Mkuu
wa mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo(kushoto)akipokea kutoka kwa Mhandisi
Shin Pil Soo sehemu ya msaada mabati 300 na mifuko ya Sementi 500
iliyotolewa na Kampuni ya ujenzi ya Hanil Jiangsu Joint Venture Ltd
inayojenga barabara ya Sakina hadi Tengeru yenye urefu wa kilometa 14.1
,kulia ni Meneja wa Tanrods mkoa wa Arusha,Mhandisi John Kalupale,msaada
huo umetolewa kwa Mkuu wa mkoa ili umwezeshe kusaidia shughuli za
maendeleo zilizoanzishwa na wananchi na alikabidhi ili utumike kwaajili
ya ujenzi wa Kituo cha Afya Makuyuni wilayani Monduli.
Mkuu
wa mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo akishirikiana na askari wa JKT kambi ya
Makuyuni na wananchi wa Kata ya makuyuni katika ujenzi wa Kituo cha
Afya katika ziara yake wilayani Monduli.
Mkuu
wa mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo(katikati) akilakiwa na wanafunzi wa
Shule ya Sekondari Rifit Valley Kata ya Majengo wilaya ya
Monduli,kushoto ni Mkuu wa wilaya hiyo,Idd Kimanta na kulia ni Mkuu wa
Shule,Julius Maghembe.
Mkuu
wa Shule ya Sekondari Rift Valley ,Julius Maghembe akiinua Sh 500,000
zilizotolewa na Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho gambo kwaajili ya kununua
viti vitano vya walimu.
Mkuu
wa mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo(kushoto) akiwa na viongozi wa wilaya ya
Monduli ndani ya moja vya vyumba viwili madarasa vilivyozinduliwa baada
ya ujenzi wake kukamilika katika Shule ya Sekondari Rifit Valley.
Wananchi wakichangia nguvu zao katika ujenzi wa jengo la Upasuaji kwenye Kituo cha Afya Mto wa Mbu
Mkuu
wa mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo akishiriki kazi za mikono pamoja na
wananchi katika ujenzi wa jengo la Uapsuaji katika Kituo cha Afya Mto wa
Mbu aliahidi kutoa mifuko 100 ya Sementi na Mabati 100.
No comments:
Post a Comment