Katibu tawala wilaya ya Iringa Joseph Chitinka akiwasalimia wachezaji wa timu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IMFC) kabla ya mchezo kati yao dhidi ya timu ya kijiji cha Mangalali uliochezwa katika uwanja wa kalenga kwenye mashindano ya Mbuzi Cup. Katibu tawala wilaya ya Iringa Joseph Chitinka akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IMFC) kabla ya mchezo kati yao dhidi ya timu ya kijiji cha Mangalali uliochezwa katika uwanja wa kalenga kwenye mashindano ya Mbuzi Cup.
Katibu tawala wilaya ya Iringa Joseph Chitinka akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya kijiji cha Mangalali kabla ya mchezo kati yao dhidi ya timu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IMFC) uliochezwa katika uwanja wa kalenga kwenye mashindano ya Mbuzi Cup.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
MASHINDANO
ya kombe Mbuzi Cup yatafikia tamati tarehe 30 mwezi wa tatu kwa
kuzikutanisha timu za Mkwawa Rangers na Waandishi wa habari mkoa wa
Iringa na fainal hiyo itachezwa katika kijiji cha Kalenga kata ya
Kalenga wilayani Iringa mkoani Iringa ikiwa lengo la kuinua vipaji wa
wachezaji kata hiyo.
Akishudia mchezo wa nusu fainal kati ya timu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IMFC) na timu ya kijiji cha Mangalali uliochezwa katika uwanja wa kalenga katibu tawala wilaya
ya Iringa Joseph Chitinka ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema ni wakati
mzuri kwa sasa kuyageukia mashindano ya mchangani kwani yamesheheni
vipaji vingi vitakavyosaidia kuendeleza mpira wa Tanzania wakati ambapo
taifa likiendelea kupata matokeo yasiyoridhishwa kwenye soka kwa sasa,
"Mashindano
haya ni muhimu sana kwa wakati huu kwani yatasaidia kuinua vipaji vya
vijana wetu na kuweza kupata timu bora ya taifa hivyo nidhamu ni muhimu
wakati wa michezo hiyo" alisema Chitinka
Aidha
Chitinka aliongeza kwa kusema kuwa mpira wa miguu umekuwa na faida kwa
wachezaji kwani wanaweza kujitengezea vyanzo vya ajira kama mbwana
samatta na wachezaji wengine walipwa vizuri saizi hapa nchini hata nje
ya nchi.
“Mwaka
huu tumekuja na wataalamu wanachagua vipaji maalumu kwaajili ya
kujiunga na timu mbalimbali na lengo likiwa ni kuhakikisha vipaji vyote
vinaonekana na vinafika mbali kwa kuwa sasa mpira ni ajira si mnamuana
mchezaji Mbwana Samatta”.alisema Chitinka
Mwenyekiti
wa Kamati ya Mashindano hayo Obeid Msigwa aliwataka washiriki wa
mashindano hayo kujituma ili ipatikane timu ya bora ambayo itakuwa
ikiwakilisha katika mashindano ya mbalimbali.
“Soka
imewapa ajira mamilioni ya wachezaji na viongozi ulimwenguni na
wameweza kuishi maisha ya kifahari kutokana na mishahara wanayopata”,
alisema Msigwa
Kwa
upande wake mlezi wa mashindano hayo kamanda wa vijana wa chama cha
mapinduzi (ccm) wilaya Iringa Jackson Kiswaga alisema ataendelea
kwaunganisha vijana kupitia michezo na kusaidia kukuza mpira wa wilaya
ya Iringa.
“Ilani
ya chama cha mapinduzi inatutaka mwenyeviti kote nchini kuhakikisha
michezo inafanyika mara kwa mara na kuleta tija kwa taifa ili tuondokane
kuwa kuwa vichwa vya wendawazimu”alisema Kiswaga.
Mashindano
ya Mbuzi Cup ni miongoni mwa mashindano yanayolenga kuibua vipaji vya
vijana vijijini ili kuwawezesha kupata nafasi ya kucheza katika vilabu
vikubwa nchini.
No comments:
Post a Comment