Thursday, February 9, 2017

BREAKING NEWZZZ: MANJI AJISALIMISHA POLIS KUTII AGIZO LA MKUU WA MKAO PAUL MAKONDA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu Yusuf Manji amefika katika kituo cha kati (Central Police) kwa ajili ya mahojino.Manji ambaye ni mwenyekiti wa klabu ya Yanga aliwasili majira ya saa 5 asubuhi akiongozana na mawakili wake.Baada ya kuwasili, Manji alisalimiana na wanachama wa klabu ua Yanga na kuingia moja kwa moja kituoni kuendelea na taratibu nyingine.
 Mwenyekiti wa klabu ya Yanga ,Yusufu Manji akiwasili katika kituo cha Polisi Kati jijini Dar es Salaam mara baada ya kuamua kujipeleka hapo yeye mwenyewe kutii agizo la Mkuu wa Mkoa Paul Makonda,ambaye watuhumiwa wote 65 aliowataja jana katika sakata la dawa za kulevya,aliwataka kufika kesho Ijuma kituo cha Polisi kati kwa mahojiano zaidi.
 Yusufu Manji akipokelewa na baadhi ya wanachama wa Yanga katika kituo cha Polisi kati mara baada ya kujipeleka leo badala ya kesho
 Manji akisalimiana  na wanachama wa Yanga katika kituo cha Polisi Kati
 Mnaji akiwa akiwa ameongozana na mawakili wake na wasaidizi kuingia kituo cha kati jijini Dar es Salaam
 Mwenyekiti wa Yanga Yusufu Manji akisalimiana na Waandishi wa Habari jijini Dar ess Salaam katika kituo cha Polisi KatiNo comments: