Thursday, February 9, 2017

UKAGUZI WA MABASI KATIKA I KITUO CHA UBUNGO WAPAMBA MOTO , ABIRIA WAPONGEZA UKAGUZI WA MABASI

Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii.

Abiria wa walioshushwa  katika basi la Shukurani Coach linalofanya safari zake Dar kuelekea mikoa ya Kusini wamesema ukaguzi unaofanyika katika kituo cha mabasi ubungo ni mzuri kwani safari yao isingekuwa  nzuri kama wangeweza kupita bila kukaguliwa.

Akizungumza na Michuzi Blog, Shinza Lymo amesema kuwa utaratibu wa ukaguzi kabla ya basi kondoka uendelee kwa wamiliki watakuwa hawapeleki basi katika kituo hicho na kuwa wameweepusha abiria na ajali zinazotokana na uzembe.

Nae Halima Bakari amesema kuwa katika siku ambayo hatasahau ni kuzuiwa kwa basi hilo ambapo leo kitu ambacho kingetokea ni makosa ya watu kushindwa kufanya matengenezo ya mabasi wakati yanaingia katika kituo hicho .

Amesema jeshi la polisi wamekuwa makini katika kuhakikisha wanaokoa roho za watu ambao wanasafiri na vyombo vya moto hasa mabasi ya mikoani ambayo basi moja linabeba roho 100.

Kwa upande wa dereva Simwanzi Minja amesema kuwa jeshi la polisi limenyoosha wamiliki wa mabasi ambao hawataki kupeleka mabasi  yao Gereji na kituo  cha ukaguzi wa mabasi  cha ubungo kinazua safari.
Amesema kuwa kutokana na ukaguzi huo ajali zimepungua zinazotokana na mabasi mabovu kubaki matatizo ya kibinadamu ambayo nayo yamedhibitiwa ipasavyo.

Chami amesema kuna siku alimwambia mmiliki wa basi kuwa basi lake linamatatizo alikata na kuamuka kuita polisi kufanya ukaguzi ili walizuie kufanya safari kabla hajafanyiwa ukaguzi akiwa na abiria.
Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Geita Mponjoli Mwabulambo akipata maelezo  kwa Mkuu wa Usalama Barabarani  Kituo cha Mabasi ya Mikoani cha  Ubungo, Ibrahim Samwix a juu ya ukaguzi wanaofanya kabla ya mabasi hayo kuondoka kuelekea mikoani  alipofika kituo hicho kwa shughuli za kawaida.Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
 Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo akimueleza Mkuu wa Usalama Barabarani  Kituo cha Mabasi ya Mikoani cha  Ubungo, Ibrahim Samwix  juu ya utaratibu wanaoufanya katika ukaguzi wa magari na kuwapongeza kwa hatua wanazozichukua kwa basi itakayoonekana na tatizo leo jijini Dar es Salaam.
 Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita ,Mponjoli Mwabulambo akiangalia ukaguzi unaofanywa katika kituo cha mabasi ubungo kabla ya mabasi hayo hayajaanza safari leo jijini Dar es Salaam na Basi hilo ni Shukrani  Coach ambalo limezuiliwa kufanya safari zake leo baada ya kubaini usukani wake hauko leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Usalama Barabarani  Kituo cha Mabasi ya Mikoani cha  Ubungo, Ibrahim Samwix akikagua injini ya basi kabla halijaanza safari zake leo ubungo jijini Dar es Salaam.
 .Abiria akilalamikia kurudishiwa nauli katika basi alilotaka kusafiri nalo leo ambalo limerudishwa kituoni  kutokana na kuwa na matatizo  kwenye injini yake kabla halijaanza safari zake leo ubungo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Usalama Barabarani  Kituo cha Mabasi ya Mikoani cha  Ubungo, Ibrahim Samwix aking’oa namba za usajili katika basi CM  Millenium  linalofanya safari za Dar es Salaam  kuelekea Mtwara baada ya kubaini basi hilo linatatizo  na baadae baadae limekufa injini yake kabla halijaanza safari zake leo ubungo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Usalama Barabarani  Kituo cha Mabasi ya Mikoani cha  Ubungo, Ibrahim Samwix   (katikati) akitoa maelekezo kwa askari wake leo katika kituo cha ubungo jijini Dar es Salaam.









No comments: