Mkuu wa majeshi ya ulinzi Jenerali, Venance Mabeyo akisalimiana na Mkuu wa Majeshi Mstaafu Mirisho Sarakikya wakati akishiriki Mashindano ya Maadhimisho ya Miaka 10 ya Klabu ya Gofu ya Lugalo Jana Jijini Dar es Salaam.
Na Luteni Selemani Semunyu, JWTZ
Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania limepania kukuza Mchezo wa Gofu kwa kujenga Miundombinu na Viwanja vya kanda katika maeneo mbalimbali nchini kwa Kuanzia Mkoani Dodoma ambapo Serikali imetangaza kuhamia.
Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo wakati akifunga Mashindano ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu Kuanzishwa kwa Klabu ya Golf ya Lugalo Jana Jijini Dar es Salaam.
“ Tumeshapata eneo la Jeshi Dodoma hivyo Tutatumia uzoefu tulioupata kwa Ujenzi wa Klabu hii ili Kujenga Klabu ya Kisasa ya Gofu Mkoani Dodoma ili watakaokwenda Dodoma kikazi au kwa shughuli nyingine wasikose sehemu ya Kucheza Gofu.” Alisema Jenerali Mabeyo.
Mmoja wa Wachezaji wa Mashindano ya Maadhimisho ya Miaka 10 ya Klabu ya Gofu ya Lugalo ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa kamati ya Maandalizi Dkt Edmund Mndolwa akiwa katika harakati za Mchezo huo Jana Jijini Dar es Salaam.
Aliongeza kuwa mbali na Ujenzi wa Uwanja wa Golf Dodoma lakini pia kuna Uwezekano wa kujenga Viwanja vya kanda na Lugalo kuwa na mashina katika Mikoa ya Arusha,Morogoro,Mwanza na Simiyu ili kuchangia katika ukuzaji wa Michezo na ukizingatia Serikali imetilia Mkazo suala la Michezo kwa Wananchi.
Jenerali Mabeyo ambaye ni Mlezi wa Klabu hiyo alisema mbali na Ujenzi wa Viwanja hivyo vya Gofu lakini bado wataendeleza Uwanja wa Lugalo pale ambapo watangulizi wake wameishia na kuhakikisha unakuwa wenye sifa za kuchezeka wakati wote kwa kuangalia miundombinu ya Maji.
“ Nilikuwa naongea na mwenyekiti kamati ya mashindano Dk Edmund Mndolwa alinidokeza tatizo la kukauka kwa Uwanja kipindi cha Kiangazi na kutochezeka Vizuri nimelichukua na tutalifanyia kazi tunashukuru Afande waitara kwa Ubunifu na namshukuru Mtangulizi wangu Jenerali Mwamunyange kwa kuilea klabu kwa Mafanikio nami kwa kushirikiana na Wanachama nitaendeleza ili klabu izidi kuimarika”. Alisema Jenerali Mabeyo.
Mkuu wa majeshi ya ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akikabidhi Zawadi kwa mshindi wa Jumla wa Mashindano ya Maadhimisho ya Miaka 10 ya Klabu ya Gofu ya Lugalo Amani Saidi Jana Jijini Dar es Salaam.
Pia aliwashukuru Waandishio wa habari na wadau Mbali mbali katika kuitangaza na kufanikisha shughuli mbalimbali zinazoandaliwa na Klabu hiyo kwa mafanikio makubwa na imejidhihirisha kutokana na Umati mkubwa uliojitokeza katika maadhimisho hayo.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Klabu hiyo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo alisema katika kipindi cha Miaka 10 wamepata mafanikio makubwa hivyo sasa licha ya kufanya uwanja kuwa na hadhi ya kimataifa na mpango maalumu wa ukuzaji vipaji kwa watoton lakini walenga kupata viwanja kwa ajili ya Michezo mingine ikiwemo kuogelea.
Aliongeza kuwa Lugalo itabaki kitovu cha Ukuzaji vipaji kutokana mpango maalum wa watoto ambao idadi yao sasa inafikia zaidi ya 50 ambayo ni kubwa ukilinganisha na Klabu zote nchini.
Kwa Upande Wake Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mashindano hayo Dkt Edmund Mndolwa alisema wanashukuru JWTZ kwa kutoa fursa kwa raia kushiriki katika Klabu hiyo hali iliyoondoa adha kubwa kwa wazalendo.
Mmoja wa Wachezaji wa Mashindano ya Maadhimisho ya Miaka 10 ya Klabu ya Gofu ya Lugalo Angel
Eaton akiwa katika Harakati za Mchezo huo Jana Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa majeshi ya ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo akikabidhi Zawadi kwa mshindi wa Jumla wa
Mashindano ya Maadhimisho ya Miaka 10 ya Klabu ya Gofu ya Lugalo Amani Saidi Jana Jijini Dar es
Salaam.
Baadhi ya Wasanii wa Ngoma kutoka kundi la Ngoma la Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Band
Coy wakitumbuiza wakati wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Klabu ya Gofu ya Lugalo Jana Jijini Dar es
Salaam.
Mshindi wa kundi la Wanawake wa Mashindano ya Maadhimisho ya Miaka 10 ya Klabu ya Gofu ya
Lugalo Vicky Elias akiwa katika Harakati za Mchezo huo Jana Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment