Monday, February 13, 2017

WANANCHI WA MKOA WA DODOMA WAPIMA AFYA ZAO KATIKA BANDA LA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE NA KUPATA ELIMU YA AFYA

Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Andrew Kabeho akimpima mapigo ya moyo Afisa Muuguzi wa Hospitali ya mkoa wa Dodoma Mariam aliyefika katika banda la Taasisi hiyo kwa ajili ya kupima magonjwa ya moyo. JKCI ilishiriki katika kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi na kupima afya bila malipo iliyoandaliwa na Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto na kufanyika katika uwanja wa Jamhuri jumla ya wagonjwa 408 walihudumiwa katika banda hilo.
Mtaalamu wa Afya na Mazoezi ya viungo kutoka Chama Cha Wafanya Mazoezi Tanzania Waziri Ndonde akiwaelekeza wananchi waliokuwa wanasubiri kwenda kupima magonjwa ya moyo katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) umuhimu wa kufanya mazoezi na aina ya mazoezi wanayotakiwa kuyafanya. Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto hivi karibuni ilizindua kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi na kupima afya bila malipo kwa muda wa siku mbili kwa wananchi wa mkoa wa Dodoma.
Mtaalamu wa Dawa na Tiba kutoka Hospitali ya SANITAS Dk. Sajjad Fazel akiwafundisha wananchi waliokuwa wanasubiri kwenda kupima magonjwa ya moyo katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) aina ya vyakula bora wanavyotakiwa kula ili waepukane na magonjwa yasiyoambukiza. Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto hivi karibuni ilizindua kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi na kupima afya bila malipo kwa muda wa siku mbili kwa wananchi wa mkoa wa Dodoma.
Mratibu wa Magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa watu wazima na magonjwa ya saratani kutoka Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Sara Maongezi akiwafundisha wananchi waliokuwa wanasubiri kwenda kupima magonjwa ya moyo katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) aina za saratani na umuhimu wa kupima afya mara kwa mara. Hivi karibuni Wizara hiyo ilizindua kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi na kupima afya bure kwa muda wa siku mbili kwa wananchi wa mkoa wa Dodoma.
Twaha Dofa (aliyeshika karatasi) akitoka kupima magonjwa ya moyo katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi na kupima afya bila malipo kwa siku mbili iliyoandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto na kufanyika katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma. Picha na Anna Nkinda – JKCI
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Pedro Pallangyo akimsikiliza mtoto Oliva Mushi aliyefika katika banda la Taasisi hiyo kwa ajili ya upimaji wa magonjwa ya Moyo. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto ilizindua kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi na kupima afya bila malipo Mkoani Dodoma ambapo wananchi wa mkoa huo walipimwa afya zao bila malipo kwa muda wa siku mbili zoezi lililofanyika katika uwanja wa Jamhuri.

No comments: