Monday, February 13, 2017

Utamaduni wa Mtanzania ni Sehemu ya Kivutio cha Utalii: Waziri Nape.

NP1
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akizungumza wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania jana jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.
NP2
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Makumbusho ya Taifa Profesa Audax Mabulla akizungumza wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania jana jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.
NP3
Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mossa Farharng (wa pili kutoka kushoto) akifuatilia hotuba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye (hayupo pichani) wakati wa kilele cha Wiki ya Utamaduni wa Shiraz iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa Profesa Audax Mabulla, Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Iran Ali Bagheri na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.
NP4
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akicheza Bao na Mwenyekiti wa Shirikisho la Michezo ya Jadi Tanzania Bw. Mohamed Kazingumbe (kulia) wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania jana jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.
NP5
Baadhi ya Wasanii kutoka Iran wakitumbuiza muziki wa Ala wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania jana jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.
NP6
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akiangalia moja ya vitabu vyenye maneno ya Kishiraz wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania jana jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Bibi. Lilian Beleko, Balozi wa Iran nchini Mossa Farharng na Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Iran Ali Bagheri.
NP7
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akisikiliza maelezo kuhusu michoro ya Kiutamaduni ya Iran wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania jana jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.
NP8
: Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Utamaduni wa Bodi ya Filamu Tanzania Bw. Benson Mkenda alipotembelea meza ya Bodi hiyo wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania jana jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.
NP9
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akifurahia jambo mara baada ya kupata maelezo ya namna ya kufanya marekebisho ya Vitabu kutoka kwa Ali Navidogooe Shiraz wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania jana jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.
NP10
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akipiga Gitaa  lililotengenezwa na Msaanii wa Uchoraji na Uchongaji Bw. Washington Steven Masanja (kushoto) wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania jana jijini Dar es Salaam.Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”. Kushoto kwa Waziri ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.
NP11
Wasanii wa Mashairi Bw. Issa Amiri Kilimo aka. Kijoka Kidogo na Mwajuma Seleman Yombe wakiimba shairi kwa njia ya majibizano ikiwa ni kujibu shairi la Siri la mtunzi Haji Myaka bin Haji la mwaka 1405 jana jijini Dar es Salaam wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania.
NP12
Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mossa Farharng akimkabidhi zawadi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye  wakati wa kilele cha Wiki ya Utamaduni wa Shiraz iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam jana. 
NP13
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akifurahia jambo na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mossa Farharng wakati wa kilele cha Wiki ya Utamaduni wa Shiraz iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam jana. 
NP14
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mossa Farharng na baadhi ya viongozi kutoka taasisi za Serikali na ubalozi wa Iran wakati wa kilele cha Wiki ya Utamaduni wa Shiraz iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam jana. 
Picha na: Frank Shija – MAELEZO.
…………………………………………………………
Na Shamimu Nyaki-WHUSM.
 Serikali chini ya Wizara ya Hbari Utamaduni Sanaa na Michezo inaendelea na juhudi za kuhakikisha kuwa Utamaduni wa Mtanzania unakuwa sehemu ya muhimu ya kivutio cha Utalii ili kutengeneza ajira na kuingizia Serikali mapato.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye alipokuwa anafungwa maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa Washirazi yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa madhimisho haya yanaimarisha undugu wa damu wa kiuchumi na kiutamaduni ulioachwa na wahenga.
“Maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa Shirazi ni fursa pekee ya kujifunza kutoka kwa kwa wairani namna ya kukuza ,kulinda na kuendeleza Utamaduni,Sanaa,Filamu,Mila na Desturi zetu”Alisema Waziri Nape.
Aidha ameongeza kuwa Wizara yake  itaweza kufanikisha shughuli za Utamaduni na kuziendeleza  kwa kushirikiana na wadau  wa ndani na nje ya ya nchi  kama ilivyofanyika katika maadhimisho ya mwaka huu kwani yanatangaza vikundi vya Sanaa na Wasanii.
Kwa upande wa wake Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha Irani hapa nchini Bw.Ally Baghari amesema kuwa ushirikiano wa Kiutamaduni baina ya Tanzania na Irani umeongeza mafanikio ya kiuchumi na kijamii katika nchi hizo hasa kupitia ubadilishanaji wa Utamaduni tangu enzi za ukoloni.
“Tumejifunza utamaduni  wa kitanzania kupitia maadhimisho haya na tunaamini watanzania pia wamejifunza utamaduni wa Irani ambao umesaidia kuimarisha ushirikiano wetu”Alisema Bw Baghari.
Maadhimisho hayo yaliyokuwa na kauli mbiu “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.

No comments: