Monday, March 6, 2017

BODI MPYA VETA YAAGIZWA KUANZA KUCHUKUA HATUA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET –Board) leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo Peter Maduki na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Dkt. Bwire Ndazi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET – Board) Peter Maduki akizungumza mara baada ya Bodi ya uzinduzi wa rasmi wa Bodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako na Kaimu Mkurugenzi wa VETA Dkt. Bwire Ndazi.
Kaimu Mkurugenzi wa VETA Dkt. Bwire Ndazi akizungumza mara baada ya Bodi ya uzinduzi rasmi wa Bodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET – Board) Peter Maduki (kushoto).
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akimkabidhi taarifa ya utekelezaji wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Mamlaka hiyo, Peter Maduki wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET –Board) leo Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akimsikiliza mmoja wa wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET – Board) kupitia Bakwata Suleiman Lolila (kulia) mara baada ya kuzindua Bodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti Mpya wa Bodi hiyo Peter Maduki (katikati).
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Bodi Mpya ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET – Board) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Waliokaa kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa VETA Dkt. Bwire Ndazi na Kushoto ni Mwenyekiti Mpya wa Bodi, Peter Maduki.

Picha na: Frank Shija – MAELEZO.


Na: Frank Shija, MAELEZO.

BODI ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET –Board) imeagizwa kuanza mara moja kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo utekelezaji wake umekuwa ukisuasua kwa muda mrefu huku kukiwa na fedha zilizotengwa kwa ajili ya utekelezaji miradi hiyo.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na wakati akizindua Bodi Mpya ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET –Board) leo Jijini Dar es Salaam.

Profesa Ndalichako ameshangazwa na kitendo hicho cha ucheleweshaji wa utekelezaji wa miradi hiyo huku kukiwa na shilingi takribani bilioni 14.5 zilizotengwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2016/207 kwa ajili ya kazi hizo.

“Inasikitisha kuona kuwa tunakaribia robo ya mwisho ywa mwaka wa fedha 2016/2017, huku karibu miradi yote ya maendeleo haijaanza kutekelezwa,isipokuwa ile tu ya kujengea uwezo na siyo ya ujenzi wa VETA ambazo ndiyo hitaji kubwa kwa sasa.”Alisema Profesa Ndalichako.

Ndalichako ameongeza kuwa Bodi hiyo inapaswa kuanza kazi mara moja ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua watendaji watakao bainiuka kuhusika katika ucheleweshaji wa kuanza kwa miradi hiyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo Peter Maduki amempongeza Waziri Ndalichako kwa kuwa muwazi katika kuelezea kutolridhishwa na udhaifu katika utendaji kwa baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka hiyo na kuahidi kushughulikia suala hili huku akiwataka wajisahihishe badala ya kusubiri kuwajibishwa.

“Mhe Waziri, maelekezo yako tumeyapokea, nikuahidi tu kuwa mimi pamoja na timu yangu tutayafanyika kazi, ni nisememe wazi tupo tayari kushirikiana nawe wakati wowote,” alisema Mduki.

Awali akisoma maelezo mafupi kuhusu Bodi ya Mamlaka hiyo wakati, Kaimu Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi(VETA) Dkt. Bwire Ndazi amebainisha changamoto kadhaa katika eneo hili la utoaji wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi kuwa ni pamoja na uwezo mdogo wa VETA na wadau katika kufikia mahitaji ya elimu na mafunzo ya ufundi akitolea mfano kuwa watu wanaohitaji kujiunga na mafunzo wanakadiriwa kuwa laki sita kwa mwaka, uwezo wa vyuo vyote vya VETA, VYA Serikali na binafsi ni kati ya 125,000 tu kwa mwaka.

Bodi iliyomaliza muda wake iliundwa Agosti 2011 na kumaliza muda wake kisheria Agosti 2014, na baadaye kuongezewa muda hadi desemba 2016 alipoteuliwa Mwenyekiti Mpya wa Bodi hiyo yenye jumla ya wajumbe 10 kutoka maeneo ya ujuzi mbalimbali.

No comments: