Monday, February 20, 2017

VITUO VINAVYONYAYASA WAGONJWA VILIVYOPO NDANI YA MPANGO WA HUDUMA YA AFYA (NHIF), KUFUTIWA USAJILI VIKIBAINIKA


Mwenyekiti wa bodi ya mfuko wa bima ya afya Taifa(NHIF)Anna Makinda akifungua mkutano wa wadau wa mfuko wa bima ya afya Mkoa wa Kagera katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Kaimu Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa bima ya afya(NHIF)Benard Konga akiongeo na wadau wa mfuko huo(hawapo pichani)wakati wa kikao cha wadau wa mfuko wa NHIF kilichofanyika leo Mkoani Kagera

Meneja wa mfuko wa bima ya afya(NHIF)Mkoa wa Kagera Elias Odhiambo akieleza changamoto na mafanikio ya mfuko katika Mkoa wa kagera kwa wadau wa mfuko wa Bima. 

Meneja wa mfuko wa bima ya afya Mkoa wa Kagera Elias Odhiambo akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo wakati wa kikao cha wadau wa mfuko huo,Kushoto ni Mwenyekiti wa bodi wa mfuko huo Anne Makinda Baadhi ya wadau wa mfuko wa bima ya afya wa Mkoa wa Kagera wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa mkutano wa wadau wa bima ya afya na viongozi kutoka makao makuu ya mfuko huo.Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kagera

MWENYEKITI wa Bodi ya mfuko wa Taifa wa bima ya afya(NHIF) Anne Makinda amesema kuwa kituo chochote kilichosajiliwa kwa ajili ya kutoa huduma ya afya kwa wateja wa mfuko wa bima ya afya, ambacho kimeajiri wahudumu wenye mfumo wa unyanyasaji kwa wagonjwa ikiwemo Lugha za kejeli kwa wateja vitaondolewa kwenye mpango wa huduma ya afya.

Makinda alisema hayo leo wakati wa mkutano wa wadau wa NHIF na CHF Mkoani Kagera katika ukumbi wa mikutano wa mkuu wa mkoa wa Kagera Mjini Bukoba.

"Hivi wewe mtoa huduma wa afya unapotoa lugha ya kejeli na vitisho,matusi kwa wagonjwa unapata faida gani?,unapata fedha kiasi gani?sasa naagiza vile vituo ambavyo tumevisajiri kutoa huduma zetu ambavyo bado vinaendekeza mfumo wa kunyanyasa wagonjwa, sasa tunasema basi hatuwezi kuvumilia kinachofuata kuwafuatia sajili alisema Makinda.

Aidha aliwaagiza wamiliki wa vituo hivyo kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja kuweka mkakati madhubuti wa kuhakikisha wanaondoa kero hiyo haraka iwezekanavyo kwani watu wakijiunga na bima lengo ni wapate huduma stahiki ikiwemo mapokeo mazuri jambo ambalo linampa mgonjwa faraja hata kabla ya kupata dawa.

Pia aliwashauri wadau wa mkoa wa Kagera kutoa maoni yao hata kama mfuko huo una mapungufu ili kwa ushirikiano wa pamoja yaweze kutafutiwa ufumbuzi wa kina na huduma ziendelee kutolewa ipasavyo.

Kaimu mkurugenzi mkuu wa Nhif makao makuu Bernard Konga alisema kwasasa wamejikita katika kuboresha huduma na kuondoa chamgamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili wateja wao ambazo amezitaja kuwa ni,kupewa majina ya kejeri na watoa huduma wa afya kama vile nyie wa bure,unyanyapaa,uhaba wa dawa ikiwemo misongamano wa wateja ambapo kwa sasa zinaendelewa kutatuliwa kwa kina.

Meneja wa Nhif mkoa wa Kagera Elius Odhiambo alitaja changamoto zinazowakabili katika utendaji wao kuwa ni pamoja na kuwepo na vitendo vya udanganyifu na kughushi madai ya malipo kwa huduma za matibabu,mwitikio Mdogo wa wananchi kujiunga na mpango wa bima ya afya na ucheleweshwaji wa michango ya wanachama kwa baadhi ya waajiri.

Odhiambo alisema ili kukabiliana na changamoto hizo pia wamejiwekea mipango endelevu katika kufanya kazi zao ambapo ni pamoja na kuhamasisha watoa huduma ili watumie fursa ya mikopo ya vifaa,tiba,ukarabati wa majengo,dawa na vitendanishi ili kuboresha huduma za matibabu.

Pia kuendelea kuchukua hatua kali kupambana na vitendo vya udanganyifu kwa baadhi ya watoa huduma wasio waaminifu.

No comments: