Bwana Jackson Oganga akiwa anatoa maelezo kwa vijana jinsi ya kupata 'Scholarship' katika zinazotolewa sehemu mbalimbali.
Mwakilishi wa Asasi ya Kiraia Global Peace Foundation (GPF) Tanzania aliyewakilisha katika Semina hiyo Bi. Anna Mwalongo akielezea kwa kifupi kuhusu Asasi hiyo.
Mshauri wa mambo mbalimbali ya Kijamii na uchumi Bw. Anthony Luvanda akitoa masomo mbalimbali ya namna vijana wanavyoweza kujikwamua na kujitegemea kwa kufanya shughuli mbalimbali.
Baadhi ya vijana wakiendelea kusikiliza kwa makini mambo mbalimbali katika Semina Hiyo
Bi. Bernice Fernandes akielezea namna alivyopata nafasi ya kwenda kusoma Marekani kupitia 'Scholarship' na kuwasihi vijana wasikate tamaa kwa kuwa nafasi za kwenda kusoma nje zipo nyingi
Muandaaji wa Semina hiyo na Mwenyekiti wa UNESCO Youth Forum Bw. Frank Joash akieleza namna ambavyo vijana wanaweza kujiunga katika programu mbalimbali za Umoja wa Mataifa.
Mwakilishi kutoka Raleigh Bi. Alice Norbert akitoa maelezo namna ya vijana ambavyo wanaweza kushiriki shughuli mbalimbali za kujitolea katika Asasi mbalimbali za Kiraia.
Baadhi ya vijana wakiuliza maswali mbalimbali kwa wasemaji
Picha ya pamoja ya watoa mada mbalimbali Kutoka Kushoto ni Frank Joash,Anthony Luvanda, Evance Exaud,Alice Norbert, Anna Mwalongo, Bernice Fernandes, Nelson Amar na Jackson Ogonga.
Watoa Mada wakiwa pamoja na Baadhi ya washiriki waliohudhuria Semina hiyo
Picha na Fredy Njeje
Katika kuhakikisha vijana wanashiriki na kujikwamua katika mambo mbali mbali UNESCO Youth Forum waliandaa semina ambayo ilihusu vijana kushiriki katika programu mbalimbali za umoja wa mataifa, Kudumisha amani kutoka ngazi ya vijana na jamii kwa ujumla ambapo Global Peace Foundation Tanzania walitoa mafunzo juu ya maswala hayo, kuhusu kusoma nje na kuelekezwa njia mbali mbali za kufanya kazi kwa kujitolea katika asasi mbalimbali za kiraia.
Akizungumza na vijana hao kutoka vyuo mbalimbali na wale ambao walimaliza vyuo mwakilishi wa asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation(GPF) nchini Tanzania Bi. Anna Mwalongo alisema kuwa Global Peace Foundation ni Taasisi isiyo ya kiserikali,ambayo si ya kidini na haitengenezi faida ya aina yoyote ile ina makao yake makuu katika jiji la Washington DC nchini Marekani na lenye matawi yapatayo 23 duniani kote, yakiwemo mabara ya Afrika,Ulaya, Asia na Marekani ni “Taasisi hii kwa Tanzania ilianzishwa kati kati ya Mwaka juzi 2015 ambapo pamoja na uchaga wake wameonesha juhudi kubwa katika kuhamasisha amani nchini kuanzia ngazi ya familia na jamii kwa ujumla.” Alisema Anna.
Aliongeza kuwa Mnamo mwezi wa saba mwaka 2015 Global peace foundation waliandaa Mkutano mkubwa wa amani uliofanyinka Zanzibar uliojulikana kwa jina la Global peace Leadership Conference (GPLC Zanzibar) ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Makamu wa pili wa Rais Mh. Balozi Seif Ali na kuhudhuriwa na marais wastaafu kutoka nchi mbalimbali.
"Kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015 walifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuendesha kampeni ya “AMANI KWANZA” ambapo aliwalenga wanawake na vijana kushiriki katika uchaguzi huo kwa amani, alimalizia kwa kusema kuwa kwa sasa GPF wanampango wa kupanua wigo zaidi ili kuwafikia watanzania wengi zaidi kueleza mambo mbalimbali ya amani kupitia kampeni yao ya “VIJANA NA AMANI” " Alisema Anna
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UNESCO Youth Forum Bw. Frank Joash alisema vijana wengi hawana uwelewa wa program mbali mbali za umoja wa mataifa hivyo waliamua kuwakutanisha ili kuwapa uelewa ili wapate kujiunga.
Nae Bi. Bernice Fernandes pamoja na Bw. Jackson Oganga ambao walishawahi kusoma nje ya nchi kupitia ufadhili ‘Scholarship” walielezea kwa kina namna walivyo fika huko, changamoto na jinsi zinavyotokea na kuwasihi vijana hao kutokata tamaa na kuendelea kuomba nafasi hizo mpaka pale watakapo fanikiwa nao kutimiza ndoto zao za kwenda kusoma nje.
Mwisho Mshauri na mwezeshaji katika mambo mbalimbali ya Bw. Anthony Luvanda aliwasihi vijana kujitambua na kufahamu vipaji vyao na kujua namna ya kutimiza ndoto zao, ambapo aliwaomba pia vijana wasitegemee sana kazi za kuajiliwa bali wawe na mawazo chanya ili kuweza kutimiza malengo yao
Semina hiyo ilihudhuriwa na vijana kutoka vyuo vya, Chuo kikuu cha Dar es salaam, DUCE,TIA, NIT,Bagamoyo University,DIT na TIA , wanavyuo waliomaliza pamoja na vijana wengine ambapo jumla yao walikuwa zaidi ya 196.
No comments:
Post a Comment