpaka nchi za SADC na EAC zote ziwe na utulivu wa kisiasa.Naye Balozi Mero akitoa neno la shukurani, alimuahidi Bw. Guterres ushirikiano wa karibu kati ya Tanzania na Umoja wa Mataifa katika kufanikisha malengo ya maendeleo na ulinzi wa amani.
Aidha, alimwonyesha matarajio iliyonayo Tanzania kwake kwa kuzingatia ushirikiano mzuri aliounesha wakati alipokuwa akishughulikia masuala ya wakimbizi duniani, ambapo kwa pamoja na serikali ya Tanzania waliweza kutekeleza mengi kwa mafanikio makubwa

No comments:
Post a Comment